Nitasema kwa uzoefu na yale niliyoyashuhudia. Mke wangu ni mwanaharakati wa haki za wanawake ambapo kwenye issue zake nyingi za uanaharakati huwa namsaidia kuweka sawa. Niliwahi kumwambia hivi “Vita yenu ya haki sawa haitafanikiwa kamwe mpaka pale mtakapojua adui wa kweli kwenye hiyo vita yenu ni nani” mwanzoni tulibishana kidogo kwasababu hakuelewa nilimaanisha nini lakini Siku hizi anaelewa na amekubaliana kauli yangu. Kiuhalisia adui wa haki za wanawake ni wanawake wenyewe na kamwe sio wanaume.
Ntatoa mifano kadhaa, Leo hii utakuta mwanaume ametelekeza familia yake kwasababu ya mwanamke mwingine ambaye anajua kabisa kwamba kuwa kwake na mwanaume huyo kunamuumiza mwanamke mwenzake ambaye ndiye mwenye haki ya kuwa na mwanaume huyo. Leo hii wanawake wenyewe wanasifiana kuwaumiza wanawake wenzao kwa kutoka na wanaume wao tena bila huruma.
Mfano mwingine ni uhalisia wa mazingira. Wanawake wengi wamekuwa wanadanganyana kuhusu haki sawa inayopelekea ndoa nyingi kuvunjika na kuzalisha “single mothers wengi” tabu ni pale hao wanawake tena wanapoishi kwa fadhila za wanaume wengine (Hii inafanya wanaume hao kuwadharau wanawake hao na kamwe huwezi kudai haki sawa kwenye situation hii)
Kumekuwa na malalamiko mengi sana ya wanawake Siku hizi kuwa wanawake ndio wamekuwa bread winners na sio wanaume. Yes hizi ndio effects za haki sawa, kama ambavyo wanaume wamekuwa hawalalamiki kuwa bread winners huko nyuma wanawake pia waache kulalamika sasa kuwa wamekuwa bread winners.
Kuna suala la kibaiolojia, kuzaa ni suala la kibaiolojia la wanawake na Hali a substitute, hilo halifanyi mmoja kuwa superior ya mwingine kwenye suala la uzazi. In fact attachment ya mtoto haiko kwenye kubeba mimba na kuzaa Bali hutengenezwa baada ya hapo na ndio maana nyumba nyingi Siku hizi watoto wako attached zaidi kwa wasichana wa kazi kuliko wazazi wao. So kama baba pia anataka kuwa attached na mtoto wake anaweza kutengeneza hiyo attachment. Kama watu wanakutana ukubwani na kuwa wapenzi na kuwa na hiyo bond kiasi cha kutengeneza instincts pale mwingine anapopata tabu hata akiwa mbali itakuwa kwa mwanao mwenyewe? Mimi I am too close to my son kuliko mama yake, nikiwepo mimi hamtaki kabisa mama yake.
Mwisho wa Siku ni kwamba mazingira yamebadilika ambayo yanalazimisha pia mfumo wa maisha ubadilike. Lakini bado tuendelee kuthamini tofauti zetu za kibaiolojia ambazo zinafanya jinsia moja kufanya vizuri kwenye sehemu Fulani kuliko nyingine. Wale wanaoamini katika dini (Ukristo na uislam) wanajua maandiko yanavyosema juu ya namna ya kuishi kwa wanawake na wanaume. Wasioamini katika dini na wanaamini katika tamaduni, Mila na desturi pia wanajua zinasemaje juu ya hili.
Wengi wetu tumerithi issue ya haki sawa kutoka nchi za magharibi lakini angalieni namna gani wao wanapractice hili tofauti kabisa na matangopori wanayotulisha huku. Wao wote wanafanya kazi na wanaweka pesa mezani na kupanga matumizi ya pesa yao, bado mama ndio mwenye jukumu ya kuhandle issue za watoto hii hata wao haina mbadala na kwao hawaamini sana kwenye house maids maybe babysitters pale wanapokuwa na shughuli zinazowaweka wote nje kwa muda masaa mengi. So wanathaminj hizo tofauti za kibaolojia.
Mwisho nakumbuka maneno ambayo Makamu wa rais aliwahi kusema “Mimi ni makamu wa rais nikiwa ofisini, nikiwa nyumbani mimi ni mke na ninampikia mume wangu, ninamnawisha na ninampigia magoti”