Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Kwani nani kakataa? Mbona sisi hatuna shida kabisa ila je ni wanaume wote wamaostahili heshime? Najua kwa sababu ya akili zako finyu utasema ndiyo ila kaa ukijua kuwa wanaume wanaostahili heshima ni wale ambao wanajielewa na wana sifa zifuatazo waamimifu, wasikivu, wanaojali na wanatunza

Tofauti na hapo mwanaume hastahili kuheshimiwa tena anatakiwa kutukanwa kabisa sasa kama mnadhani mkiendelea kuwa hivyo mlivyo ndo mtarudisha heshima yenu basi endeleeni kusubiri hiyo meli uwanja wa ndege kumbuka siyo kila mwanaume anafaa kuwa mume na siyo kila mwanamke anafaa kuwa mke

Na wanawake ndo wanazidi kukengeuka kila siku hakuna mwanamke atakubali kuongozwa na jianaume lisilojitambua lina sifa za hovyo lisaliti, libabe, halijali na wala halitunzi hapa mnasema tu kuwa wanawake wenye mitazamo kama ya kwangu hawaolewi

Ila mbona ndo tunazidi kushuhudia kila weekend ndoa zinafungwa baadhi ya wanaume wenzenu wanawaoa wanawake wa aina hiyo hiyo mnayoiponda na ndoa zinadumu kabisa siku wanaume mtakapojua kutofautisha kati ya kututawala na kutuonea basi ndo mtajua mnakwama wapi
 
nyumbani kwenu mnaishije?? baba ako huwa anaosha vyombo au kupiga deki???
Ndiyo alikuwa anafanya mara moja moja kama msaada tu sana sana kama mama anaumwa lakini pia baba ndo alikuwa anahudumia familia nzima yaani anamhudumia mama pamoja na sisi watoto ila mama alikuwa anahudumia familia mara moja moja kumsaidia baba anapokwama tu
 
nikisema baba ako ni bwege anaosha vyombo,nitakuwa nasema urongo???
 
nikisema baba ako ni bwege anaosha vyombo,nitakuwa nasema urongo???
Halafu mwanaume akifanya majukumu ya mwanamke ni bwege ila mwanamke akifanya majukumu ya mwanaume ni nani? Mbona umemshangaa baba kufanya majukumu ya mama lakini haujamshangaa mama kufanya majukumu ya baba?
 
Halafu mwanaume akifanya majukumu ya mwanamke ni bwege ila mwanamke akifanya majukumu ya mwanaume ni nani? Mbona umemshangaa baba kufanya majukumu ya mama lakini haujamshangaa mama kufanya majukumu ya baba?
baba ako kuosha vyombo, kukuna nazi,kupiga deki na kufagia uwanja wewe unaona sawa???
 
Ndio wanawake wa leo hii mnapenda sana usawa wa kijinsia japo hamuwezi kuishi maisha ya usawa wa kijinsia hata kidogo.

Kwanza wengi wenu hamuujui hata huo usawa wa kijinsia uko vipi, nini kinaleta huo usawa wa kijinsia na athari au faida zake ni zipi. Wengi wenu mmejawa na double standard aidha kwa kujua au kutokujua kwenye hilo hitaji lenu la usawa wa kijinsia.

Unakuta mwanamke anatafuta mwanaume na kigezo chake cha kwanza ni kwamba mwanaume lazima awe na mshaara/kipato kikubwa kuliko yeye. Hapo hapo mwanamke huyo anajinasibu na yeye anataka usawa na wakati ukiangalia kusudio la yeye kuhitaji mwanaume mwenye nguvu kubwa ya kiuchumi kuliko yeye ni kuona mwanaume huyo anabeba sehemu kubwa ya majukumu hasa yanayohusiana na fedha Wakati huo yeye akichangia kidogo tu ndani ya mahusiano. Mpaka hapa tayari anakuwa ameshajitoa kwenye usawa bila kujua.

Kuna wanawake hasa wakikristu hususani waliosoma wameamua kushi maisha ya kuzitumikia career zao na kuweka kando majukumu ya kike ndani ya ndoa zao. Ila sasa cha ajabu likitokea tatizo lolote zito hao hao wanawake utaskia wakisema "mimi kazi yangu ni kuzaa kwa uchungu tu mengine hayanihusu". halafu hao hao wanawake hawataki uwaingilie kwenye maamuzi yao.

Wanawake wa leo hii wanataka kuoneka wako sawa na mwanaume kwenye kila kitu ilihali bado wanaona fahari kutolewa mahari kubwa wanapoolewa.

Wanawake wa leo hii wanataka usawa mpaka kwenye usaliti. Mume akichepuka na yeye anaona njia pekee ya kutatua tatizo ni kuchepuka pasipo kujali kuwa maumbile yake yamekaa kuingiza tofauti na ya mwanaume yaliokaa kutoa, hivyo hata athari kubwa iko upande wake.

Wanawake wa Leo hii wanataka kuwa na sauti/maamuzi sawa na mwanaume ilihali hata wakiskia kishindo cha mtu usiku nje ya nyumba hawana ujasiri hata wa kufungua dirisha kuchungulia kuna nini nje.


Wanawake wanataka kuwa na maslahi sawa na wanaume wakati huo impact yao kwenye mambo mbali mbali ya kijamii ni ndogo sana kulinganisha na ya wanaume na hii ni duniani kote...

Kuna siku nilikuwa namsikliza mwanajeshi mmoja wa kike wa Marekani analalamika eti kuwa wanajeshi wa kiume wanalipwa bonus kubwa kulinganisha na wao... anasahau kwamba hao wanajeshi wa kiume hawana mambo ya martenity leave na pia ndio wanaokuwa posted kwenye terror zones Mara kwa Mara.

Mwaka Jana nilimskia captain wa timu ya taifa ya wanawake ya USA Alex Morgan akikiomba chama cha soka cha marekani kiwaoboreshee maslahi yao kisa tu eti wao wamekuwa wakifanya vizuri kuliko timu ya wanaume kwa miaka ya karibuni.

Hivi Karibuni nilimskia katibu mkuu wa Fifa Fatma Samoura akilalamika eti zawadi na posho wanazopata washindi wa kombe la dunia la wanawake ni ndogo kulinganisha na zile wanazopata washindi wa kombe la dunia la wanaume... anasahau kwamba idadi ya viewers na wadhamini wanaojitokeza kwenye kombe la wanaume inaizidi kwa mbali sana ile inayojitokeza kwenye kombe la wanawake na ndio inayoleta tofauti ya kimaslahi.

Wanawake makazini wanapenda kupata promotion sababu tu wamefanya kazi mahali hapo muda mrefu na sio kwa sbabu ya jambo kubwa waliolifanya, na wakati huo wao ndio huwa hawishiwi kuwa na dharura za Mara kwa Mara.

kihalisia wanawake wanataka EQUITY na sio EQUALITY.

USAWA WA KWELI KATI YA MWANAUME NA MWANAMKE UTAKUJA KUTOKEA SIKU MWANAMKE AKIWEZA KUKOJOA KWENYE CHUPA HUKU AKIWA AMESIMAMA.
 
Kitu pekee nnachojua Most Women demand equal rights and not equal Responsibilties
And that's where their hypocrisy lies how can you demand equal rights and escape equal responsibilities?
 
Daah... wanaume tunapitia changamoto nyingi sana mkuu.

Ndio maana mimi sasa hivi nakaribia kuanza kuwachukulia wanaume kama wanawake na wanawake kama wanaume.

I am about to start treating women like men and vice versa.
 

Unajua we dada hujielewi, sasa kama hayo majukumu yanaonekana ni ya kike kwenye jamii, kwann wanaume wayafanye..half inaonekana una hasira sana na wanaume Edelyn
 
baba ako kuosha vyombo, kukuna nazi,kupiga deki na kufagia uwanja wewe unaona sawa???
Je kama mama anaumwa na baba akaamua kumsaidia? Ndo maana nikakuuliza kwahiyo mama kumsaidia baba majukumu yake ndo siyo kitu cha ajabu? Mbona haujajibu swali?

Hii ndo shida ya kuwadharau wanawake hatimaye mnadharau hadi majukumu yao bado sijaona sababu ya mwanaume kukataa kufanya hizo kazi kwani akizifanya anaumwa au anakufa? Nipe madhara makubwa anayopata mwanaume akifanya hizo kazi kama hakuna basi kaeni kimya

Kuna wanaume wengi tu huko wamekimbia majukumu yao na hawahudumii tena familia ila hao ndo mnawaona wajanja na wanaohudumia familia zao lakini wanawasaidia wake zao kazi mnawaona wajinga?

Halafu unavyobisha hapo utadhani hakuna kabisa kwenye jamii ya leo wanaume wanaofanya hizo kazi looh mbona wamejazana na kila kukicha na wanazidi kuongezeka usipofanya wewe watafanya wanaume wenzio halafu nimekwambia nipe maana ya bwege haujanipa naona unazunguka tu
 
Umeongea mengi sana ila haujagusia hata kidogo swala la mwanaume kumsaidia mkewe kufanya kazi za nyumbani yaani umeongelea tu mwanamke kumsaidia mumewe kutafuta pesa na umekwepa kitu ambacho ni hoja ya msingi sana

Na pengine ndo sababu kubwa ya wanawake wengi kuwa hivi walivyo leo hamuwezi kukubali ila huo ndiyo ukweli na kwa vile hakuna ambaye hayuko tayari kuukubali ukweli na kubadilika basi tuache tu utabiri utimie maana hakuna binadamu mwenye uwezo wa kuuzuia
 
And that's where their hypocrisy lies how can you demand equal rights and escape equal responsibilities?
We don't escape responsibilities but it has reached to a point where men want women to perform more responsibilities than them
 
Daah... wanaume tunapitia changamoto nyingi sana mkuu.

Ndio maana mimi sasa hivi nakaribia kuanza kuwachukulia wanaume kama wanawake na wanawake kama wanaume.

I am about to start treating women like men and vice versa.
Wewe ndo unataka kuanza? Mbona kuna wanaume wenzio walishaanza kitambo?
 
Unajua we dada hujielewi, sasa kama hayo majukumu yanaonekana ni ya kike kwenye jamii, kwann wanaume wayafanye..half inaonekana una hasira sana na wanaume Edelyn
Mbona wanawake tunafanya majukumu yanayoonekana ni ya kiume kwenye jamii?

Kuwa na hasira na wanaume? Kwa sababu ipi ya kuwaambia ukweli na kuwarekebisha makosa au kuna sababu nyingine?
 
hakika hata wewe hujanielewa..

swali lako linasema "hivi wanaume mnamaanisha nini mnaposema tunataka usawa"?

na mimi nimeelezea jinsi gani msivyo uelewa hata huo usawa wenyewe mnaoutaka na badala yake mnahitaji FAVOR au EQUITY...

BTW, kwa hiyo wewe unataka usaidiwe kuosha vyombo na kupika?

je, utaweza kukabiliana na majambazi saba yenye silaha usiku wa manane wakati huo mimi nimejificha chini ya meza?
 
We don't escape responsibilities but it has reached to a point where men want women to perform more responsibilities than them
please put more elaboration on this, more responsibilities in which sense actually?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…