DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 23,928
- 63,499
Ko unaiweka wapi hio chumvii yan maeneo gan katk biashara
Unazungushia ktk eneo la biashara then nyingine uneogea kabla ya kuingia ofisini kwako.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ko unaiweka wapi hio chumvii yan maeneo gan katk biashara
Jifunze kuwa Bora ktika huduma na kauli pia jaribu kuweka bei rafiki kujenga jina taratibu ili nawe uwe na wateja wako wa kudumu.Mimi ni mfanyabiashara wa nafaka hapa jijini Dar es Salaam. Sio mgeni katika kufanya biashara ila naweza sema ni mgeni katika kufanya biashara ya kwangu. Kwa sababu hapo awalii nilikuwa nafanya biashara za watu tuu.
Na sikujua kama biashara zina changamoto hivi hasa ukiwa wewe ndio mwenye biashara.
Mpaka sasa huu ni mwezi wa tatu nipo katika biashara yangu mpya ya nafaka nauza mchele na maharage nimepitia changamoto nyingi sana haswa matapelii, dalali kukutumia mzigo mbaya ambao unachukua kwa bei ya juu halafu ukifika sokoni lazima ukakate hela unauza bei ya chini kurudisha hela mda mwingine unaokoa tu hela. Changamoto ni nyingi kwakwelii ila sijakata tamaa napambana.
Sasa kuna hili swala.. ninapouza kuna jirani yangu naye anauza biashara kama yangu nimemkuta na inaonesha ana muda mrefu sana katika biashara, ana wateja wa kutosha na ana mtajii wa kutosha kiufupi kanizidii pakubwa sana.
Changamoto ipo kwenye wateja hivi wenzangu huwa mnahisi vipi mwenzako mmefungua duka sawa mna biashara zinazofanana ila chakushangaza mwenzako anauza gunia kumi asubuhi wewe ndo kwanza hata kilo moja hujauza 😁😁 mikokoteni inapaki kila muda plus mapikipiki muda wote hayakaukii yananunua mizigo pale wewe bado ngoma ngumuu.
Hivi wafanyabiashara wenzangu mliwezaje kudeal na mpinzani wako ambaye kakuzidiii kila kitu na ukizingatia wewe ndio kwanza unaanza ila miezi ndio hivyo mwezi watatu? Msaada wenu tafadhali
Nyongeza: Biashara ya mchele ni pasua kichwa sana walioweza sijui wanafanya vipi aiseee toka nimeanzaa faida siioni.
Nawatamani sana wateja wa jumla ila wanataka mchele mzuri halafu kwa bei mteremko bila kujua mimi nakochukua nachukua bei kubwa.
Swali lingine kwa wafanyabiashra wana mchele faida inabidi iwe sh ngapi kwa gunia kwa kawaida huenda mimi naweka faida kubwa halafu sijui.
Mimi ni mfanyabiashara wa nafaka hapa jijini Dar es Salaam. Sio mgeni katika kufanya biashara ila naweza sema ni mgeni katika kufanya biashara ya kwangu. Kwa sababu hapo awalii nilikuwa nafanya biashara za watu tuu.
Na sikujua kama biashara zina changamoto hivi hasa ukiwa wewe ndio mwenye biashara.
Mpaka sasa huu ni mwezi wa tatu nipo katika biashara yangu mpya ya nafaka nauza mchele na maharage nimepitia changamoto nyingi sana haswa matapelii, dalali kukutumia mzigo mbaya ambao unachukua kwa bei ya juu halafu ukifika sokoni lazima ukakate hela unauza bei ya chini kurudisha hela mda mwingine unaokoa tu hela. Changamoto ni nyingi kwakwelii ila sijakata tamaa napambana.
Sasa kuna hili swala.. ninapouza kuna jirani yangu naye anauza biashara kama yangu nimemkuta na inaonesha ana muda mrefu sana katika biashara, ana wateja wa kutosha na ana mtajii wa kutosha kiufupi kanizidii pakubwa sana.
Changamoto ipo kwenye wateja hivi wenzangu huwa mnahisi vipi mwenzako mmefungua duka sawa mna biashara zinazofanana ila chakushangaza mwenzako anauza gunia kumi asubuhi wewe ndo kwanza hata kilo moja hujauza 😁😁 mikokoteni inapaki kila muda plus mapikipiki muda wote hayakaukii yananunua mizigo pale wewe bado ngoma ngumuu.
Hivi wafanyabiashara wenzangu mliwezaje kudeal na mpinzani wako ambaye kakuzidiii kila kitu na ukizingatia wewe ndio kwanza unaanza ila miezi ndio hivyo mwezi watatu? Msaada wenu tafadhali
Nyongeza: Biashara ya mchele ni pasua kichwa sana walioweza sijui wanafanya vipi aiseee toka nimeanzaa faida siioni.
Nawatamani sana wateja wa jumla ila wanataka mchele mzuri halafu kwa bei mteremko bila kujua mimi nakochukua nachukua bei kubwa.
Swali lingine kwa wafanyabiashra wana mchele faida inabidi iwe sh ngapi kwa gunia kwa kawaida huenda mimi naweka faida kubwa halafu sijui.
Sawa ila hata mimi huu si mwezi wa tatu ila bado ngoma ngumuu, halafu soon tu natakiwa kulipa kodii afu hata faidaa haijaingia daah
Sawa boss, nimekusomaUna mawazo ya kibeki tatu, yawezekana hujawahi uza hata nyanya za gengeni.
Hakuna biashara ambayo washindani hawajifanyii evaluation na kujipima kulingana na market na industry. Na hiyo haiitwi wivu wala kijicho.
Big point brooo ila na kwenyew kununua moja kwa moja kwa mkulima ni mtihani kwa sabb kila mashine akienda tiyar kuna madalali wapo hapoKwanza napenda kukupongeza kwa hatua uliyofika ya kuwa na biashara yako kutoka kufanya biashara za watu. Lakini napenda pia kukupongeza kuwa ujue biashara haina ujanja, wala huyo jirani yako sio kuwa anafanya uchawi wala nini, usije kudanhanywa ukaenda kwenye ushirikina.
Yeye kuwa na wateja sio ajabu kwakuwa yuko siku nyingi na anajuana na wateja wengi. Unachotakiwa kufanya wewe ni kuanza kujifunza sehemu ya kupata biadhaa nzuri na kwa bei nafuu ambayo wewe ukija kuuza usitake faida kubwa sana, ni bora upate faida ndogo uuze sana kuliko kusubiri faida kubwa ukauza kidogo.
Angalia sana na epuka madalali, jaribu kununua kwa mkulima mwenyewe. Biashara ni changamoto kikubwa kila siku jifunze kupunguza hasara na uwe rafiki wa wateja wako, ifike sehemu akija kwako anatakani kununua kwako na awe tayari kukusubiri kama umefunga duka, hakuna ujanja hapo.
Shida mim wateja wang wa kitonga. Mbeya bei zenu zipo juu sana mimi michele yang ya 1000, 1100, 1200, je unayo michele ya hio beiMzee pole kwa changamoto unazopitia mim mwenyew nauza mchele jumla nipo Mbeya ukitaji mchele mzuri , wakati unaweza nicheck PM
Tafuta connection na wakulima, wenye mashine ili kuwaepuka madalali.Kitu kingine madalali ndo wanafanya biashara ionekane ngumu hasa wa morogoro ifakara wana tamaa kila mashine utawakuta wapo hapo mpka wanakela mchelee wanauza bei kubwa ukilinganisha na anayouza mwenyewe mkulima
Umenena vema mkuuLakwanza kabsa anza kwa kuchunguza jiran yako wateja wake anaishi nao vp, je bei zake vp je quality ya mzgo wake vp
Lapili jipe mda kua mvumilivu
La tatu acha kuangalia wengne jipange na biashara yako kla mtu na njia zake zakufanya biashara
Jamaa anaonekana hana uvumilivu wa biashara,pili hakujipanga kufanya utafiti wa kutosha kuanzia bei za kununua shambani na bei za kuuzia sokoni.Umesema jirani yako ana muda mwingi katika biashara hiyo halafu unapànic kuona ana wateja wengi.
Uko sahihi.Nishafanya biashara za aina hio mkuu mwaka 2011 moja ya sababu kubwa ya kuuza sana sio kwamba anawateja wengi , mara nyingi unakuwa na wateja wako ambao wananunua kwako kila siku yaani hawa hata usipate mteja wao watakuja kununua tu... kwa mfano wakati huu wateja wetu wakubwa walikuwa nje ya eneo duka lilipo na biashara zao zilikuwa migahawa maana yake mchele wanahitaji mwingi.
Hivyo kabla ya kusubiria mteja kuja kununua kwako wafuate na ongea nao uwashawishi , tengeneza namna ambayo wataona ni faida kuchukua mchele kwako kuliko kwa wengine , huu tunaita urafiki wa kibiashara.
Mimi nilikuwa nakaa dukani enzi hizo , ila Bi mkubwa yeye anatembekea waumini wenzake kanisani na watu anao wajua ambao wanabiashara anawapa pitch nzuri ndio wanakuja kununua mzigo mkubwa(Hapa kuna namna nzuri ya kuwavutia mfano unawapa mchele na wanalipa baada ya mauzo n.k)
Biashara za Nafaka hasa hizi za jumla hazitaki ukae dukani na usubirie mteja akutafute , mteja mkubwa unamtafuta wewe , kaa dukani subiria wateja wa reja reja tu akija mkubwa ni bahati yako .
Mambo mengine ni ya kiimani plus mazindiko sitaki kuyazungumzia
Bi mkubwa alikuwa anamwaga sana maji yaliombewa na kunipaka mafuta kabla sijaenda kufungua duka[emoji23][emoji23]
POINT YA MUHIMU SANA.Kitu Cha kwanza kwenye biashara Ni position yaani biashara ilipo. Cha pili Ni position.
Cha tatu nidhamu na kuweka sura ya tabasamu hasa kwa wateja wa kike.
Cha nne. Unakonunulia mzigo.
Ushauri huu nami nimeuchukuaMambo matatu ktk biashara ni muhimu nanlazima kuyajua na kufanya kwa usahihi
1. Namna ya kununua mzigo
Ubora sokoni,bei rafiki,chaneli ya kupata mzigo kwa usahihi,wadau wa kudili nao nk
2. Namna ya kuuza
Bei yako sokoni,customer care,sera za ofisi na usimamizi wake nk
3. Namna ya kudhibiti pesa
Kila senti ya biashara lazima itumike kwa hesabu sahihi za kihasibu. Sera na usimamizi wa pesa ya biashara ni kitu muhimu sana sbb ndio uhai na ukuaji wa biashara ulipo
Kwa hiyo mkuu hayo mambo tajwa hapo juu huenda ndipo mafanikio ya jirani yako yalipo na ndipo anguko lako lilipo. Kutoka hapo ni ucheki maendeo hayo uboreshe
Nina simu mbovuu haichukui kamera vizurii ndo maana nashindwa kujitangaza kweny mtandaoJamaa anaonekana hana uvumilivu wa biashara,pili hakujipanga kufanya utafiti wa kutosha kuanzia bei za kununua shambani na bei za kuuzia sokoni.
Kitu kingine alikuwa anawaza akianza tu apate wateja wa ghafla na kupiga faida kitu ambacho hakipo kwenye biashara.
Kitu kingine anawatam
Uko sahihi.
Watu siku hizi wanauza kisomi.
Zama za kukaa dukani unangojea wateja wa kubahatisha zimepitwa na wakati.
Kwa mfano kuna jamaa yetu mmoja ni school mate wetu anauza biashara kama hiyo ya nafaka kwa jumla na rejareja yeye huwa anatutangazia kwenye magroup yetu ya whatsapp ina maana kila mwezi ana uhakika wa kupata wateja 10 kutoka kwenye group letu la whatsapp baada ya hapo akienda kuwatangazia wenye migahawa akiwapata watano basi biashara inaenda hata kama hajapata wateja wapya.
Cha msingi mtoa mada ajipange kutafuta wateja wake kwa kutumia hizi mbinu asiangalie au kuwatamani wateja wa mpinzani wake pengine aliwaandaa kwa muda wa miaka 10 hatoweza kuwahamisha kirahisi anavyodhani.
Sio lazima kwa simu.Nina simu mbovuu haichukui kamera vizurii ndo maana nashindwa kujitangaza kweny mtandao