Hivi wafanyabiashara wenzangu, mliwezaje kudeal na mpinzani wako ambaye kakuzidi kila kitu!

Ngoja nikufundishe polepole utaelewa inavyoonekana wewe una uwezo mdogo wa kujiongeza unaishi kwa kukariri,ukishaona kichwa chako kipo hivyo wewe hufai kuwa mfanyabiashara maana biashara haikubembelezi ukibweteka utaa
mbulia sifuri na wenzako wanauza kama kawaida.
Haya chukulia mama ntilie alikuwa ananunua mchele kwa mangi kwa bei ya 1800 kwa kilo moja wewe unaenda kumwambia nitakuuzia kwa 1600 hii nayo hadi upelekwe shule kujiongeza?
Yani maelezo meeeeengiiii halafu unaandika upuuzi tupu. Nadhani majibu ya wadau yametosha kukutoa ujinga.

Mchele wa 1,800 ukipata 200 ni biashara haswa. Sasa kumshauri atoe faida si atakuwa anafanya biashara kichaa. Na itakuwa ni kutangaza vita vya angani, majini na nchi kavu kwa mpinzani wake.

Bora mara mia ushauri uweke bidhaa kama mafuta ya kupikia, sukari, chumvi nk kama mpinzani wake hana ili kuwavuta mamantilie. Afu aviuze kwa bei ya chini kidogo.
 
Ishu ni kuamini katika mungu ndumba sio nzuri mfanyabiashara mbaya analoga ila mfanyabiashara mzuri anaomba na kusali katika imani yake karma is a biitch kama umemkuta kaanza kabla yako jifunze kwake kama mko sawa mshauriane
Hakuna mfanyabiashara jilani/mpinzani wako atakupa his/her business secrets ili upambane nae mzee. Hizi porojo ebu tuziacheni.

Labda aongee na mtu aliye mbali nae. Ambae hana mgongano nae wa masirahi at least ampe siri za chimbo analochukulia mzigo kwa bei sahihi ila sio mshindane wake.
 
Dah nahangaika sana mwezi wa tatu huu nimeagiza trip 4 na zote nimekula loss nauza kwa bei ambayo soko linahitajii ukisema uweke faida yako huuzi hupatiii wateja mpka inafikia stage nataka kukata tamaaa aisee. tena muda mwingine unaenda shamba unarud na mchele uuze labda 1500 afu unakuta wafanyabiashra wengine mchele unaotaka kuuza 1500 wao wanauza 1300 mpka unajiuliza hawa watu wanachukua wapiii mzgo naumiza kichwa mamamke hadiii nahisii kuumwa
Wengine ni magiant mzee, wanamitaji. Unakuta alichukua mzigo let's say mwezi wa 5 bei ilikuwa 1,000 kg. Anaweka store then anapush miezi miwili baadae, anaochukua mwezi wa huu kwa 1,400 anauza wa 9 kwa 1,800/1,900. By then we utachukua kwa 1,900 unataka uuze kwa 2,100.

Pia, kuna namna ulibugi kupick location. Kuna technic pia kwenye kuchagua location. Location ziko segment katika namna mbili.

A. Market place: hapa kunakuwa na wafanyabiashara wengi wa aina moja ya biashara. Kwa mfano motumba ilala. Advantage yake, hakuna mtu mwenye umiliki na mteja. Wateja wote wanakuwa ni wateja wa soko sio mtu mmoja. So bei na ubora wa bidhaa ndiyo vitakubeba.

B. Non market place: hapa ni mtu anatafuta sehemu ambayo haina biashara za mlengo mmoja anaweka Kambi (kama huyo jirani yako). Mara nyingi hapa wateja wanakuwa loyal sana kwa huyo mfanyabiashara. Kuwahamisha kipengele maana Kuna strong bond na mteja.

Kwa hiyo, watu wanaweza wakawa wanataka kabisa kuja kununua kwako lakini wanamuonea aibu jamaa hata kama bei zinalingana. Binafsi nahisi ungekuwa mbali nae ingekuwa rahisi kumuibia wateja.

Pia, nenda kesho kanisani ukatoe sadaka, au mtumie babu yako hela ya ulanzi kesho. Sio mnavamia shughuli za watu kiboyaboya tu.
 
Mimi ni mfanyabiashara wa nafaka hapa jijini Dar es Salaam. Sio mgeni katika kufanya biashara ila naweza sema ni mgeni katika kufanya biashara ya kwangu. Kwa sababu hapo awalii nilikuwa nafanya biashara za watu tuu.

Na sikujua kama biashara zina changamoto hivi hasa ukiwa wewe ndio mwenye biashara.

Mpaka sasa huu ni mwezi wa tatu nipo katika biashara yangu mpya ya nafaka nauza mchele na maharage nimepitia changamoto nyingi sana haswa matapelii, dalali kukutumia mzigo mbaya ambao unachukua kwa bei ya juu halafu ukifika sokoni lazima ukakate hela unauza bei ya chini kurudisha hela mda mwingine unaokoa tu hela. Changamoto ni nyingi kwakwelii ila sijakata tamaa napambana.

Sasa kuna hili swala.. ninapouza kuna jirani yangu naye anauza biashara kama yangu nimemkuta na inaonesha ana muda mrefu sana katika biashara, ana wateja wa kutosha na ana mtajii wa kutosha kiufupi kanizidii pakubwa sana.

Changamoto ipo kwenye wateja hivi wenzangu huwa mnahisi vipi mwenzako mmefungua duka sawa mna biashara zinazofanana ila chakushangaza mwenzako anauza gunia kumi asubuhi wewe ndo kwanza hata kilo moja hujauza 😁😁 mikokoteni inapaki kila muda plus mapikipiki muda wote hayakaukii yananunua mizigo pale wewe bado ngoma ngumuu.

Hivi wafanyabiashara wenzangu mliwezaje kudeal na mpinzani wako ambaye kakuzidiii kila kitu na ukizingatia wewe ndio kwanza unaanza ila miezi ndio hivyo mwezi watatu? Msaada wenu tafadhali

Nyongeza: Biashara ya mchele ni pasua kichwa sana walioweza sijui wanafanya vipi aiseee toka nimeanzaa faida siioni.

Nawatamani sana wateja wa jumla ila wanataka mchele mzuri halafu kwa bei mteremko bila kujua mimi nakochukua nachukua bei kubwa.

Swali lingine kwa wafanyabiashra wana mchele faida inabidi iwe sh ngapi kwa gunia kwa kawaida huenda mimi naweka faida kubwa halafu sijui.
Kabla ya kuanzisha biashara hiyo ilitakiwa uijue kwakufanya utafiti wa soko na nakuandika mpango wako wa biashara, (kufanya makosa kwenye makaratasi),
Jibu la swali lako fanya yafuatayo 1.yatambue mapungufu yako vs mapungufu ya mshindani wako
2.Nguvu za mpinzani wako vs nguvu zako
3. Wateja wa mpinzani wako ni wakina nani na wanaishi wapi
4.je unazitambua tabia za mjasiriamali aliyefanikiwa, (traits)
 
Hakuna mfanyabiashara jilani/mpinzani wako atakupa his/her business secrets ili upambane nae mzee. Hizi porojo ebu tuziacheni.

Labda aongee na mtu aliye mbali nae. Ambae hana mgongano nae wa masirahi at least ampe siri za chimbo analochukulia mzigo kwa bei sahihi ila sio mshindane wake.
Wewe una roho iyo mimi sina roho iyo kama ningekuwa mfanyabiashara
 
Yani maelezo meeeeengiiii halafu unaandika upuuzi tupu. Nadhani majibu ya wadau yametosha kukutoa ujinga.

Mchele wa 1,800 ukipata 200 ni biashara haswa. Sasa kumshauri atoe faida si atakuwa anafanya biashara kichaa. Na itakuwa ni kutangaza vita vya angani, majini na nchi kavu kwa mpinzani wake.

Bora mara mia ushauri uweke bidhaa kama mafuta ya kupikia, sukari, chumvi nk kama mpinzani wake hana ili kuwavuta mamantilie. Afu aviuze kwa bei ya chini kidogo.
Kuna kitu kimoja hivi wabongo wengi huwa tunafeli kwenye biashara,ya kufikiria faida ya leo tu ya haraka haraka, no future plans/no strategies.
Fahamu ya kwamba kutafuta wateja na kuwanasa ni mchakato mwingine na kupata faida ni mchakato mwingine.
Cha kwanza vuta wateja wakujue na kukuzoea na wakishakuzoea sasa weka bei unayoitaka yenye faida,usilazimishe kupata faida leo wakati ndio kwanza umeanza biashara na wateja hawakujui wala hawaijui huduma yako ikoje.
Ndio maana unashauriwa unapoanza biashara mbali na pesa ya mtaji hakikisha una pesa nyingine ya ziada kwa ajili ya kujikimu mahitaji yako binafsi kipindi ambacho biashara yako itakuwa haiingizi faida ili kupunguza presha ya kutaka faida kwa pupa.
Jambo lingine fikiria ndio umeanza biashara bei yako iko juu na wapinzani wako ambao ndio wenyeji kwenye gemu wanauza bei ya chini hapo maana yake biashara ishakushinda ni either ukafikirie biashara nyingine tofauti au urudishe mpira kwa kipa ukaajiriwe kwa muhindi,sasa unafikiri ni mteja gani mjinga aache kununua kwa muuzaji wake wa siku zote kwa bei ya chini aje kununua kwako kwa bei ya juu na haijui huduma yako,labda huyo mteja awe mke wako😀😄😄😄
 
Kwa hili nakubaliana na wewe. Lakini la kutoa 200 kwa kg hilo kipengere kiongozi.

Ni kweli angetenga at least 6months ya kusoma soko na kujijenga mwenyewe kibiashara. Ila sio ku'run kwa hasara.
 
Yani maelezo meeeeengiiii halafu unaandika upuuzi tupu. Nadhani majibu ya wadau yametosha kukutoa ujinga.

Mchele wa 1,800 ukipata 200 ni biashara haswa. Sasa kumshauri atoe faida si atakuwa anafanya biashara kichaa. Na itakuwa ni kutangaza vita vya angani, majini na nchi kavu kwa mpinzani wake.

Bora mara mia ushauri uweke bidhaa kama mafuta ya kupikia, sukari, chumvi nk kama mpinzani wake hana ili kuwavuta mamantilie. Afu aviuze kwa bei ya chini kidogo.

Punguza makasiriko ..

Jamaa Ametolea mfano tu ili jamaa aangalie anaweza ku apply vipi hii theory ya Punguzo kwenye bidhaa zake
 
H
Wengine ni magiant mzee, wanamitaji. Unakuta alichukua mzigo let's say mwezi wa 5 bei ilikuwa 1,000 kg. Anaweka store then anapush miezi miwili baadae, anaochukua mwezi wa huu kwa 1,400 anauza wa 9 kwa 1,800/1,900. By then we utachukua kwa 1,900 unataka uuze kwa 2,100.

Pia, kuna namna ulibugi kupick location. Kuna technic pia kwenye kuchagua location. Location ziko segment katika namna mbili.

A. Market place: hapa kunakuwa na wafanyabiashara wengi wa aina moja ya biashara. Kwa mfano motumba ilala. Advantage yake, hakuna mtu mwenye umiliki na mteja. Wateja wote wanakuwa ni wateja wa soko sio mtu mmoja. So bei na ubora wa bidhaa ndiyo vitakubeba.

B. Non market place: hapa ni mtu anatafuta sehemu ambayo haina biashara za mlengo mmoja anaweka Kambi (kama huyo jirani yako). Mara nyingi hapa wateja wanakuwa loyal sana kwa huyo mfanyabiashara. Kuwahamisha kipengele maana Kuna strong bond na mteja.

Kwa hiyo, watu wanaweza wakawa wanataka kabisa kuja kununua kwako lakini wanamuonea aibu jamaa hata kama bei zinalingana. Binafsi nahisi ungekuwa mbali nae ingekuwa rahisi kumuibia wateja.

Pia, nenda kesho kanisani ukatoe sadaka, au mtumie babu yako hela ya ulanzi kesho. Sio mnavamia shughuli za watu kiboyaboya tu.
Hapa umenena 👏
 
Kila nilichotaka kusema kimeshasemwa..nakazia tu

1. Tengeneza na wewe wateja wako kwa kuwafuata ukiwa na sampo na Bei Yako mfano mama ntilie, madukani n.k , ukisema uwasubiri dukani Itachukua muda mrefu

2. Kama ulivyosema Jaribu kusource mwenyewe direct kutoka mashambani au kwa wakulima au huko mashineni uone Kama utapata kwa Bei poa ili na wewe uweze kuweka Punguzo kuvutia wateja hii ni Kama chambo maana wewe ni mgeni kwenye soko ukilinganisha mshindani wako
 
Wengine ni magiant mzee, wanamitaji. Unakuta alichukua mzigo let's say mwezi wa 5 bei ilikuwa 1,000 kg. Anaweka store then anapush miezi miwili baadae, anaochukua mwezi wa huu kwa 1,400 anauza wa 9 kwa 1,800/1,900. By then we utachukua kwa 1,900 unataka uuze kwa 2,100.
Hili nalo ukalitizame aBuwash
 
Non market place: hapa ni mtu anatafuta sehemu ambayo haina biashara za mlengo mmoja anaweka Kambi (kama huyo jirani yako). Mara nyingi hapa wateja wanakuwa loyal sana kwa huyo mfanyabiashara. Kuwahamisha kipengele maana Kuna strong bond na mteja.

Kwa hiyo, watu wanaweza wakawa wanataka kabisa kuja kununua kwako lakini wanamuonea aibu jamaa hata kama bei zinalingana. Binafsi nahisi ungekuwa mbali nae ingekuwa rahisi kumuibia wateja.
Na hili pia ndugu aBuwash ukalitizame
 
Waheshimiwa, mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCO) nikisomea sheria.

Nimekuwa nikikumbana na changamoto kubwa za kifedha baada ya kukosa mkopo licha ya kuambatanisha nyaraka muhimu kama cheti cha kifo cha baba yangu.

Control number yangu ni TU233351786402
Jina Joseph Msehi
Nambà yangu ya simu 0741995421

Hali hii imenifanya nifikirie kusitisha masomo kwa muda kutokana na ugumu wa maisha.

Naomba msaada wenu kwa namna yoyote, hasa katika kulipia ada ya mwaka huu, au hata ushauri kuhusu njia bora ya kusonga mbele. Kwa taarifa, nilihitimu shule ya sekondari kwa daraja la kwanza.
 
Back
Top Bottom