Englishlady
JF-Expert Member
- Apr 11, 2013
- 2,736
- 3,644
Wana mmu habri zenu.Naombeni msaada. Nipo kwenye maswali mengi kama hii inawezekana au mazingaombwe au naibiwa?Nipo kwenye mahusiano na mkaka toka mwezi wa tatu mwaka jana, kwa kipindi chote kaka huyu hajawahinigusa kwa mapenzi zaidi ya kushikana na kubusiana tu au wakati mwingine kumaliza ashiki kwa romance. Kila nikijitahidi kuweka mazingira ya kudo anachomoa, atatoa maelezo mengiii. Sio mtu wa dini maana hata kwenda kanisani ni maramojamoja, ni mnywaji na ni mkaka wa mjini. Sielewi hivi wapo wanaume wa jinsi hiyo miaka hii? Au naibiwa mie, yupo anayemmalizia ashiki zake.Nyongeza sikujui kazini kwake wala kwao kwa ndugu zake najua tu ni mtaa fulani hajawahi nipeleka na hutoa sababu nyingi nikitaka kwenda kwao. Kwake nimewahi enda mara mbili tu kwa miezi yote hii. Kila nikifanya jitihada za kuachana nae anasumbua, anatumia marafiki zangu ama ndugu zake kudai ananipenda, kila nikipima upendo wake siuoni. Naona kama napoteza muda tu, naomba ushauri wenu.