Ndiyo hakuna kitu kinauma kama mwanamke anasaidia majukumu ya mwanaume wakati mwanaume hasaidii majukumu ya mwanamke halafu mwanamke anasikia mwanaume anachepuka na wanawake wengine kwa kisingizio cha kuwa mkewe kajisahau sana kwenye ndoa na hamridhishi tena kama kwenye uchumba
Sasa kwa akili ya kawaida tu hebu fikiria mwanaume na mwanamke wanaamka alfajiri wote wanaenda kazini ila mwanamke ndo asafishe nyumba akitoka hapo ajiandae yeye akamuandae na mumewe ndo waende kazini wakati huo mume amekaa tu haya kurudi wanarudi wote usiku ila mwanamke akirudi aingie jikoni apike ale yeye amlishe na mumewe wakati huo mume amekaa tu wakimaliza hapo waingie chumbani wote washughulike kitandani mwanamke asikae kama gogo
Haya weekend mume unakuta mume yupo nyumbani ila mke ndo atapika, atafua, ataosha vyombo na atasafisha nyumba wakati huo mume amekaa tu sebuleni lakini mume akilipa kodi mke atanunua mahitaji ya nyumbani mume akilipa bili ya umeme mke atalipa bili ya maji na mume anakuwa hamhudumii tena mkewe kwa sababu mke naye anatafuta pesa zake wakati huku mke anamlea mume na ukizingatia huyo mume siyo kilema
Halafu ikitokea mwanamke akapunguza ufanisi katika hayo majukumu huyo huyo mwanaume anachepuka na mwanamke ambaye hampikii kila siku na wala hamfulii na bado huyo mwanaume anauhonga huo mchepuko na afanya yote hayo eti ili kumkomoa mke wake ajirekebishe sasa naomba nikuulize wewe wanaume mnaweza kufanya hayo niliyoyataja hapo ambayo anayafanya mwanamke?