Hivi! Viongozi wetu huwa hawatamani watanzania wafe ili wawepo wao tu?

Hivi! Viongozi wetu huwa hawatamani watanzania wafe ili wawepo wao tu?

Trable

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2023
Posts
1,781
Reaction score
3,288
Hisia zangu kwa sasa ni kwamba!

Tumekuwa nchi yenye viongozi wanaotamani waishi kama maisha ya kama wako peponi na kuwadharau kabisa wanaowafanya wafikie hatua ya kuishi hivyo, watu has ni, walipa kodi na masikini kabisa ambao wanaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu!

Watu hawa wanyonge na wazalendo wa kulipa kodi, kila sheria inayohusu kodi na kulipa kodi, haijawabagua, tofauti kabisa na viongozi ambao wengi wao, sheria hiyo imewaruka kwa sababu wanazojua wao wenyewe!

Viongozi wa watu hawa masikini, huwenda wanatamani kabisa wanyonge hawa na masikini, wasiwepo kabisa katika uso huu wa dunia, ni bahati mbaya tu kwamba, hawana uwezo wa kuiondoa pumzi ndani yao, kwa sababu tu, anayewafanya waishi hawa masikini, sio wao, bali ni Mwenye kuwapa uhai watu wote yaani(Jehova) (Mola) muumbaji wa vyote

Bajeti ya serikali, Karibu asilimia kubwa si ya kurudisha maendeleo kwa walipa kodi, bali inagharamia maisha mazuri ya viongozi wao,

Utasikia, serikali imetenga kununua magari mapya elfu ngapi huko, magari ambayo moja tu linauzwa nusu bilioni na......

Magari hayo hayo yanayotumia pesa nyingi za walipa kodi, mengine mengi yanaishia kwa watu binafsi! Hii inauma sana

Utasikia, serikali imetenga bilioni sijui ngapi kugharamia safari za viongozi, bilioni kadhaa kugharamia seminar, bilioni kadhaa kugharamia posho za viongozi, seminar na warsha mbalimbali

Tukirudi kwenye masuala jumuishi ya kijamii!

Hakuna hata kiongozi mmoja anayeonyesha kukerwa na gharama za matibabu,

Gharama hizi za matibabu kuendelea kupanda, sio mpango wa viongozi hawa waliolewa na kodi wa watanzania kuwaona watanzania hawa wameshindwa kujitibu na ili wafe?

Kwenye suala hili, ni dhahiri kwamba, viongozi wetu ni kama wako kwenye kuwatakia kufa wananchi!
 
Back
Top Bottom