Hivi Vodacom wanajitambua kweli?

Hivi Vodacom wanajitambua kweli?

Majwahis

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
575
Reaction score
545
Vodacom mnatuboa sana sisi wateja wenu! Kila siku mnanitumia msg tuma hela Leo kwa m-pesa upate mb 2 za bure!!!! Mara ukivuta zaidi ya sh.20,000/- kutoka bank kwenda m-pesa yako utapata dk. 2 bure za maongezi!!!.

Mara ukinunua kifurushi chochote Leo utapata dk,1 bure!! Nk. Sasa haya mambo yenu ya kitoto wateja mnatusumbua mno! Hivi tangy lini kd 1 au 2 au mb2 ziliwahi msaidia mtu?

Kuweni wastaarabu basi mjue hao mnao watumia msg za kichovu namna hiyo wengine ndiyo wenye share kubwa huko vodacom! Wengine ni matajiri/viongozi wakubwa!

Hamuonagi aibu? Mnaboa sana!.
 
Jifunze kupotezea mambo mkuu utaishi kwa amani Sana
Mm nkiona massage yoyote ya mtandao wa simu uwa nafuta tu siitaj hata kusoma
Sijui
MPESA
SONGESHA
VODACOM
MPAWA
POLISI
TCRA

WE FUTAAA

[emoji23][emoji23]
 
Ukiona unatumiwa meseji za kichovu jua na laini yako ndio iko hivyohivyo. Kuna wateja vodacom hawathubutu kuwatumia meseji za namna hiyo
 
Jifunze kupotezea mambo mkuu utaishi kwa amani Sana
Mm nkiona massage yoyote ya mtandao wa simu uwa nafuta tu siitaj hata kusoma
Sijui
MPESA
SONGESHA
VODACOM
MPAWA
POLISI
TCRA

WE FUTAAA
Kuna mambi siyo ya kupotezea, wanaudhi sana voda. Toka asubuhi hadi jioni ni mimeseji ya matangazo, tene usiombe unasubiria kahela toka sehemu, sms ikiingia unaangalia kwa hamu unashangaa ni voda. Kuna siku wanapiga hadi simu ?

Hizi ni kero kwa wateja, hamna nanmna ya kuset waache masms ya ofa na matangazo?
 
Voda wapo vizuri itakuwa wanaangalia na ntu na ntu mkuu binafsi nikiongeza salio hata la jero tu napewa dk 5 bure! We komaa na hizo dk moja zako..😂
 
Ata TiGo pia tunatatizo ilo, kwa siku napokea sms adi 15 za mtandao, heri ya Airtel wako simple tatizo network ya hovyo sijawai kuona
Voda ktk huduma kwangu ni namba moja sema internet spidi wanazingua halotel ndo babalao kwenye internet..
 
Mkuu shida ni pale tuna-accept terms & conditions ktk usajili. Unakuta umekubali promotional terms.
 
Vodacom wanaongoza kutuma ma sms ya kipuuzi sana, sijui yakoje haya majitu na server zao! Kuna muda nawaza hivi hii style yao ya marketing ndio wasomi wenzetu wamekaa wakawaza? Huu ni upuuzi sana!
 
Back
Top Bottom