Hivi Wabunge wetu hawa hutumia muda gani kutafakari mambo, muda wote ni makofi na kuimba tu

Hivi Wabunge wetu hawa hutumia muda gani kutafakari mambo, muda wote ni makofi na kuimba tu

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2016
Posts
1,770
Reaction score
5,423
Mimi ni mfuatiliaji wa mabunge mbalimbali duniani.

Katika mabunge makini ninayoyafuatilia huo naona panapofanyika mawasilisho (submissions),Wabunge huwa watulivu na wenye kutafakari mambo (digest issues).

Sisi wabunge wetu hapo ni kupiga meza (makofi),kucheka na hata kuimba muda wote! Do we real have serious and competent MPs as a Country? Or group of mediocres paid to represent their stomaches?

Bajeti tegemezi,Serikali inakopa hadi Wananchi tunaogopa lakini Wabunge wetu ni vicheko hadi meno 32 yote yako nje!

Hii Nchi siyo bure kuna shida mahali.

Haiwezekani tuwe na rasilimali nyingi hivi lakini tuwe na watu " mandondocha" hivi.
 
Mkuu hao watu huwa hata hawafuatilii nini kinaendelea ndio maana kuna vitu wanapitishaga hata wenyewe wakiwa nje wanashangaa .
 
Back
Top Bottom