Hivi unaweza kuwa na akili timamu ukakubali baba yako mzazi auze samaki akiwa na umri wa miaka 92 na ukakubali alalie mkeka?

Hivi unaweza kuwa na akili timamu ukakubali baba yako mzazi auze samaki akiwa na umri wa miaka 92 na ukakubali alalie mkeka?

Ssasa kama hela zakw yeye ujana wake alizitumia kula Pombe kuvua Wanawake Vyupi kwa idadi nyingi tena akitamba mtaani unataka Badae aje kul hela za nani bure??

Maisha ni kujipanga. Ule za kwako bata harafu sisi tuliojinyima uje kutulilia huruma?
Kwenye Post #32 Hilo Gazeti Linazungumzia Watanzania Kama Wewe KwA Mujibu Wa Huo Utafiti.
 
Wazee wengine waone tu hivyo hivyo,huwezi kujuwa watoto wake walipitia nini katika makuzi yao na huyo mzee,ndiyo maana kuna baadhi ya watoto wakiondoka nyumbani hawarudi labda kuwe na jambo linalomlazimisha kurudi hapo nyumbani,lakini hivi hivi kama kuenda kusalimia ni uwongo.
 
Jukumu la kuwa na maisha mazuri ni wewe mwenyewe mzazi (baba). Huwezi kuwalaumu watoto wakujengee nyumba na kukupa maisha mazuri wakati wewe kipindi cha ujana wako ulishindwa kutengeneza maisha mazuri. Kuwa na watoto siyo kigezo cha mwanaume kuwa masikini (tengeneza kipato)
Watu hasa sisi wanaume tukiwa kwenye ujana tunaendekeza, pombe, wanawake na anasa zisizo na maana. Mimi kama mwanaume siwezi kuwategemea watoto wanipe maisha mazuri hilo ni jukumu langu
Mzazi Akosei.
Sasa Watoto Umewazaa Wa Nini?
Kwa Mujibu Wa Uislamu
Watoto Na Mali Zao Vyote Ni Mali Ya Baba.
 
Kuna mzee miaka kama 80 hapa jirani anauza samaki Deepsea yaani hata nyuma ni chakavu imepigwa bati upande mmoja ,hamna sakafu wala nn ...Ana watoto wakubwa ,mmojq ni muhasibu kaajiriwa huko Mbeya hajawahi kurudi na mwingine yuko Tanga ana nyumba kama tatu ; mbili kapangisha ...Ila mzee ni jihad anapamba mwenyewe .
Usikute alipambana watoto waende shule akasahau kuwekeza
 
Mimi sijawahi kuishi na mama yangu karibia miaka 15 yaani ile hakuna kuonana wala hakuwahi kunipigia simu ,but nilivyomake mambo yangu nikamchek mpaka sasa anakula posho kila mwisho wa mwezi ila hakuwa na shobo na mimi kabisa.
Baba umemtelekeza
 
Kuuza samaki au kujishughulisha sishangai maana pia ni sehemu ya kuondoa Stress.....Ila kulalia mkeka haijakaa vizuri....Ijapokuwa uwezi elewa maana kwa hali ilivyo sasa wemgi tunafanya kazi lakini hakuna tunachopata......Unaweza ukashangaa huyo mzee anayeuza samaki anawapatia fedha wanae kwa kuwainea huruma ma maisha yao yalivyo magumu
 
Wazee wengine waone tu hivyo hivyo,huwezi kujuwa watoto wake walipitia nini katika makuzi yao na huyo mzee,ndiyo maana kuna baadhi ya watoto wakiondoka nyumbani hawarudi labda kuwe na jambo linalomlazimisha kurudi hapo nyumbani,lakini hivi hivi kama kuenda kusalimia ni uwongo.
Mkuu sio sababu kabisa hiyo. Ni kukosa utu tu.

Babu yetu kizaa bab alimkataa mzee wetu na kama haitoshi akamtimua bibi alipokua mzee akapelekwa ujombani akasoma huko hadi la darasa la 4 na kuajiriwa ualimu.

Baba akamuuliza bibi (mama yake) amwambie ukweli baba yake halisi ni nani na kwanini babu alimkataa.
Bibi akamwambia baba yako ni huyuhuyu hakuna mwingine.

Babu wale watoto wote aliozaa na mwanamke mwingine baada ya kumtimua bibi hakusoma hata mmoja.Hivyo alipozeeka mbaya zaidi aliugua alikuja kwa mzee zaidi ya miaka7 tupo nae na mzee alimjari mno hadi umauti ulimkuta akafariki akiwa kwetu na umri wa miaka 97.

Japo alikuwa amesema akifa apelekwe akazikwe karibu na mke wake mdogo maana ndiye alitangulia.Mzee alifanya hivyo na sisu ndo ikawa mara ya kwanza kwenda kuonana na watoto wenzetu watoto wa akina baba mdogo.

Wengine walikuja kusomea kwetu baada ya msiba wa babu yaani tulipo fahaamiana na hata sasa tupo wamoja mno.

Hiki ni kisa cha familia yetu wenyewe mimi nimeanza kuwaona baba wadogo kipindi babu alipokuja nyumbani nikiwa form2. Hata mzee hakuwa kutuambia kwenda kule kumsalimia babu
 
Ni hivi babako au mamako waliokuzaa ni sura yako.hivyo hata kama hukubaliani na tabia zao,huna wazazi wengine ya hao.Kama ukiweza wape kila aina ya msaada na watu wataona na kukubariki.Mungu hapangiwi ratiba zake
 
Back
Top Bottom