Hivi UTI ni Ugonjwa Mpya au ni Jina tu Limebadilika?

African Believer

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
436
Reaction score
426
Habari Wana JF!

Nimekuja na swali la kitabibu na natumai wana Jf wenye ufahamu juu ya hilo watanipatia majibu stahiki.

Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na kuenea kama si kukua kwa ungojwa unaojulikana kama Urinary Tract Infection (UTI). Kama itakuwa ni mimi pekee ninayeliona hilo kwa kutokufahamu kwangu naomba mnisamehe.

Mara nyingi mtu alipohisi kuwa na dalili kama za homa, kuchoka, kuumwa kichwa pamoja na kukosa hamu ya kula au kutapika alijihisi huenda ana malaria. Na mara nyingi kwa kipindi cha miaka ya nyuma mtu angeenda kupima akiwa na dalili hizo angeambiwa ana malaria au typhoid jambo ambalo kwa sasa ni tofauti.

Kwa sasa hali imekuwa ni tofauti kabisa kwani kila ukijihisi una homa na ukaenda hospitali au kituo cha afya kujicheak mara nyingi utaambiwa una UTI, na hili hutokea mara nyingi kwa vituo vya afya na hospitali binafsi.

Swali langu ni je, ugonjwa wa UTI umeanza siku za karibuni au ni Jina tu limebadilika? Au ni nini basi kimetokea?

Wanajamvi naombeni jibu.
 
Hata mi nashangaa eti mtoto wakiume naenda kupima homa imenikamata nambiwa UTI wakat zaman walikua nao madem tena huwez kuskia mtu anaugua akalazwe nadhan mashetwan wamevirenew vidudu vyahuu ugonjwa saiv uko updated
 
Tatizo haya maboxer tunayovaa mtu unalivaa siku tatu hujalifua lazima upate UTI
 
Hospitali nyingi huwa wanabase kwenye biashara , muda mwingine wanakupa ugonjwa ambao sio wauze tu , nimeshawahi pima malaria sehemu tatu tofauti ndani ya masaa kumi na mbili na kila sehemu majibu yalikuwa tofaiti , nilipima pharmacy na vile vipimo vya fasta wakaniambia sina malaria , baadae nikaenda hispital nikaambiwa nina malaria kumi na nane , nikaona hii sio nikaenda hospital nyingine malaria mbili . Juzi kati nimepima malaria na typhoid dokta akataka kuniambia nina uti nikamuuliza kupima damu na uti wapi na wapi akazuga zuga ikaishia hapo.
 
Inawezekana kwenye mitaala mipya ya utabibu wanafundisha sana hii UTI, maana sasa hadi wanaume tunaambiwa tuna UTI, sasa sijui ni ugonjwa mpya au ni kundi fulani la magonjwa wameamua kuliita UTI kwa pamoja ili kujirahisishia kazi
 
Tatizo haya maboxer tunayovaa mtu unalivaa siku tatu hujalifua lazima upate UTI
Mbona kipindi cha nyuma haikuwa hivyo? Siku hizi kila unapojisikia vibaya ukienda kupima utakutwa na UTI au ndiyo kusema tumezidi kuwa wachafu?
 
Inawezekana kwenye mitaala mipya ya utabibu wanafundisha sana hii UTI, maana sasa hadi wanaume tunaambiwa tuna UTI, sasa sijui ni ugonjwa mpya au ni kundi fulani la magonjwa wameamua kuliita UTI kwa pamoja ili kujirahisishia kazi
 
Inawezekana kwenye mitaala mipya ya utabibu wanafundisha sana hii UTI, maana sasa hadi wanaume tunaambiwa tuna UTI, sasa sijui ni ugonjwa mpya au ni kundi fulani la magonjwa wameamua kuliita UTI kwa pamoja ili kujirahisishia kazi
Hata mimi nahisi hivyo.
 
UTI ni kifupi cha maneno URINARY TRACT INFECTION
Ni maambukizi kwenye njia ya mkojo na jinsia zote mbili tunaweza kupata haya maambukizi.
Zamani walikuwa hawauhesabu kama ugonjwa ila ni maambukizi tu ila kutokana na mabadiliko ya mitaala ndo wakaamua kuutambua kama ni ugonjwa ila zamani ulikuwa ukionekana na UTI daktari anakwambia una mkojo mchafu
 
At least sasa naanza kupata picha, kwani imekua balaa!
 
Wanaume wapiga 0713 na wale wenye vibamia wapo kwenye hatar kubwa ya kupata maambukizi
 
At least sasa naanza kupata picha, kwani imekua balaa!
kingine mkuu dalili za malaria,typhoid na uti zinafanana sana kwa hiyo muhimu ukijisikia tu homa,uchovu,kichwa kuuma n.k basi wahi kupima hayo magonjwa matatu.
pia wengi hudhani UTI ni ugonjwa wa zinaa kwa sababu moja ya njia za maambukizi ya ugonjwa huu ni kupitia kujamiiana kati ya mwanaume na mwanamke. lakini kinachotokea ni kuwa wanaume kibailojia njia zetu za mkojo na ile ya kupitishia shahawa zimeungana na kuwa njia moja kuanzia kwenye shina la uume ndio maana tunakojoa na kumwaga shahawa kwa kutumia uume. ila kwa wanawake ni tofauti kidogo wao njia ya uzazi na njia ya mkojo ziko tofauti.

kingine ni kuwa wanawake wapo kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya ugonjwa huu kuliko wanaume na sababu ni kuwa wanawake huwa wanachuchumaa wakati wanakojoa tofauti na wanaume kwa hiyo kama choo kimetumiwa punde na mwathirika wa uti na hakijasafishwa vizuri basi ni rahisi kwa mwanamke kupata uti.

njia kuu za maambukizi ya uti ni ngono zembe na kushare choo kichafu.
samahani kwa mwandiko wa weekend.
 
Asante sana kwa maelezo mazuri.
 
Back
Top Bottom