Sawa ila inakuwaje pale mnapotaka wanawake wawasaidie kutafuta pesa na kuhudumia familia?
mwanamke mpumbavu huvunja ndoa kwa mikono yakeTatizo hawa wenzetu Wanaongozwa na ubinafsi zaidi...mfano mwanaume akichepuka anaona ni halali yake kuchepuka ila mwanamke akichepuka ataambiwa ni malaya.... Mwanaume akizingua ndoa ikavunjika mke wake ataambiwa siyo mvumilivu,,, Mara sijui unatakiwa kumuombea mume wako..ila mwanamke akizingua ndoa ikavunjika ataambiwa ana tabia mbaya na mwanaume hataambiwa anatakiwa kumvumilia na kumuombea mwenzake
wanaume wanapenda wanawake wasiohoji kabisa hata pale wakiona mambo hayakai sawa....ukihoji unaambiwa unashindana na mwanaume, unataka usawa n.k. but mwanaume nani aliwaambia sisi siyo wanadamu? Sisi siyo wa kuhoji? Kwamba tukihoji ni kutaka usawa? Kwamba ninyi mna haki ya kukosea ila sisi hatuna? Kwamba ninyi ni bora kuliko sisi?
Siku mkiacha ubinafsi mtaacha na huu msemo wa kwamba wanawake tunapenda usawa
N.B Sisi kama binadamu tuko sawa humanly lakini mwanamke hawezi kuwa mwanaume na mwanaume hawezi kuwa mwanamke. Kila mtu atambue haki za mwenzake katika familia, ndoa na jamii kwa ujumla.
Vizuri sana hata wanaume walipoambiwa watakula kwa jasho lao walipewa uwezo wa kustahimili kutafuta pesa juu chini na kuhudumia familia sasa inashangaza wanawaume wa leo wanaposhindwa majukumu yao na kutaka wake zao wawasaidieUnakosea sana. Huwezi kusema uwezo aliopewa mwanamke ni mkubwa kuliko mwanaume kwa sababu ameumbwa' kike' hivyo huna sababu ya kumsikitikia kwa maana wakati anaumbwa amepewa na uwezo wa kuyastahimili hayo unayoyaona ni magumu. Kila mtu ana size yake
Hahahaha unajibu kirahisi sana unajua ni kwanini shetani alimuita mwanamke ndo ale tunda halafu akamwambia ampe mwanaume? Kwanini asingemuita mwanamume ndo ale kwanza halafu ampe mwanamke? Najua utakuja na jibu lako hilo hilo kuwa wanawake ni dhaifu kuliko wanaume kitu ambacho siyo jibu la hayo maswali niliyokuuliza anyway ngoja nikuache uamini unachoaminiNadhani ni kwa sababu alijua kabisa mwanamke ni kiumbe dhaifu sana yaani hata kujitawala tu mwenyewe hawezi, hivyo anahitaji kutawaliwa maisha yake yawe katika mstari mnyoofu.
duuu!! sijawahi kusikia hiyo,case ipo katika 0.0001% ya wanaume then una generalize kwa woteKuna mada ilianzishwa humu kuwa je ni sawa mwanamke kumtongoza mwanaume? Niliona wanaume wengi walisema ndiyo eti kama tumewapenda tusiogope kuwatongoza ila wanawake wengi walisema hapana kutokana na tamaduni za Africa mwanaume ndo anayetongoza
Na hata mtaani pia naona wanaume wengi wanataka na wanawake tuanze kutongoza kama wao ila wanawake wengi wanaona aibu na hata wanaotongoza wenyewe wanatongoza kwa ishara na siyo moja kwa moja nikajiuliza sasa hawa si ndo wanasema hawataki usawa? Sasa na wanawake tukianza kutongoza kama wanaume hakutakuwa na usawa kweli hapo?
vyovyoteHuyo mwanamke unayetembea naye unakuwa na mpango wa kumuoa na kutokumsaliti?
jibu swali hao watoto unazaa na wanawake wenzake au??Yaani unafananisha zoezi la kumwaga mbegu tu na zoezi la kubeba mimba, kuzaa watoto na kunyoyesha watoto? Wewe hebu nenda kabishane na wavulana wenzio huko mimi hapa nabishana na wanaume tu.
nakuuliza swali,unaniumiza swali,hivi unajielewa weweNipe definition yako ya akili halafu ndo nitakwambia tuna akili gani
Mapenzi ya kweli hayaishi, mali na material zingine ndio huisha.Kama mnaelewa hilo sasa mbona hiyo hali ya mapenzi kuisha ikitokea kwa mwanamke kuacha kumpenda mumewe huwa mnatulaumu na kusema kuwa sisi ni wakatili?
Siyo useme vyovyote mwanamke anayeona muelekeo wa ndoa hawezi kukuchuna ila mwanamke ambaye haoni mueleko wowote wa kuolewa lazima akuchune sababu kumbuka unapomchezea unampotezea muda wake wa kuolewavyovyote
Kitu pekee nnachojua Most Women demand equal rights and not equal Responsibilties
Hivi kwani bado unaongelea usawa au unaongelea mgawanyo wa majukumu? Kwani nani kasema wanaume na wanawake tuko sawa? Hebu nukuu hiyo sehemu niliyosema hivyo nikufafanulie vizuri, wanaume na wanawake hatuko sawa ila inapokuja kwenye swala la majukumu usiniambie maswala ya kujikinga na majambazi kitu ambacho ni tendo la dharura tu na siyo tendo la kila siku
Kwanza ulishakubaliana na mimi hapo juu kuwa ndoa ambazo mwanamke ndo anafanya majukumu mengi kuliko mwanaume hazifai yaani ilitakiwa mjadala uishie pale huku kwingine tunatafuta ligi tu yaani mimi mashaka yangu makubwa ni pale ninapoona mwanamke anafanya majukumu mengi kuliko mume wake yaani hiyo tu ndo hoja yangu ya msingi na hapa ndipo wanaume wengi wanapobisha