African Believer
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 436
- 426
Habari Wana JF!
Nimekuja na swali la kitabibu na natumai wana Jf wenye ufahamu juu ya hilo watanipatia majibu stahiki.
Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na kuenea kama si kukua kwa ungojwa unaojulikana kama Urinary Tract Infection (UTI). Kama itakuwa ni mimi pekee ninayeliona hilo kwa kutokufahamu kwangu naomba mnisamehe.
Mara nyingi mtu alipohisi kuwa na dalili kama za homa, kuchoka, kuumwa kichwa pamoja na kukosa hamu ya kula au kutapika alijihisi huenda ana malaria. Na mara nyingi kwa kipindi cha miaka ya nyuma mtu angeenda kupima akiwa na dalili hizo angeambiwa ana malaria au typhoid jambo ambalo kwa sasa ni tofauti.
Kwa sasa hali imekuwa ni tofauti kabisa kwani kila ukijihisi una homa na ukaenda hospitali au kituo cha afya kujicheak mara nyingi utaambiwa una UTI, na hili hutokea mara nyingi kwa vituo vya afya na hospitali binafsi.
Swali langu ni je, ugonjwa wa UTI umeanza siku za karibuni au ni Jina tu limebadilika? Au ni nini basi kimetokea?
Wanajamvi naombeni jibu.