singanojr
JF-Expert Member
- Sep 24, 2020
- 1,974
- 10,361
Nishafanya biashara za aina hio mkuu mwaka 2011 moja ya sababu kubwa ya kuuza sana sio kwamba anawateja wengi , mara nyingi unakuwa na wateja wako ambao wananunua kwako kila siku yaani hawa hata usipate mteja wao watakuja kununua tu... kwa mfano wakati huu wateja wetu wakubwa walikuwa nje ya eneo duka lilipo na biashara zao zilikuwa migahawa maana yake mchele wanahitaji mwingi.
Hivyo kabla ya kusubiria mteja kuja kununua kwako wafuate na ongea nao uwashawishi , tengeneza namna ambayo wataona ni faida kuchukua mchele kwako kuliko kwa wengine , huu tunaita urafiki wa kibiashara.
Mimi nilikuwa nakaa dukani enzi hizo , ila Bi mkubwa yeye anatembekea waumini wenzake kanisani na watu anao wajua ambao wanabiashara anawapa pitch nzuri ndio wanakuja kununua mzigo mkubwa(Hapa kuna namna nzuri ya kuwavutia mfano unawapa mchele na wanalipa baada ya mauzo n.k)
Biashara za Nafaka hasa hizi za jumla hazitaki ukae dukani na usubirie mteja akutafute , mteja mkubwa unamtafuta wewe , kaa dukani subiria wateja wa reja reja tu akija mkubwa ni bahati yako .
Mambo mengine ni ya kiimani plus mazindiko sitaki kuyazungumzia
Bi mkubwa alikuwa anamwaga sana maji yaliombewa na kunipaka mafuta kabla sijaenda kufungua duka[emoji23][emoji23]