Hivi unawezaje kula chakula huku unawashwa?

Hivi unawezaje kula chakula huku unawashwa?

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Unakuta mtu ananunua chakula kwa pesa aliyoitafuta kwa shida halafu anaweka pilipili kwenye mboga kiasi kwamba jicho linakuwa nyanya, jekunduuuu! Muda huo anakula huku ametumbua macho na kuachama (kuacha mdomo wazi) ili hewa ya oksijeni iupooze mdomo, muda huo lips zimekuwa tomato! Zimedoda mpaka basi. Kikohozi na mafua ya rasha rasha ya hapa na pale yakimtoka bila huruma, yeye ni humu tu huku akijifuta pua kwa kiwiko cha mkono. Hela ni yako, kwanini ujipe mateso wakati kula ni starehe. Hauna tofauti na mwanaume anayepakaa mkongo ili akafanye mapenzi

Ila suluhisho la haya yote ni 2025
Na hili nalo serikali ikalitizame kwa jicho la upembuzi
 
Chakula chenyewe unakipata kwa shida bado unaongeza pilipili
 
HILI NALO MKALITAZAME.

Namuagiza Bashite aunde tume ya kuchunguza jambo hili ili tupate muafaka kama Taifa.
 
Siku hizi pilipili na malimau/ndimu sitii kwenye supu, naona inaniharibia ladha halisi ya supu. Tena supu yenyewe iwe ya utumbo usiokamuliwa kisawasawa uwe na mabaki ya kinyesikinyesi cha ngombe, mbuzi au kondoo itakuwa na ladha halisi ya supu
 
Pilipili inaongeza joto mwilini pia ashiki ya Tendo...Vijana wajuaji wa bongo

. HA!HA!HA
 
Nimeanza kutumia pilipili tangia nikiwa 7yo, saiz naitumia marachache kwa sababu ya gastric ulcers.
 
Nahisi kuna jambo unataka kulizungumza hapa ila unajishuku. Zungumza tu mkuu tuone tunalitatua vipi
. Hapana mkuu, kipindi Nimeenda tanga jamiu ya kule walikuwa wanashanga ninavyokula pilipili moja alafu naimaliza..

. Wakawa waniuliza "kwa nini unakula kitu kinachowasha" ???
 
Back
Top Bottom