Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Hahahaha naona wengi mnakazania kutoa huo mfano wa kuvamiwa na majambazi utadhani hayo majambazi ni sehemu ya maisha yaani kwamba yanavamiaga nyumba yenu kila siku mkuu tuongelee yale majukumu ambayo ni sehemu ya maisha yenu yaani yanafanywa kila siku

Mkianza kutolea mifano ya majambazi ni sawa na sisi tuanze kutolea mifano ya wanawake kubeba mimba na kuzaa watoto kitu ambacho hakihusiani na hatuna haja ya kufika huko hapa tunaongelea majukumu ambayo mtu yeyote anaweza kuyafanya na siyo majukumu yanayotokana na maumbile
Katika maisha Ya mwanadamu hitaji moja wapo kubwa na la muhimu ni ulinzi.

hatuweza tukaacha kutoa mfano wa majambazi wakati ndio yanayotutushia uhai wetu...

nakuuliza tena, mimi niko tayari kuosha vyombo,kupika,kupiga deki n.k

sasa je, wewe uko tayari kupambana na hata vibaka waliokuja kutuvamia huku mimi nimejificha chini ya uvungu na watoto?

maana ndio mnachokitaka hasa kuwa sawa na mwanaume kwenye kila kitu.
 
You need to come up with concrete evidence to support your argument(s).

Ndo maana nikakwambia hauwezi kunielewa hadi nikutolee ufafanuzi wa kina ambao nao naona kama vile bado hautauamini kwahiyo wacha nikuache hivyo hivyo
 
Nielimishe sasa sio unipe pole.

maana hizo akili nnazozilenga Mimi ndio zinaendesha Maisha yetu kwa kiasi kikubwa
Kwahiyo wewe unadhani kwamba Mungu alipowaambia wanaume muishi na wanawake kwa akili alimaanisha muishi nao kwa akili hizo za darasani na za ugunduzi?
 
aisee kama zipo ndoa za hivi, basi huyo mwanamke na yeye ana kihere here cha kukaa kwenye hiyo ndoa. Binafsi siwezi hata kumshauri dada yangu aolewe na mwanaume na dizaini hiyo.

Na ndoa kama hizi usipende kuzitoles mifano maana naamini kama zipo basi ni chache sana.
Mnajifanya hamzioni ndoa ambazo wanawake wanatafuta pesa na wanawasaidia waume zao kuhudumia familia? Kitu usipokiona au kukisikia wewe basi haimaanishi kwamba hakipo au hakijawahi kutokea haya mambo yapo na tunayashuhudia kwenye ndoa nyingi

Na kuna ndoa nyingine mwanaume hatimizi kabisa majukumu yake yaani yote kamuachia mke kwahiyo mwanaume hafanyi chochote nyumbani ila mwanamke anafanya majukumu yote ya mumewe na ya kwake sasa nikiuliza ni wanaume wangapi wanaweza kufanya majukumu yao na ya wake zao huku wake zao wamerelax tu sidhani kama yupo hata mmoja
 
Katika maisha Ya mwanadamu hitaji moja wapo kubwa na la muhimu ni ulinzi.

hatuweza tukaacha kutoa mfano wa majambazi wakati ndio yanayotutushia uhai wetu...

nakuuliza tena, mimi niko tayari kuosha vyombo,kupika,kupiga deki n.k

sasa je, wewe uko tayari kupambana na hata vibaka waliokuja kutuvamia huku mimi nimejificha chini ya uvungu na watoto?

maana ndio mnachokitaka hasa kuwa sawa na mwanaume kwenye kila kitu.
Kwani kuzaa siyo hitaji la mwanadamu? Kwahiyo wakati sisi tunafanya hayo ninyi mtakuwa mnazaa si ndiyo? Be logical my friend wanaume kutulinda ni jukumu linalotokana na maumbile kwa sababu mmetuzidi nguvu

Na vile vile sisi kuzaa ni jukumu la kimaumbile ambalo wanaume hamuwezi kulifanya sasa tuachane na hayo majukumu ya asili ya kimaumbile tuongelee majukumu ambayo kila mtu anaweza kuyafanya hivi kuna kazi yoyote ya ndani ambayo wanaume hamuwezi kujifunza na kujua kuifanya?
 
aisee kama zipo ndoa za hivi, basi huyo mwanamke na yeye ana kihere here cha kukaa kwenye hiyo ndoa. Binafsi siwezi hata kumshauri dada yangu aolewe na mwanaume na dizaini hiyo.

Na ndoa kama hizi usipende kuzitoles mifano maana naamini kama zipo basi ni chache sana.
Basi hizo ndizo ndoa ambazo ninazilaani kila siku na si nyinginezo
 
Kwahiyo wewe unadhani kwamba Mungu alipowaambia wanaume muishi na wanawake kwa akili alimaanisha muishi nao kwa akili hizo za darasani na za ugunduzi?
Women are stupid~Esther villar(your fellow woman) not my words

Wanawake mnahitaji uangalizi wa mwanaume hili maisha yaende, tukiwaacha nyie wenyewe tu dunia itakuwa sio mahala salama sababu nyie ni emotional driven decision makers na sio logical driven decision makers kama walivyo wanaume.

Ndio maana tunaambiwa sisi tuishi na nyie kwa akili na sio nyie muishi na sisi kwa akili, maana akili zenu haziwatoshi kwanzia nyie tu.
 
Hivi kati ya mwanaume na mwanamke ni nani ana nguvu ya ushawishi?
 
Kwani kuzaa siyo hitaji la mwanadamu? Kwahiyo wakati sisi tunafanya hayo ninyi mtakuwa mnazaa si ndiyo? Be logical my friend wanaume kutulinda ni jukumu linalotokana na maumbile kwa sababu mmetuzidi nguvu

Na vile vile sisi kuzaa ni jukumu la kimaumbile ambalo wanaume hamuwezi kulifanya sasa tuachane na hayo majukumu ya asili ya kimaumbile tuongelee majukumu ambayo kila mtu anaweza kuyafanya hivi kuna kazi yoyote ya ndani ambayo wanaume hamuwezi kujifunza na kujua kuifanya?
my statements are still in logical table.

Suala la ulinzi wala hata sio jukumu la kibailojia, ni jikumu ambalo jinsia yoyote anafanya vizuri kabisa. Ndio maana siku hizi mnakuwa mpaka mageneral wa jeshi, ukienda kwenye jeshi la marekani hadi vitengo vigumu kama navy seal kuna wanawake wapo.

Hii inatuonyesha kuwa tofauti zetu za kibailojia hazikufanyi wewe ushindwe kuwa mlinzi wa familia.

Naona wewe ndio unaingiza masuala ya kuzaa kitu ambacho ni irrelevant kabisa hapa.

Nakuuliza tena, kuosha vyombo, kupiga deki n.k mimi niko tayari, je wewe uko tayari kuniokoa kwenye hatari yoyote ile hasa dhidi ya maadui wenye silaha kali?

ukishindwa kujibu hili swali basi mjadala unaishia hapa, na utakuwa umekubali kuwa mwananke kamwe hawezi kuwa sawa na mwanaume.
 
Wanataka tufanye majukumu yao kama yapi?

Mie nachoona kiko fair ni kila mtu haijalishi ni mwanaume ama mwanamke kufanya anachoweza kufanya ambacho kiko ndani ya uwezo wake....sio eti kusubiri ooh hiki kitu anatakiwa afanye mwanamke ama kile afanye mwanaume

Hapo hapo unapotaka mwanamke afanye awezacho na mwanamume kadhalika ndipo pasipo na usawa. Usawa ni kutekeleza majukumu yote bila ubaguzi, labda tu kwa kupeana zamu.
 
Tatizo ni sisi wanaume kuacha majukumu yetu na kuwaachia wanawake wayafanye. Kwa vyovyote vile lazima wataanza kujiona wame qualify kutaka usawa na wanaume.
Tatizo sio hilo, ni movement zilizoanzia ulaya kutaka haki sawa zimepelekea wanaume kuporwa majukumu yao, na sasa tunawalea watoto wetu katika mazingira ya kutokuchukua majukumu yao. For every action there is an equal and opposite reaction.
 
Kama hayo majukumu ni mepesi mbona wanaume wengi huwa mnayachukia? Tunasema umsaidie mkeo hayo majukumu endapo na yeye anakusaidia majukumu yako ila kama yeye hakusaidii majukumu yako basi haina haja ya wewe kumsaidia majukumu yake
Nani aanze??
 
Je kama mama anaumwa na baba akaamua kumsaidia? Ndo maana nikakuuliza kwahiyo mama kumsaidia baba majukumu yake ndo siyo kitu cha ajabu? Mbona haujajibu swali?

Hii ndo shida ya kuwadharau wanawake hatimaye mnadharau hadi majukumu yao bado sijaona sababu ya mwanaume kukataa kufanya hizo kazi kwani akizifanya anaumwa au anakufa? Nipe madhara makubwa anayopata mwanaume akifanya hizo kazi kama hakuna basi kaeni kimya

Kuna wanaume wengi tu huko wamekimbia majukumu yao na hawahudumii tena familia ila hao ndo mnawaona wajanja na wanaohudumia familia zao lakini wanawasaidia wake zao kazi mnawaona wajinga?

Halafu unavyobisha hapo utadhani hakuna kabisa kwenye jamii ya leo wanaume wanaofanya hizo kazi looh mbona wamejazana na kila kukicha na wanazidi kuongezeka usipofanya wewe watafanya wanaume wenzio halafu nimekwambia nipe maana ya bwege haujanipa naona unazunguka tu
nauliza hivi,baba ako kuosha vyombo, kukata nyanya na vitunguu,kufagia uwanja,kukuna nazi, kupiga deki,wewe unaona sawa????
 
Kwani kuzaa siyo hitaji la mwanadamu? Kwahiyo wakati sisi tunafanya hayo ninyi mtakuwa mnazaa si ndiyo? Be logical my friend wanaume kutulinda ni jukumu linalotokana na maumbile kwa sababu mmetuzidi nguvu

Na vile vile sisi kuzaa ni jukumu la kimaumbile ambalo wanaume hamuwezi kulifanya sasa tuachane na hayo majukumu ya asili ya kimaumbile tuongelee majukumu ambayo kila mtu anaweza kuyafanya hivi kuna kazi yoyote ya ndani ambayo wanaume hamuwezi kujifunza na kujua kuifanya?
kwenye kuzaa unazaa na wanawake wenzako au???
 
Back
Top Bottom