Hivi wali una nini cha mno?

Zamani tulikua tunaanzisha safari kutembelea ndugu wanaishi mbali, ili upikiwe wali, maana mgeni ili ajisikie amekilimiwa na mwenyeji wake, wampikie wali kuku, na sinia la wali lifunikwe na kawa.
 
Hawa ndio wale ambao wakila wali wanasema hawashibi!!!!
 
Zamani tulikua tunaanzisha safari kutembelea ndugu wanaishi mbali, ili upikiwe wali, maana mgeni ili ajisikie amekilimiwa na mwenyeji wake, wampikie wali kuku, na sinia la wali lifunikwe na kawa.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Aiseee hata mimi Sijui huu ubwabwa wanaupendea nini
 
Kinapendwa sababu kile kingine kinamapungufu, wali una mafuta, chumvi nk. Wakati ugali unachemshwa tuuu bila kitu vitalinganaje? Wenzio wanaumiza vichwa kwa mambo ya maana we unawaza tofaut ya wali na ugali,,,,!!!??
Mwache awaze hivyo, ndio kiwango chake cha ufaham kilipo ishia. Lakini kumbuka kati ya watu 4 mmoja wao ni...
 
Tena siku mkila Pilau hutaki hata kunawa mkono na ukitoka nje unaenda kuwanusisha rafiki zako "Nuseni mikono yangu leo mama kapika Pilau tumekula" utoto wa enzi hizo ilikua raha sana.
 
Kiporo cha Wali enzi hizo tulikua tunanywea chai asubuhi..Daah!! Where are those old gold days!
 
Enzi za zamani wali lazima "Ubanikwe" unafunikwa na mfuniko wa bati juu ya Sufuria na kuwekewa makaa ya moto juu ya Sahani ili kupata "Ukoko" ambo huliwa na mtu "mzito" kwenye familia na hasa Baba.


Tafadhali yakhee hiyo kitu ipatie heshima yake inayostahili, haitwi ukoko, hiyo kitu inaitwa "Matandu", Ukoko ni yale mabaki ya chini kabisa ya sufuria ambayo unaweza kukwangua na kijiko.

Raha ya Matandu uletewe kwenye kisosi huku umekalishwa kwenye kigoda walishwa weyee kama kinda la ndege vile!
 
Dah! Upo sahihi kabisa Mkuu, unajua imekua ni miaka mingi sana aisee..
 
Wallah umenikumbusha shemeji yangu NIMPENDENANI. Yaani yule Mwali apika haijapata kutokea.
 
Siku hizi wali watumbukizwa kwenye rice cooker tu, ladha hakuna kama ule wa 'kubanika'

Mbona lugha zenu zinaleta ukakasi atii !, huo wali haubanikwi, bali unakuwa unapaliwa na makaa ya moto , kwa maana ukishaiva kabla ya kukauka, unachukua chombo cha kufunika juu yake unaweka makaa ya moto, ndiyo kupalia kwenyewe hukooo!
 
Kinachopendwa na Waarabu, lazima kipendwe na kila mmoja!

Labda ni kizuri maana hawa wenzetu huwa wanajua vitamu hasa viko wapi!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu, nimewaza kuhusu mtandao pendwa na hawa ndugu zetu
 
Mbona lugha zenu zinaleta ukakasi atii !, huo wali haubanikwi, bali unakuwa unapaliwa na makaa ya moto , kwa maana ukishaiva kabla ya kukauka, unachukua chombo cha kufunika juu yake unaweka makaa ya moto, ndiyo kupalia kwenyewe hukooo!
Ndio hicho kitendo cha kuweka sahani juu na makaa ya moto kinaitwa KUBANIKA.
 
Hii kitu ina majina meengi kweli kweli wala hujakosea na mengi ya majina hayo ni kuonesha sifa zake na aina za mapishi kwa mfano

Mpunga

Wali

Punje ( Ilitumika zaidi sehemu za Skuli)

Mpunyenye ( Hiii kwa wazee wetu waleee wa zamani)

Pilau ( Raha yake uwe na kachumbari na ndizi mbivu) na haswaa kwenye shughuli

Biriani ( Mapishi ya kihindi)

Ubwabwa ( Huu uliwe na maharage ) haki ya nani weka mbali na watoto !

Boko ( Hapa aidha mapishi yameenda doroo au uji wa mgonjwa)

Mchele ( kwa ndugu zetu wa Uganda na akina Omera pale za kanda ya ziwa)

Ubeche ! heee heee heee !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…