Hivi wanafunzi wanaosoma shule za kata wana matatizo gani?

Mboka man

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2020
Posts
478
Reaction score
1,647
Matukio yanayonihuzunisha

1.Wanapiga makonda mpaka wanawapa vilema

2.Mwalimu akizingua wanamchapa kama mtoto mdogo

3.Yaani shule wanaingia saa 4

Kuhusu taaluma
1.Kufaulu 1 kati ya 120

2.Mwanafunzi mwaka mzima kasoma page 2

3.Muda wa masomo wanashinda vijiweni wakicheza kamari

4.Akienda ana daftari moja ambalo hilo hilo anaandikia masomo yote

5.Wengi wao hawapendi kuchomekea mashati waikenda shuleni

Japo sio wote ila wengi wao wako hivyo je, tatizo ni nini?
 
Panya Road wengi inasemekana ni absentees wa form 3 na 4
 
Matukio yanayonihuzunisha
1.wanapiga makonda mpaka wanawapa vilema
2.mwalimu akizingua wanamchapa kama mtoto mdogo
3.yani shule wanaingia saa 4
kuhusu taaluma
1.kufaulu 1 kati ya 120
2.mwanafunz mwaka mzima kasoma page 2
3.muda wa masomo wanashinda vijiweni wakicheza kamari

4.akienda ana daftari moja ambalo hilo hilo anaandikia masomo yote

5wengi wao hawapendi kuchomekea mashati wakenda shuleni

Japo sio wote ila wengi wao wako hivyo je tatizo ni nini
Asilimia kubwa ya hao wanafunzi wanaochaguliwa kwenda shule za kata ni wale ambao walikuwa hawapendi shule tangu wakiwa shule za msingi so kule huwa wanazolewa na kujazwa shule za kata kwa ajili ya kusogeza muda mbele tu.

Na asilimia kubwa shule za msingi walifeli ila wanawabeba tu,wewe fikiria mtu hajui hata kusoma halafu anaambiwa kafaulu huo mtihani aliufanya vipi ikiwa hata kusoma kiswahili hajui
 
Waache shule wakalime wengine wakaolewe tuweze kufikia uchumi wa bluu🔵
 
Asilimia kubwa ya hao wanafunzi wanaochaguliwa kwenda shule za kata ni wale ambao walikuwa hawapendi shule tangu wakiwa shule za msingi so kule huwa wanazolewa na kujazwa shule za kata kwa ajili ya kusogeza muda mbele tu.
Na asilimia kubwa shule za msingi walifeli ila wanawabeba tu,wewe fikiria mtu hajui hata kusoma halafu anaambiwa kafaulu huo mtihani aliufanya vipi ikiwa hata kusoma kiswahili hajui
Sure Mkuu vilaza wengi wapo huko kwenye shule za kata
 
Naanza;

1. Wananyanyaswa na makonda kwa kutopanda daladala na nyie wenyewe mkishuhudia bila kufanya lolote

2. Wanakosa elimu bora, miundombinu ya kiufundishaji pamoja mazingira mabovu ya shule

3. Manyanyaso kutoka kwa baadhi ya walimu, ikiwemo adhabu kali, maneno machafu, dharau na udhalilishaji

4.Baadhi yao wana hali ngumu kimaisha, ikiwemo kukosa vifaa vya kusomea na hela ya kula shuleni

6.Juu ya changamoto zote ila baadhi wanatoboa vizuri kushinda wale broilers, wako very smart
 
Alafu ndio wanakotoka Marais wa nchi,mawaziri wa kuu na wabunge.
 
Ni mihemko tu ya kipindi cha balehe na kukosa muongozo mzuri toka kwa wakubwa wao.
 
Na bado wamepunguziwa muda wa kusoma.

Toka miaka 7 mpaka 6.

Taratibu tu wataanza kuwapa vyeti bila kwenda shule.
 
Naanza;

1. Wananyanyaswa na makonda kwa kutopanda daladala na nyie wenyewe mkishuhudia bila kufanya lolote

2. Wanakosa elimu bora, miundombinu ya kiufundishaji pamoja mazingira mabovu ya shule

3. Manyanyaso kutoka kwa baadhi ya walimu, ikiwemo adhabu kali, maneno machafu, dharau na udhalilishaji

4.Baadhi yao wana hali ngumu kimaisha, ikiwemo kukosa vifaa vya kusomea na hela ya kula shuleni

6.Juu ya changamoto zote ila baadhi wanatoboa vizuri kushinda wale broilers, wako very smart
Salute Salute salute mkuu, umejibia hii hoja vema kama GT,again humu tuna working class ambao wanajifanya kabisa hawajui kinachoendelea in a real life, wao vitoto vyao vinasomeshwa huko kwenye English medium schools, vitoto vyao vinatibiwa kwenye vizahanati vya uchuchuroni wanajiona wameyatoa maisha, hakuna mtoto au mzazi anayependa shule za kayumba na huyo aliyezianzisha hata kitukuu chake hakisomi huko
 
Naanza;

1. Wananyanyaswa na makonda kwa kutopanda daladala na nyie wenyewe mkishuhudia bila kufanya lolote

2. Wanakosa elimu bora, miundombinu ya kiufundishaji pamoja mazingira mabovu ya shule

3. Manyanyaso kutoka kwa baadhi ya walimu, ikiwemo adhabu kali, maneno machafu, dharau na udhalilishaji

4.Baadhi yao wana hali ngumu kimaisha, ikiwemo kukosa vifaa vya kusomea na hela ya kula shuleni

6.Juu ya changamoto zote ila baadhi wanatoboa vizuri kushinda wale broilers, wako very smart
Nakazia [emoji419][emoji419][emoji419]
 
Uko sahihi mkuu.
Wale watoto wanakosa mwongozo na kujaliwa hivyo muda wote wanakua kwenye self-defence mode...wanajihami muda woote kama wamejizira hiv kwakua hakuna wa kuwapambania kama wasipojipambania...so wana act ku claim something they feel missi g to them.
 
Wanafata ushauri wenu kuwa elimu si chochote mbele ya pesa. Hivyo wanasaka pesa zaidi kuliko elimu
 
Hio kudunda makonda ni sawa tu.....kuna makonda wanafanyaga gari ni za baba yao......eti hii sio school bus......tena kichapo cha makonda kiendelee
 
Matukio yanayonihuzunisha
1.wanapiga makonda mpaka wanawapa vilema
2.mwalimu akizingua wanamchapa kama mtoto mdogo
3.yani shule wanaingia saa 4
kuhusu taaluma
1.kufaulu 1 kati ya 120
2.mwanafunz mwaka mzima kasoma page 2
3.muda wa masomo wanashinda vijiweni wakicheza kamari

4.akienda ana daftari moja ambalo hilo hilo anaandikia masomo yote

5wengi wao hawapendi kuchomekea mashati wakenda shuleni

Japo sio wote ila wengi wao wako hivyo je tatizo ni nini
Kwa taarifa yako hao wanafunzi hawana shida yoyote ile. Mwenye shifa hapo ni Serikali iliyokuja na sera ya kipuuzi, ya kuifanya elimu ya sekondari kuwa ya msingi.

Kilichotakiwa kufanywa kilikuwa ni kuwatengenezea mazingira mazuri hao watoto. Wenye uwezo mkubwa wangepelekwa shule za sekondari za bweni! Na wale wenye uwezo wa wastani wangepelekwa vyuo vya vyeta ili wakajifunze ufundi.

Kitendo cha kuwalazimisha watoto wasio na mzuka wa kukariri masomo wasiyo yaelewa; kusoma mpaka kidato cha nne, tena katika mazingira magumu na hatarishi! na mwisho wa siku kupata division 0! Ni wastage of time and resources.
 
Kwa taarifa yako hao wanafunzi hawana shida yoyote ile. Mwenye shifa hapo ni Serikali iliyokuja na sera ya kipuuzi, ya kuifanya elimu ya sekondari kuwa ya msingi.

Kilichotakiwa kufanywa kilikuwa ni kuwatengenezea mazingira mazuri hao watoto. Wenye uwezo mkubwa wangepelekwa shule za sekondari za bweni! Na wale wenye uwezo wa wastani wangepelekwa vyuo vya vyeta ili wakajifunze ufundi.

Kitendo cha kuwalazimisha watoto wasio na mzuka wa kusoma; kusoma mpaka kidato cha nne, tena katika mazingira magumu na hatarishi! na mwisho wa siku kupata division 0! Ni wastage of time and resources.
Ubaya wa watanzania wengi akili zimezama kuona mtu mwenye akili nyingi ni yule mwenye ma vyeti mengi

Na kushindwa kutambua uhalisia wa maisha wenyewe unahitaji watu wa namna gani na kwa wakati gani

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom