Hii nimeikuta mahali nami nikaamua kushare nanyi.
Wajinga ni vibarua Milioni moja wanao changa Tsh. 500 kila siku sawa na 500,000,000/= ambayo ni (Blioni 1.5) kwa mwezi na kumpa bilionea ambaye baadae huwashukuru kwa kumchagua kibarua mmoja na kumpa milioni 10 kama shukrani tena baada ya wiki.
Nadhani wale wakali wa KUBETI wanaweza kulithibitisha hili zaidi yangu.
Kundi kubwa la vijana limeendelea kuwa masikini kwa tamaa ya kupata utajiri wa haraka wakidhani watakuwa miongoni mwa watakaochaguliwa wapewe hiyo M 10.
Hebu mkumbushe Kijana wa Africa kwamba hakuna utajiri wa ghafla.
Ili aondokane na ndoto za kuwa bilionea kwa Kubeti. Mwambie aache kuibiwa kwa faida ya wachache.
Ukiachana na hilo kijana huyu anakuwa pia hajasalimika mbele ya mola wake ambae amemkataza yeye kwa kumuharamishia kijana huyo kwa kucheza kamari.
Mwenye zimungu anasema katika Quran katika suratul maida aya 90
( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ )
المائدة (90) Al-Maaida
Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.
Sasa Allah anatumbia vijana wa kiislam "Basi jiepusheni navyo ili mpate kufanikiwa, sasa wewe kijana wa kiislam acha kabisaa kucheza kamari, kwasababu aliekuumba amekukataza.
KUBET NI HARAMU, MUOGOPE MUNGU WAKO