Hivi Vitambulisho vya Magufuli vina lengo gani?

Hivi Vitambulisho vya Magufuli vina lengo gani?

Hapo atakusanya fedha nyingi sana, jumla vitambulisho ni 670,000 ukizidisha bei ya kila kitambulisho sh 20,000 utapata jumla ya Tsh 13,400,000,000, fedha nyingi sana. Halafu mjasiriamali anayemlenga ni yupi hasa. Maana wafanyabiashara wengi wenye mtaji wa milioni 4 tayari wanalipa kodi TRA na wana leseni za biashara.
Hii elfu ishirini ni kwa mwaka au ukishanunua hicho kitambulisho ndo basi?
 
Sijamuelewa Rais huyu anataka nini hadi kutuletea vitambulisho vyake. Mamlaka zinazohusika zilimpiga chini kwa matakwa yake ya vitambulisho visivyo kisheria. Anataka nini hasa, atutambue au anataka pesa ya kitambulisho?
Eti mwenye mtaji wa chini ya Mln 4 ndo awe nacho, nani anajua kama mimi mtaji wangu upo chinivya Mln 4?
Kodi ya kichwa hiyo muulize babu yako enzi ya ukoloni ilikuwepo, mwaka wa kwanza rahisi, mwaka wa pili TRA wakiingia kijijini wote manakimbilia msituni
 
Ninachowaza hapa ni kwamba anataka kwanza hawa wafanyabiashara wadogo wadogo wasibugudhiwe.

Pili serikali itaweza kujua, ni wananchi wangapi biashara zao zipo katika level ya chini. Hili litasaidia serikali kutengeneza program maalumu za kuwaendeleza ili waweze kukuza mitaji yao na hatimaye kulipa kodi
 
Kuna watu hapa watakuwa na fremu wanapanga vitu vichache dukani mzigo wa maana unakaa store , ,afu wanavaa na Vitambulisho vyao
 
Back
Top Bottom