Hivi unamfahamu mtu mjinga kuliko wote? Ona hii

Hivi unamfahamu mtu mjinga kuliko wote? Ona hii

Mkuu mambo ya bahat nasibu ni sawa na kudumbukiza sh kwenye maji,unaweza ukaipata au usiipate,
Sawa, ila utadumbukiza mara ngapi hizo sh zako kwenye maji? huku ukitegemea kushinda wakati uhalisia ni kua unazidi kumtajirisha muhindi.
 
Yaani hawa wamekuja kutulemaza kiakili mtu hafanyi kazi anasubiri bahati nasibu eti ndoto zake zitimie kweli ni maajabu.
 
Watu wanashindwa kuelewa tu lakini mafanikio yana siri ndogo tu ambayo hata mm siijui ndio mana bado masikini

[emoji3][emoji3][emoji3] ulitaka nikudanganye?
 
Ukianza kuBet unapata arosto km vile kubwia unga .Kuacha inahitaji ushauru nasaha.Hiyo ni roho toka kuzimu!
 
View attachment 682895


Hii nimeikuta mahali nami nikaamua kushare nanyi.

Mjinga ni vibarua Milioni moja wanao changa Tsh. 500 kila siku sawa na 500,000,000/= ambayo ni (Blioni 1.5) kwa mwezi na kumpa bilionea ambaye baadae huwashukuru kwa kumchagua kibarua mmoja na kumpa milioni 10 kama shukrani tena baada ya wiki.

Nadhani wale wakali wa KUBETI wanaweza kulithibitisha hili zaidi yangu.

Kundi kubwa la vijana limeendelea kuwa masikini kwa tamaa ya kupata utajiri wa haraka wakidhani watakuwa miongoni mwa watakaochaguliwa wapewe hiyo M 10.

Hebu mkumbushe Kijana wa Africa kwamba hakuna utajiri wa ghafla.
Ili aondokane na ndoto za kuwa bilionea kwa Kubeti. Mwambie aache kuibiwa kwa faida ya wachache.

Ukiachana na hilo kijana huyu anakuwa pia hajasalimika mbele ya mola wake ambae amemkataza yeye kwa kumuharamishia kijana huyo kwa kucheza kamari.

Mwenye zimungu anasema katika Quran katika suratul maida aya 90

( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ )

المائدة (90) Al-Maaida

Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.

Sasa Allah anatumbia vijana wa kiislam "Basi jiepusheni navyo ili mpate kufanikiwa, sasa wewe kijana wa kiislam acha kabisaa kucheza kamari, kwasababu aliekuumba amekukataza.

KUBET NI HARAMU, MUOGOPE MUNGU WAKO
Tutabeti milele daima! Kuna watu wanasomesha watoto kwa hela ya kubeti, kuna watu wamejenga nyumba kwa hela ya kubeti mm nina Altezza nimenunua kwa kubeti kitu kama hukijui ni heri ukae kimya [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Wivu umekujaa mtoto wa kiume yani unaona watu wakibeti wanafaiiiidi ukiona mtu anabeti analiwa ujue huyo kaanza juzi
 
Halafu nani kawadanganya kubeti ni Bahati nasibu? Hivi Barcelona akicheza na Las palmas unafikiri kushinda ka Barcelona ni Bahati nasibu? Man city akicheza na Stoke city hivi unadhani man city kushinda ni bahati nasibu? Bahati nasibu ni Biko na Tatu mzuka ila kubeti kuacheni kama kulivyo tena msiingilie kabisa eti tena mnakuja na vifungu vya vitabu vitakatifu, yani watu Wanafirana huko daily hamuwaoni? Ila kubeti ndo mnaona dhambi kubwa
 
Back
Top Bottom