Hivi wanaume wengine mnawezaje hivi vitu Mimi binafsi siwezi na sitaweza kamwe

Hivi wanaume wengine mnawezaje hivi vitu Mimi binafsi siwezi na sitaweza kamwe

Siku vyuma vikikaza utaambiwa una michepuko unayoitoa out,ogopa mazoea halafu yakakatika utapata taabu sana katoka kwa hawa viumbe

kwa upande wangu nina CHUMA kimoja KIKALI sanaaa,,,,, yaan kuna muda unatamani akusindikize hata dukani... ilimradi ULINGISHE tu...

kuhusu vyuma kukaza.. sizani kama atanisumbua maana yeye ndio anapenda kunitoa OUT.. mie siku moja moja sana maana sipendi Kutoka OUT..
 
Mie najua katika ndoa kikubwa maelewano tu na kila anayekifanya ndoani ambacho mwenzie anaona hawezi basi ndio maelewano hayo.

Japokuwa namba 1, 2 na namba 06 uko sahihi. Ila hiyo namba nne haikwepeki hasa utakapofanya kitu chenye kuudhi na muhusika akashindwa kukustahi aiseee kibao kitakuhusu kisha kuombana radhi baadae.
Uwiii bora yote yasifanyike ila kibao ni kosa kubwaaaaaaa ambalo utakuwa umelifanya katika maisha yangu,na itabidi nichukue kwanza diary ninote tukio hilo ili liwe katika historia ya maisha yangu nikimaliza nianze kukupa dozi
 
Kabla sijakuuliza umri wako..... Naomba nijue kama unamke...???
 
Yes, kila kitu ni makubaliano tu.
Kama mtu na mkewe wamejipangia utaratibu wao, we inakuhusu nini??

Kama mwanaume ameridhika kupika, kuosha vyombo, kutandika kitanda nk, hakuna shida yoyote.

Kiranga anakwambia mambo ya ngoswe muachie ngoswe mwenyewe

Faragha za watu hizoo
Haya makubaliano ndo yanaleta matatizo mbeleni na ukichunguza kwa undani wa migogoro ya ndoa chanzo kimojawapo ni kuvurugika haya makubaliano na sasa kila mmoja ni mbabe kwenye ndoa

Hapa ndo utasikia kila mmoja anajipikia yaani mwanamke anapika chakula chake kisha na mwanaume anapika chakula chake,ogopa hii kitu
 
Haya makubaliano ndo yanaleta matatizo mbeleni na ukichunguza kwa undani wa migogoro ya ndoa chanzo kimojawapo ni kuvurugika haya makubaliano na sasa kila mmoja ni mbabe kwenye ndoa

Hapa ndo utasikia kila mmoja anajipikia yaani mwanamke anapika chakula chake kisha na mwanaume anapika chakula chake,ogopa hii kitu
Ukiona kuna mgogoro jua hakukuwa na makubaliano, au mmoja wapo kaamua kuvunja makubaliano.
 
Habari wanajamvi,bila kupoteza muda kwa kweli sijui nimeathiriwa na jamii yangu au la pamoja na kusoma kote huko binafsi siwezi kufanya mambo yafuatayo kwenye ndoa

1,Kupangiana zamu za kupika,kufua,kuosha vyombo na usafi wa ndani,yaani niwe na mke wa ndoa halafu tunapangiane na zamu za kupika haitatokea

2,Kupikiwa na house girl na mwanamke yupo amekaa hata kama mke yupo kazini ,namwambia house girl pika mle na watoto,nitamsubiria mke atoke kazini aje anipikie,kama anaumwa nitapika vizuri sana,lakini yupo sofani anasaapuka na facebuka Mimi ndo napika haitatokea


3, kila weekend natoka out na mwanamke hiyo haipo,labda kwenye matukio muhimu kama baadhi ya siku kuu na kama tuna watoto tunaenda wote na kama bado lala ndani

4,kupigwa Kofi na mwanamke,yaani anigombeze atakavyo ila epuka mambo mawili ,Kofi au tusi,yakitokea hayo ujue hapo hakuna ndoa,na unaweza ukala kipigo cha mbwa koko

5,kusalimiana asubuhi,si tunalala kitanda kimoja,hata kama game ilichezwa SAA 11 tukishamaliza lazima mwanamke anisalimie tena ashuke kitandani apige magoti anisalimie ndo aondoke kwenda kwenye shughuli zingine

6, kuamka asubuhi sana ni jukumu la mwanamke aniandalie chai na maji ya kuoga sio niamke nimuache amelala niandae chai,hapo binafsi siwezi

7,kama tuna watoto wakubwa wanaokaribia balehe au waliobalehe,hapa kama mwanaume utakuwa strong watoto watakuwa na tabia nzuri na kama hautakuwa strong ujue mke wako atachangia watoto wako kuharibika,hii ndo stage baba wa mji unatakiwa uonyeshe ubabe wako bila ubabe,ndo machangudoa na watumia madawa ya kulevya yataanzia hapa,mkeo anatakiwa awe anakupa taarifa za ndani za mtoto wako wa kike na wa kiume na baba unatakiwa umwambie mwanao wa kike na kiume live mambo duniani bila kumumunya maneno na mstakabali wa maisha yao na wa Mali zako,kuwa mali zangu unazoziona ni zangu na mama yenu tu,kama utakaa siku moja ufikirie hizi mali umefeli,ni jukumu lako kupambana utafute Mali zako

Mapenzi mbashara na kubembelezana yanaishia kwenye uchumba

Ila sometimes ukiwa hivi ndoa yako itadumu lakini kama unataka yanayofanywa kwenye tamthilia ujue huna ndoa hapo,mwanaume acheze part yake na mwanamke acheze part yake kama mwanamke na mwanaume pia,Usomi wa mwanamke uishie getini,na uheshimiwa unaishia mlangoni

Nauliza hivi wale wanaofanya kinyume cha haya yaliyopo hapo juu mnayawezaje?
siamini kam mwanamke ni wa shughuli zote hizo dunia imebadilika kijana
 
Mkuu mimi ni.mkolon ila wee ni mkoloni sugu.

Mwanamke anahitaji kubembelezwa kisha utaona yalomazur anayafanya. Yalomabaya anayaacha.

Usipompenda mkeo kamwe usikae ukategemea yeye akufanyie unayopenda .
 
Back
Top Bottom