Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

mnajidharau wenyewe kiasi kwamba mnanekana mna akili fupi,kwa mfano unamhonga mwanamke kwa 20k,kwa hiyo umemnunua kwa 20 k,sasa kwa nini usimdharau
Huyo mwanamke unayetembea naye unakuwa na mpango wa kumuoa na kutokumsaliti?
 
Tatizo hawa wenzetu Wanaongozwa na ubinafsi zaidi...mfano mwanaume akichepuka anaona ni halali yake kuchepuka ila mwanamke akichepuka ataambiwa ni malaya.... Mwanaume akizingua ndoa ikavunjika mke wake ataambiwa siyo mvumilivu,,, Mara sijui unatakiwa kumuombea mume wako..ila mwanamke akizingua ndoa ikavunjika ataambiwa ana tabia mbaya na mwanaume hataambiwa anatakiwa kumvumilia na kumuombea mwenzake


wanaume wanapenda wanawake wasiohoji kabisa hata pale wakiona mambo hayakai sawa....ukihoji unaambiwa unashindana na mwanaume, unataka usawa n.k. but mwanaume nani aliwaambia sisi siyo wanadamu? Sisi siyo wa kuhoji? Kwamba tukihoji ni kutaka usawa? Kwamba ninyi mna haki ya kukosea ila sisi hatuna? Kwamba ninyi ni bora kuliko sisi?

Siku mkiacha ubinafsi mtaacha na huu msemo wa kwamba wanawake tunapenda usawa



N.B Sisi kama binadamu tuko sawa humanly lakini mwanamke hawezi kuwa mwanaume na mwanaume hawezi kuwa mwanamke. Kila mtu atambue haki za mwenzake katika familia, ndoa na jamii kwa ujumla.
 
Sasa kama ni kukwepa manyanyaso ya kifedha, swala la kushupaza shingo limetokea wapi
Kwa sababu tayari wanawake wameingilia majukumu ya wanaume yaani kwa kifupi hiyo ni kama message kuwa wanawake wanatakiwa kuhudumiwa wakianza kujihudumia wenyewe au kuhudumia wanaume zao basi lazima wakae kwenye nafasi za wanaume zao tu hakuna namna hiyo ni nature
 
Hilo mbona linaeleweka mkuu? Sema sasa tatizo linakuja wanawake wasipofanya hizo kazi za kujitafutia kipato chao je wanaume mtawahudumia mahitaji yao yote kiuchumi bila kuwanyanyasa wala kusimanga?
 
hahaaaaaa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]!! wanawake mna akili gani kwa mfano???
Nipe definition yako ya akili halafu ndo nitakwambia tuna akili gani
 
This is a FEMINISM THEORY formulated in EUROPE and AMERICA when a WOMEN started demanding women's rights on the grounds of political, social, and economic equality to men.
Equality feminism and American liberalism seek equality for every individual.
But this concept are suitable to western countries and America because they know how to practice in its and not to our most of African countries including Tanzania.
 
Hivi siyo nyie wanaume mnaosema mnataka wanawake wenye akili ya maisha na wanaojua kutafuta pesa? Tena si ndo mnasemaga hamtaki wanawake wenye njaa wanaowaomba pesa? Sasa kama mwanamke hatafuti pesa anatoa wapi pesa za kujikimu? Hapo maana yake si kwamba mnataka wanawake wanaotafuta pesa?
 
This is a FEMINISM THEORY and was formulated in AMERICA and WESTERN EUROPEAN COUNTRIES. This advocacy of women's rights on the grounds of POLITICAL, SOCIAL, and ECONOMIC EQUALITY to MEN.
EQUALITY FEMINISM and AMERICAN LIBERILISM SEEK EQUALITY FOR EVERY INDIVIDUAL.
Dhana hii katika nchi zetu za Kiafrika imekuwa na changamoto hasa katika kutafsiri maana halisi ya maneno mawili HAKI na WAJIBU.
Wanawake walio wengi wa kiafrika wanapenda kuona wanatendewa na wanaume HAKI lakini wanashindwa kutambua ni haki zipi ambazo wanapaswa kutendewa?
Pia wananwake walio wengi wa kiafrika wanapenda kuona wanaume wanatimiza WAJIBU lakini wanashindwa kutambua ni wajibu upi ambao wanapaswa kutekelezewa?
 
Hata wanaume nadhani mnashindwa kuelewa ni usawa upi tunaoutaka mkuu usawa tunaoutaka siyo kimaumbile wala kimajukumu ila tunataka usawa kwenye mambo kama vile kupendana, kuheshimiana, kusameheana na kuvumiliana

Jamii nyingi za kiafrika zinataka mwanamke tu ndo ampende, amheshimu, amsamehe na amvumilie mwanaume ila mwanaume hatakiwi kufanya hayo eti kwa sababu tu ya mahari anayotoa kuoa kitu ambacho siyo sahihi

Yaani jamii zetu zinataka mwanaume akikosea aachwe tu na asifanywe chochote ila mwanamke akikosea apigwe, asalitiwe, apewe talaka au aongezewe mke sasa hiyo ni haki kweli?

Kwani ina maana kwenye ndoa ni mwanaume tu ndo anakosea mwanamke hakosei? Na kwanini mwanaume akikosea aachwe ila mwanamke akikosea aadhibiwe? Kwani wanaume makosa yenu ni madogo sana kuliko ya wanawake?
 
Aise nimekosa hata cha kuongezea ndugu yangu yaani umeenda mule mule hadi nimehisi kama nikiongezea hoja yangu naweza jikuta naharibu comment yako daah umemaliza kila kitu na natamani wanaume wote wangesoma hii comment yako wakaelewa ninachomaanisha
 
kupendana, kuheshimiana, kusameheana na kuvumiliana... nikiangalia hivi vyote mnavyovililia ni EMOTIONAL DERIVED (mtu kama hakupendi hakupendi na hawezi kukuheshimu na kukuvumilia, an nothing can change that)

Bahati nzuri karne hii 99% ya wanawake hawachaguliwi wanaume wa kuwaoa. Ni vyema kuwa na mwanamme anaye kupenda, kuheshimu, kukusamehe unapokosea, na anaye weza kukuvumilia.
Mnafanya wrong personal choices alafu baadae mnalalamika kwamba waume zenu wanawanyanyasa[emoji1][emoji1][emoji1]
Kuwa on the safe side hakikisha mnatumia mapenzi kama kigezo cha kupata wenza na sio ki2 kingine.
 
Briliant,jibu limenyooka halina utata...
 
Hivi huwa mnawachukuliaje wanawake wenzenu ambao japo wanajitafutia vihela vyao binafsi ila ifikapo kwenye majukumu ya kifamilia wapo very active and responsible. Kuanzia mume watoto na nyumba kwa ujumla. How do you feel kuona kuna wanawake wenzenu wa namna hio na wanaishi freshi na waume zao tu bila kujitutumua.
 
Sasa kama mwanaume hampendi na hamheshimu mwanamke husika kwanini anafikia hatua ya kumuoa? Kwani kuna wanaume wanalazimishwa kuoa?
 
Kwahiyo kwa mtazamo wako mkuu unaona ni haki zipi ambazo mwanamke anatakiwa kupewa na mwanaume wake na ni majukumu yepi ambayo mwanamke anatakiwa kutekelezewa na mwanaume wake?
 
Kwani mbona wapo wanaume ambao pamoja na kutimiza majukumu yao ya kutafuta pesa bado wanawasaidia wake zao kufanya kazi za ndani na wanaishi vizuri tu? Ninyi wanaume wengine ambao hamfanyi hivyo mnajisikiaje? Exceptions lazima ziwepo tu kwa sababu in every general rule there is always an exception ila tuongelee kile kilicho sahihi kabisa
 

Ndivyo wanavyotakiwa kuwa ila huu usawa unatuaribu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…