Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

kwenye pesa kivipi,hebu toa mfanoo
Kamaanisha kwenye pesa ndo wanaume mnakubaligi muwe sawa na wanawake yaani wote wanaume na wanawake tufafute pesa ila kwenye mambo mengine hamtakagi tuwe sawa
 
Tangu lini Msaidizi akadai haki sawa ili alingane na Me[emoji848]
Kama mwanamke anafanya majukumu ya mwanaume halafu mwanaume hafanyi majukumu ya mwanamke lazima mwanamke adai haki sawa na mwanaume tu hakuna namna
 
Tufafanulie mpenzi, maana mwanamke anaetoa elfu moja yake akanunua fungu la kitunguu huyo pia anachangia huduma.....
Kuna ndoa mwanaume na mwanamke wanatoa pesa za mahitaji na huduma nusu kwa nusu yaani pasu kwa pasu na kuna ndoa ambazo mwanamke ndo anatoa pesa za mahitaji na huduma zaidi kuliko mwanaume hao nao unawaongeleaje?
 
Majukumu ya kupika, kufua, kuosha vyombo, kusafisha nyumba, kutunza nyumba na kulea watoto.
Mwanaume kutembea na dada wa kazi ni utashi wake yeye mwenyewe tu kama atakavyoamua kuchepuka na mwanamke mwingine yeyote yule..

Nataka nijue hayo majukumu unayoyazungumzia ni yapi haswa.. itapendeza ukiyataja..
 
Kuna ndoa mwanaume na mwanamke wanatoa pesa za mahitaji na huduma nusu kwa nusu yaani pasu kwa pasu na kuna ndoa ambazo mwanamke ndo anatoa pesa za mahitaji na huduma zaidi kuliko mwanaume hao nao unawaongeleaje?
Hiyo pasu kwa pasu inategemea unaweza mwambia mkeo akusaidie nusu ya gharama wakati wa uhitaji ila akishapata anakutumia anakurejeshea

Lakini pia kwenye hilo la mwanamke kusimamia gharama kwa 100%inategemea mwanaume anachangamoto gani. Anaweza kuwa hana pesa sababu ya kukosa ajira na mambo kutokwenda sawa.....
 
Yaani mkuu ndoa unafananisha na organization? Kweli wanaume hamjui maana halisi ya ndoa.
 
Hao mahousegirl mnaoishia kutembea nao kwa kisingizio cha kuwa wake zenu wamewaachia majukumu yote mahousegirl?
Ndo maana kuna ma house girl halafu huwa nawashangaa wengi wenu tunawawekea wasaidiz wandani kabisa mnalalamika eti majukumuu
 
Tatizo mnatakaga wanawake tukubaliane na kila kitu wanaume mnachosema hata kama ni upuuzi mlishazoea wale wanawake wa kila kitu "ndiyo mume wangu"

Sasa siku hizi mmeona wanawake wa hivyo wamebaki wachache wengi tunahoji baadhi ya maamuzi yenu ya kipumbavu mnatuona wajeuri sijui hatufai kuolewa na mnajiona mko sawa kabisa upstairs
Unajua kabisa hauko sahihi lakini bado unaendelea kuwa mbishi bado unaendelea kuleta mashindano utadhani hamjui wajibu wenu
 
Tatizo mnaexaggerate utadhani hizo ndoa hata 50 zinafika.... Tukitoa vijijini ambapo wanaume kwa asilimia kubwa ni walevi na hivyo ni unfit kudeal na familia.
Unaona sasa hebu niambie hao wanawake wenzetu wa huko vijijini wana hali gani? Mimi sishangai kuwepo wanaume wa aina hiyo ila kinachonishangaza ni kwamba na wao nao wanataka waheshimiwe na wake zao kama wanaume wengine wanaotimiza majukumu yao yaani hilo ndo la ajabu
 
mpaka hapo we unaona Kuna 50/50?
Ndiyo kwa sababu ninyi mnatuhudumia sisi tunawalea tukianza kuleana basi hakika tutaanza kuhudumiana pia na bado tutakuwa kwenye ile ile 50/50
 
Sasa si ndo amsaidie mkewe kazi za nyumbani jamani? Au yeye anakuwa anafanya nini?
 
Ndio hamfai kabisa kuolewa ni hatari kwa afya mnachotaka kukileta ni ushindani mnataka mapinduzi mwanaume akiongea na nyie muongee

Lengo mtukalie kichwani muwe na sauti nyinyi hivi vitu huwez badilisha na kamwe hatuwezi fanana kimajukumu na kimaamuzi

Majukumu yetu yatabaki kuwa yetu hata mkiyaingilia sawa ila kamwe hatuwezi Fanya majukumu yenu na nafasi yetu itabaki palepale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…