Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Mbona ninkitu cha kawaida haitakiwi kushangaa ...kwa kifupi Edelyn Hiyo dhana sisi tunawasaidia na kuwarithisha majukumu ili baadae sisi tukifa muendele kusaidia na kuendesha familia, maana pia hapo hapo shughuli zako nyingi anafanya housegairl ...
Sawa ila inakuwaje pale mnapotaka wanawake wawasaidie kutafuta pesa na kuhudumia familia?
 
Tatizo hawa wenzetu Wanaongozwa na ubinafsi zaidi...mfano mwanaume akichepuka anaona ni halali yake kuchepuka ila mwanamke akichepuka ataambiwa ni malaya.... Mwanaume akizingua ndoa ikavunjika mke wake ataambiwa siyo mvumilivu,,, Mara sijui unatakiwa kumuombea mume wako..ila mwanamke akizingua ndoa ikavunjika ataambiwa ana tabia mbaya na mwanaume hataambiwa anatakiwa kumvumilia na kumuombea mwenzake


wanaume wanapenda wanawake wasiohoji kabisa hata pale wakiona mambo hayakai sawa....ukihoji unaambiwa unashindana na mwanaume, unataka usawa n.k. but mwanaume nani aliwaambia sisi siyo wanadamu? Sisi siyo wa kuhoji? Kwamba tukihoji ni kutaka usawa? Kwamba ninyi mna haki ya kukosea ila sisi hatuna? Kwamba ninyi ni bora kuliko sisi?

Siku mkiacha ubinafsi mtaacha na huu msemo wa kwamba wanawake tunapenda usawa



N.B Sisi kama binadamu tuko sawa humanly lakini mwanamke hawezi kuwa mwanaume na mwanaume hawezi kuwa mwanamke. Kila mtu atambue haki za mwenzake katika familia, ndoa na jamii kwa ujumla.
mwanamke mpumbavu huvunja ndoa kwa mikono yake
 
Unakosea sana. Huwezi kusema uwezo aliopewa mwanamke ni mkubwa kuliko mwanaume kwa sababu ameumbwa' kike' hivyo huna sababu ya kumsikitikia kwa maana wakati anaumbwa amepewa na uwezo wa kuyastahimili hayo unayoyaona ni magumu. Kila mtu ana size yake
Vizuri sana hata wanaume walipoambiwa watakula kwa jasho lao walipewa uwezo wa kustahimili kutafuta pesa juu chini na kuhudumia familia sasa inashangaza wanawaume wa leo wanaposhindwa majukumu yao na kutaka wake zao wawasaidie
 
Nadhani ni kwa sababu alijua kabisa mwanamke ni kiumbe dhaifu sana yaani hata kujitawala tu mwenyewe hawezi, hivyo anahitaji kutawaliwa maisha yake yawe katika mstari mnyoofu.
Hahahaha unajibu kirahisi sana unajua ni kwanini shetani alimuita mwanamke ndo ale tunda halafu akamwambia ampe mwanaume? Kwanini asingemuita mwanamume ndo ale kwanza halafu ampe mwanamke? Najua utakuja na jibu lako hilo hilo kuwa wanawake ni dhaifu kuliko wanaume kitu ambacho siyo jibu la hayo maswali niliyokuuliza anyway ngoja nikuache uamini unachoamini
 
Kuna mada ilianzishwa humu kuwa je ni sawa mwanamke kumtongoza mwanaume? Niliona wanaume wengi walisema ndiyo eti kama tumewapenda tusiogope kuwatongoza ila wanawake wengi walisema hapana kutokana na tamaduni za Africa mwanaume ndo anayetongoza

Na hata mtaani pia naona wanaume wengi wanataka na wanawake tuanze kutongoza kama wao ila wanawake wengi wanaona aibu na hata wanaotongoza wenyewe wanatongoza kwa ishara na siyo moja kwa moja nikajiuliza sasa hawa si ndo wanasema hawataki usawa? Sasa na wanawake tukianza kutongoza kama wanaume hakutakuwa na usawa kweli hapo?
duuu!! sijawahi kusikia hiyo,case ipo katika 0.0001% ya wanaume then una generalize kwa wote
 
Swali la nyongeza: Je, mnataka wanawake tusifanye makosa ila wanaume mfanye makosa halafu wanawake tukae kimya tusiwaambie na wala tusiwafanye chochote au mnatakaje?
Kwahiyo hivyo ndivyo mnavyotaka?
 
Yaani unafananisha zoezi la kumwaga mbegu tu na zoezi la kubeba mimba, kuzaa watoto na kunyoyesha watoto? Wewe hebu nenda kabishane na wavulana wenzio huko mimi hapa nabishana na wanaume tu.
jibu swali hao watoto unazaa na wanawake wenzake au??
 
Mbona ninkitu cha kawaida haitakiwi kushangaa ...kwa kifupi Edelyn Hiyo dhana sisi tunawasaidia na kuwarithisha majukumu ili baadae sisi tukifa muendele kusaidia na kuendesha familia, maana pia hapo hapo shughuli zako nyingi anafanya housegairl ...
Kama anafanya housegirl sawa.
 
duuu!! sijawahi kusikia hiyo,case ipo katika 0.0001% ya wanaume then una generalize kwa wote
Kama kitu haujawahi kukisikia wala kukishuhudia wewe basi haimaanishi kwamba ndo hakipo au hakijawahi kutokea
 
Kama mnaelewa hilo sasa mbona hiyo hali ya mapenzi kuisha ikitokea kwa mwanamke kuacha kumpenda mumewe huwa mnatulaumu na kusema kuwa sisi ni wakatili?
Mapenzi ya kweli hayaishi, mali na material zingine ndio huisha.
Maamuzi ya kumuacha mtu hayaji from nowhere, mtu unaweza ishi nae kila akiamka asubuhi akakuona moyo unajaa majuto kwa miaka 40, mtu wa hivyo naweza sema maisha aliyoyachagua yamemfanya awe katili[emoji3][emoji3].
 
Siyo useme vyovyote mwanamke anayeona muelekeo wa ndoa hawezi kukuchuna ila mwanamke ambaye haoni mueleko wowote wa kuolewa lazima akuchune sababu kumbuka unapomchezea unampotezea muda wake wa kuolewa

Wakati wewe hauna cha kupoteza maana wewe hata ukifika miaka 40 utaoa tu ila kwake miaka 40 ni ngumu kuolewa sasa kama wewe unampotezea muda wake kwanini na yeye asikupotezee pesa zako?
 
Hivi kwani bado unaongelea usawa au unaongelea mgawanyo wa majukumu? Kwani nani kasema wanaume na wanawake tuko sawa? Hebu nukuu hiyo sehemu niliyosema hivyo nikufafanulie vizuri, wanaume na wanawake hatuko sawa ila inapokuja kwenye swala la majukumu usiniambie maswala ya kujikinga na majambazi kitu ambacho ni tendo la dharura tu na siyo tendo la kila siku

Kwanza ulishakubaliana na mimi hapo juu kuwa ndoa ambazo mwanamke ndo anafanya majukumu mengi kuliko mwanaume hazifai yaani ilitakiwa mjadala uishie pale huku kwingine tunatafuta ligi tu yaani mimi mashaka yangu makubwa ni pale ninapoona mwanamke anafanya majukumu mengi kuliko mume wake yaani hiyo tu ndo hoja yangu ya msingi na hapa ndipo wanaume wengi wanapobisha

Mada yako inaongelea madai ya wanaume kusema kuwa wanawake mnataka usawa wa kijinsia na sio vinginevyo, hivyo basi hata comments zangu tangu awali zimejikita kwenye kiini cha mada yako(usawa) sasa unapouliza kuwa bado tunaongolea usawa.. nnashangaa sana maana hapo sasa tunakuwa tunaenda kwenye mada nyingine ndani ya mada.

Pili, huwezi ukasema mwanamke na mwanaume hawako sawa halafu hapo hapo unataka majukumu ambayo hata kitamaduni ni ya kwako na Mimi niyafanye. Unapoongelea mgawanyo wa majukumu based on gender huwezi ukaniambia Mimi nioshe vyombo na kupika huo sio mgawanyo wa majukumu my dear na ukitaka hivyo basi kubali na wewe niwe nakubebesha majukumu ya ulinzi na kuchimba shimo la choo siku moja moja.

hizo ndoa unazopenda kuzitolea mfano sijui unazioneaga wapi.
 
Back
Top Bottom