Hivi wanangu hawa sasa wanachanganyikiwa au wanapevuka kiakili?

Hivi wanangu hawa sasa wanachanganyikiwa au wanapevuka kiakili?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kwa takriban wiki sasa nimekuwa siwaelewi kabisa watoto wangu Wapendwa wawili wa kiume Samora na wa kike Charlotte kwa maneno yao au kauli zao kwangu ambazo zinafanana.

Wote nawasomesha hapo IST ( International School Of Tanganyika ) iliyopo Upanga na sijui niseme ni bahati mbaya au nzuri kwamba walianza kusoma hapo toka wakiwa kindagarten ( Vidudu / Chekechea ) hadi sasa wapo Standard Four ( 3 )

Lakini hawa watoto ndani ya muda huu mfupi wa wiki moja wamekuwa wakiniambia tena huku wakilia kuwa wanataka niwahamishe shule na niwapeleke Kambagwa Secondary School, shule zetu hizi za Changanyikeni lakini sijaafiki bado kwani naona kama vile wanangu watapotea kielimu.

Naomba ushauri wenu wakuu, Je nikubaliane nao na niwahamishe au wabaki tu hapo hapo IST? Na je ni kwamba wanangu hawa kwa maamuzi yao haya wamechanganyikiwa kiakili au ndiyo kusema wamekomaa na wamekuwa sasa?

Karibuni.
 
Pengine kuna yanayotendeka na yenye kuudhi juu ya ''watoto'' wako hao.Fuatilia🙁🙁🙁🙁🙁
 
Watoto mara nyingi huitaji kusikilizwa ila si kila watakacho hupewa ama hupata...Kwa mfano watoto wengi huwa hawependi kula kabisa na inafikia mahali hadi wanalia kuwa hawataki kula...Sasa wewe kama mzazi utamwachia asile..
 
Kwa Takriban Wiki Sasa Nimekuwa SIWAELEWI Kabisa Watoto Wangu Wapendwa Wawili Wa Kiume SAMORA Na Wa Kike CHARLOTTE Kwa Maneno Yao au Kauli Zao Kwangu Ambazo Zinafanana.

Wote Nawasomesha Hapo IST ( International School Of Tanganyika ) Iliyopo Upanga Na Sijui Niseme Ni Bahati Mbaya au Nzuri Kwamba Walianza Kusoma Hapo Toka Wakiwa Kindagarten ( Vidudu / Chekechea ) Hadi Sasa Wapo Standard Four ( 3 ) Lakini HAWA WATOTO Ndani Ya Muda Huu Mfupi Wa Wiki Moja WAMEKUWA WAKINIAMBIA Tena Huku WAKILIA Kuwa Wanataka Niwahamishe SHULE Na Niwapeleke KAMBANGWA PRIMARY SCHOOL Shule Zetu Hizi Za CHANGANYIKENI Lakini Sijaafiki Bado Kwani Naona Kama Vile Wanangu Watapotea KIELIMU.

Naomba USHAURI Wenu Wakuu Je Nikubaliane Nao Na Niwahamishe au Wabaki Tu Hapo Hapo IST? Na Je Ni Kwamba Wanangu Hawa Kwa MAAMUZI Yao Haya Wamechanganyikiwa KIAKILI au Ndiyo Kusema Wamekomaa Na WAMEKUWA Sasa?

Karibuni.
Wanasema hamna kipindi kigumu kama kipindi cha kubarehe na hapo watakuwa wanatamni kuwa huru na maisha yao wanaona maisha ya kufungiwa kila siku yamewachosha.
Hao jaribu kwenda nao mdogo mdogo hicho ni kipindi kinapita hata wewe ulikipitia.
 
Chunguza kwanza nnini sababu ya wao kukueleza hivo inawezekana kuna ka story ka kuwapumbaza kanaendelea shuleni hivyo wa kwa kuwa upeo wao ni mdogo
wameamua kutafuta suluhisho.
 
Wewe Mkimbizii tokea umetoroka kambinii umeamua kuishi kwakutumia bandle la sifa za kijinga kila jukwaa utakalo pita humu jf..
 
Danganya kiutu uzima basi, inakuwaje wanao wasome std four watake kusoma kambagwa sek ?
 
Kaanao chini ujue kwanini wanataka kwenda huko,umefatilia mwenendo wa watoto hivi karibuni? marafiki zao ?na hapo shule maendeleo yao yakoje ? umeonana na walimu wao wakueleze mawili matatu baada ya hapo kaanao chini uamue na kama hutaki waende uko Tia mchuzi pangu pakavu waeleze sababau...
 
Wewe Mkimbizii tokea umetoroka kambinii umeamua kuishi kwakutumia bandle la sifa za kijinga kila jukwaa utakalo pita humu jf..

Tena Napenda Kweli SIFA Mkuu Na Hasa Nikiwa Faragha Na Mamako.
 
jamani mbona Kambangwa ni Sec? tena ya serikali? mtoto wa IST (primary) tena private, anawezaje kuhamia Govt sch?
 
Bora hata ungeandika sababu yao ya kwanini wanataka iwe hivyo, inaelekea labda haujawauliza bali unataka wafate yako tu. Sikilizeni watoto wenu uweze kuongea nao vizuri, na pia kuelewana hata kama ni wadogo kivipi.
 
Kaka upo vizuri.

Ada ya kusoma IST kwa mwaka nafikiri ni zaidi ya $7,000 kama sijakosea kwa mtoto mmoja.

Kama ni kweli upo vizuri. Ila mtoto anayesomea IST iwe primary au high level siku akija kukukwambia yeye ni shoga inabidi ukubali tu. Maisha yao ni ya kizungu hatari na wanajua rights zao.

Sekondari yao ndiyo balaa. kila mwanafunzi ana boyfriend na girlfriend. Na wazazi wanajua.
 
Back
Top Bottom