secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 2,998
- 4,948
Habari ya kutwa nzima wana jamvi.
Jioni ya Leo Majira ya saa maja jioni nimeshangaa sana baada ya kuangalia angani upande wa mashariki na kuona vitu mithili ya nyota vikipita, ukivichunguza kwa makini vitu vile utagundua kuwa vimeungana na kutengeneza kitu kama mnyororo unaojongea.
Ili kujiridhisha kuwa nilichokiona ni kweli ama Niko ndatoni nilimpigia jamaa yangu mmoja anayepatikana mkoa mwingine na nikamwuliza kama aliona naye alikiri kuwa ameona na kwamba ameshangazwa sana na kile alichokiona.
Katika harakati za kutaka kujua kiundani nilichokiona niliamua kuwauliza watu tofati tofauti, wakubwa kwa wadogo, wake kwa waume, Watu wa Mungu na wasio wa mungu lakini sikupata majibu yaliyoniridhisha.
Kilichonituma niwaulize wana JF ni majibu niliyopewa na mchungungaji wa kanisa moja lililoko karibu na ninakoishi, yeye alidai kuwa "SIKU ZA MWISHO ZIMEKARIBIA"🤣🤣🤣.
Hivyo basi kama kuna mtu aliyeona kike kilichotokea jioni ya Leo basi atueleze ni nini maana majibu ya mchungungaji sikuyasadiki na sipendi kuyasadiki.
Karibuni.