Mosi, penzi halina mitishamba.
Pili, mimi kama mimi hakuna mwanamke atakayenifanya nimpende pasipo mimi mwenyewe kumtamani na kutaka kulala naye. Hivyo kama ningekuwa na mke halafu nitoke nje ya ndoa basi huyo mke wangu ana haki ya kuzielekeza lawama zote, shutuma zote, na adhabu yoyote au zozote zile atakazoona zinafaa kwangu mimi. Kuelekeza nguvu na hasira kwa mtu niliyecheat naye ni sawa na kupaka rangi upepo! Tatizo siyo yule nilicheat naye. Tatizo ni mimi niliyecheat.
Tatu, huyo mama kwenye hiki kisanga ni aongee tu na mumewe ajue kinachoendelea. Kwani hata akimfukuza huyo msichana wa kazi hiyo haimaanishi huyo mumewe hawezi kutoka nje ya ndoa. Kudili na msichana wa kazi, narudia tena, ni sawa na kupaka rangi upepo!!!!