Kwanza niseme jambo moja... na hili nilizungumza tangu nilipoleta uzi wa awali kabisa wa post ya Sallam.
Ninachotaka kusema ni kwamba, Sallam needs to act as a man! Kama nilivyosema hapo awali, tatizo la Sallam sio mvumilivu! Ni utoto kama sio ujinga kumjia juu Ruge kwavile tu Ruge aliwaambia SHILAWADU wakashitaki!
Aidha, ni ujinga pia kudai SHILAWADU walienda kwa Mose kama namna ya kutaka kumshusha Diamond kwa sababu, umbeya ndio unawaweka mjini SHILAWADU na hii wala sio mara ya kwanza SHILAWADU kum-target Diamond Platnumz binafsi let alone Dancer wake!!
Hofu yangu ni kwamba, huenda Sallam ame-panic kuona promo za Aslay! Lakini kwa wanaowafahamu Clouds, hivi ndivyo wanavyofanya wanapokuwa na project na msanii fulani! Kama tunakumbuka, walim-promote sana Ali Kiba na Seduce Me yake kwa ajili ya Fiesta hadi wengine wakafikia kuongea kama tunayoongea sasa kwamba wanam-promote sana Kiba ili kumdondosha Diamond!
Project iliyopo mbele ya Clouds hivi sasa ni ya Nandy na Aslya, mosi kwa ajili ya Valentine na pili, kwa ajili ya Show itakayofanyika Escape I hapo February 17.
Now back to the topic.... hivi hao Clouds wanamshushaje shushaje Diamond Platnumz?!
Asilimia kubwa ya Wana-Bongo Flavor, wanakodolea sana macho Fiesta na ndio maana inapofika karibu na Fiesta, wasanii wengi wanaachia ngoma mpya ili kutega Fiesta (Puuzeni wanaosema Fiesta wanalipa 500K... kwa majority ya wasanii, Fiesta ni msimu wa mavuno).
Lakini wakati wengine huwa wanaitolea macho Fiesta, Diamond Platnumz sio mtu wa Fiesta tena! Sio mtu wa After School Bash! Sio mtu wa majority of the shows zinazoandaliwa hapa Tanzania!
That said, huwezi kumtisha Diamond kwa Fiesta!!!
Wengi wanataja power ya media... ni kweli kabisa na hapa nishasema sana hili! Hata hivyo, hiyo power ya media inategemea! Diamond leo hii anaweza kuishi raha mustarehe kwa kutegemea mashabiki wa Kenya peke yake ambako Clouds wala haifiki!
Tena hawa mashabiki wa Kenya, kv Wakenya wengi pia wapo ughaibuni, ndio wanunuzi wakubwa wa muziki online kuliko Watanzania!
Diamond leo hii ngoma zake zinapigwa throughout East & Central Africa na wala sio kwamba hizo nyimbo wanazipata kutokea Clouds.
Dakika kadhaa zilizopita nimeweka habari za uzushi zilizoripotiwa huko Ghana kwamba Diamond amefariki kwa ajali ya gari. Ukiangalia Waghana walivyo more concerned huko Twitter, ndipo utakapojua nguvu aliyonayo Diamond barani Afrika!
So, ili kumshusha Diamond unatakiwa kuwa na misuli ya kupiga fitina sio tu Tanzania bali Afrika Mashariki Yote especially Kenya & Rwanda and the rest of Afrika!!
Utakapojua nguvu ya Diamond, kwa kawaida huwa anaachia video Youtube usiku hata kabla hajafanya media tours! Na hadi anafanya tour, mara nyingi anakuwa tayari keshavuna Views zaidi ya 1 Million!!
Hiyo maana yake ni kwamba, tayari ana angalau Fans 1 Million ambao wala hawana muda wa kusubiria radio au tv ya mwananchi yeyote toka popote pale duniani!!
Sasa unapiga vipi fitina kwa wote hao?!
So, ingawaje media zina uwezo wa kumshusha msanii lakini kwa Diamond is kinda too late! Wanaweza tu kumtikisa lakini sio kumdondosha!
NOTE: Kama kuna msanii yeyote humu JF, please, don't be blinded by this post... hapa ni Diamond lakini kwa wewe, utadondoshwa tu kwa sababu huna base yoyote ya maana ya kuweza kushindana na watu kama Clouds!!!