Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

kwa hiyo kumbe wanawake mnaishi kwa kufuata mitazamo ya kijamii,then mnasema mna akili
 
Hilo mbona linaeleweka mkuu? Sema sasa tatizo linakuja wanawake wasipofanya hizo kazi za kujitafutia kipato chao je wanaume mtawahudumia mahitaji yao yote kiuchumi bila kuwanyanyasa wala kusimanga?
Too late,mmeshajiingiza kwenye majukumu yasiyo wahusu kiasi kwamba mshazalisha tatizo jipya tayari la wanaume marioo..

Zamani ulikuwa huwezi kutoa mwanamke outing km huna hela sababu kwanza ilikuwa Ni aibu kutaka mwanamke alipe, siku hizi mnang'ang'ania basi na sisi tunapumzika tu na kulemaa.Mwanamke kama hela zimejaa nunua zawadi mpe,mpo busy sana kujishindanisha majukumu na wanaume SI tunawachora tu siku hizi mimba nyie,kufua nyie,kuosha vyombo nyie,uchungu nyie na kulea nyie, gharama zote nyie ila mradi mujiite strong woman na mngekuwa mnaweza na mimba mngejipa wenyewe.Tunawachora tu na harakati zenu za kijinga mwishowe wa siku SI kazi yetu kugonga nakukupa cheo za ustrong woman.

Mimi hadi leo hii siwezi kukaa na kumuomba hela mwanamke wangu wala hata kumkopa sijawahi .Nilishakataa kubehave kijinga jinga mbele ya mwanamke.
 
Sijaelewa mantiki ya hoja yako inaingiaje hapo
Ilikuwa ni rahisi sana shetani kumshawishi mwanamke kula tunda kuliko kumshawishi mwanaume, maana kama angemshawishi mwanaume angekutana na upinzani mkali na hatimae kushindwa kabisa, hivyo aliona haina haja ya kujisumbua na badala yake akaona ni rahisi sana kufanikiwa kumshawishi mwanamke maana ni mwepesi kudanganyika.

Kama ilivyokuwa rahisi kwa ccm kumnunua Waitala wala sio Lisu.
 
Ndiyo tunawaachia nyie kwa sababu ya huo mgawanyo wa majukumu sawa umesema mkeo kufanya hivyo ni kukusaidia sasa na wewe kumsaidia mkeo unaona nini?
 
huwezi kutenganisha hayo maandiko na tamaduni,unajiona ulivyo kilaza,hayo maandiko ni tamaduni za kiyahudi
Ni ngumu sana kwa great thinker kumwambia mtu kuwa ni 'kilaza'. Great thinker kwa kawaida anaweka context na maana ya maneno kwa mujibu wa context husika.
Huyo unaemwita kilaza, kwa mtazamo wangu, basis ya argument yake ni 'religious faith/ creed/ belief' au perspective. Unachotakiwa wewe kufanya ni kubomoa hiyo basis kwanza, na kumwambia basis anayotumia ni weak wakati huohuo ukionesha basis yako ni strong.
 
Sasa kama mwanamke ni mwepesi kudanganyika na mwanaume ni mgumu kudanganyika kwanini ilihitaji mwanamke tu kumshawishi mwanaume kula tunda ilihali upande wa pili ilihitaji shetani ndo amshawishi mwanamke ili ale tunda?
 
Uzuri ni kwamba linapokuja suala la pesa wao ndio wanataka haki sawa.
Hapo kwenye pesa,kwenye kupata ndiyo wanataka haki sawa lakini kwenye kutoa hawataki haki sawa.
 
Yaani dada unaakili nyingi Sana, kwa majibu yako haya unaonekana unajitambua na kujielewa pia, hebu weka account number nikutumie muamala Sasa hivi
 
Siyo tamaduni za kiyahudi bali ni sheria za Mungu ambazo hauwezi kuzifananisha na tamaduni za kiafrika nilijua tu wanaume wengi nikiwaambia tuongelee maandiko mnayakwepa

Sababu mnajua maandiko kwa asilimia kubwa yanawabana ukilinganisha na tamaduni za kiafrika na huwa mnayafuata yale maandiko yanayowafaidisha tu basi ndo hivyo sasa kama hautaki tuongelee maandiko unanilazimisha tuongelee tamaduni zetu basi pita kushoto mimi nipite kulia maana mimi namuabudu Mungu siabudu mizimu ya mababu
huwezi kutenganisha hayo maandiko na tamaduni,unajiona ulivyo kilaza,hayo maandiko ni tamaduni za kiyahudi
 
kwa hiyo kumbe wanawake mnaishi kwa kufuata mitazamo ya kijamii,then mnasema mna akili
Hivi kuna jinsia inayoongoza kwa kufuata mitazamo ya kijamii kama wanaume? Wanaume asilimia kubwa mnafanya vitu kufurahisha jamii na huwa mnataka kufanya vitu vinavyowapa heshima kwenye jamii leo hii mwanaume anaogopa kuwa na mwanamke mmoja eti kisa ataitwa mwanaume Dar kwahiyo anaona ni sifa kuwa na wanawake wengi ili jamii imheshimu imuone na yeye ni kidume uongo? Acha unafiki kijana.
 
Hivi wanawake tumepigania mambo mangapi? Mbona hilo tu ndo jambo pekee ambalo wanaume mmelikubali ila mengine mnapinga hadi kesho ila hilo tu la sisi kuingilia majukumu yenu ndo mmeacha lipite mngepinga na mngekataa yote kupita basi kama kweli hamtaki usawa
 
Ndiyo tunawaachia nyie kwa sababu ya huo mgawanyo wa majukumu sawa umesema mkeo kufanya hivyo ni kukusaidia sasa na wewe kumsaidia mkeo unaona nini?

Mke kuamua mwenyewe kunisaidia kwenye suala la kutafuta pesa pasipo kushurutishwa na mtu haimaanishi kwamba ndio tiketi ya Mimi kumsaidia yeye kwenye yale majukumu yake ya kike. Na kama ikitokea nimefanya hivyo basi lazima pawepo na sababu za msingi sana zilizo nje ya uwezo.

Siwezi kumsaidia kazi za kike maana naamini kabisa hata yeye mwenyewe mbali na kutafuta pesa kuna vitu vingi sana hawezi kunisaidia nikimwambia avifanye, hivyo kutafuta pesa isiwe sababu ya yeye kutaka mimi nifanye majukumu yake.

Hiki unachokisema inatakiwa kiwe applied kwa wale wanaume wanaoishi kwa kutegemea vipato vya wake zao na sio vinginevyo.
 
Maana yake mmekuwa na viburi na kuidharau amri ya Mungu na kuifuta ya mzungu
 
Sawa mkuu hapo nimekuelewa!
 
Sasa kama mwanamke ni mwepesi kudanganyika na mwanaume ni mgumu kudanganyika kwanini ilihitaji mwanamke tu kumshawishi mwanaume kula tunda ilihali upande wa pili ilihitaji shetani ndo amshawishi mwanamke ili ale tunda?
My dear let me put it blatantly.

Men control everything in this world while women merely control men emotionally.

listen the song "we run the world" by rihana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…