Hivi wanaume wengine mnawezaje hivi vitu Mimi binafsi siwezi na sitaweza kamwe

Hivi wanaume wengine mnawezaje hivi vitu Mimi binafsi siwezi na sitaweza kamwe

Habari wanajamvi,bila kupoteza muda kwa kweli sijui nimeathiriwa na jamii yangu au la pamoja na kusoma kote huko binafsi siwezi kufanya mambo yafuatayo kwenye ndoa

1,Kupangiana zamu za kupika,kufua,kuosha vyombo na usafi wa ndani,yaani niwe na mke wa ndoa halafu tunapangiane na zamu za kupika haitatokea

2,Kupikiwa na house girl na mwanamke yupo amekaa hata kama mke yupo kazini ,namwambia house girl pika mle na watoto,nitamsubiria mke atoke kazini aje anipikie,kama anaumwa nitapika vizuri sana,lakini yupo sofani anasaapuka na facebuka Mimi ndo napika haitatokea


3, kila weekend natoka out na mwanamke hiyo haipo,labda kwenye matukio muhimu kama baadhi ya siku kuu na kama tuna watoto tunaenda wote na kama bado lala ndani

4,kupigwa Kofi na mwanamke,yaani anigombeze atakavyo ila epuka mambo mawili ,Kofi au tusi,yakitokea hayo ujue hapo hakuna ndoa,na unaweza ukala kipigo cha mbwa koko

5,kusalimiana asubuhi,si tunalala kitanda kimoja,hata kama game ilichezwa SAA 11 tukishamaliza lazima mwanamke anisalimie tena ashuke kitandani apige magoti anisalimie ndo aondoke kwenda kwenye shughuli zingine

6, kuamka asubuhi sana ni jukumu la mwanamke aniandalie chai na maji ya kuoga sio niamke nimuache amelala niandae chai,hapo binafsi siwezi

7,kama tuna watoto wakubwa wanaokaribia balehe au waliobalehe,hapa kama mwanaume utakuwa strong watoto watakuwa na tabia nzuri na kama hautakuwa strong ujue mke wako atachangia watoto wako kuharibika,hii ndo stage baba wa mji unatakiwa uonyeshe ubabe wako bila ubabe,ndo machangudoa na watumia madawa ya kulevya yataanzia hapa,mkeo anatakiwa awe anakupa taarifa za ndani za mtoto wako wa kike na wa kiume na baba unatakiwa umwambie mwanao wa kike na kiume live mambo duniani bila kumumunya maneno na mstakabali wa maisha yao na wa Mali zako,kuwa mali zangu unazoziona ni zangu na mama yenu tu,kama utakaa siku moja ufikirie hizi mali umefeli,ni jukumu lako kupambana utafute Mali zako

Mapenzi mbashara na kubembelezana yanaishia kwenye uchumba

Ila sometimes ukiwa hivi ndoa yako itadumu lakini kama unataka yanayofanywa kwenye tamthilia ujue huna ndoa hapo,mwanaume acheze part yake na mwanamke acheze part yake kama mwanamke na mwanaume pia,Usomi wa mwanamke uishie getini,na uheshimiwa unaishia mlangoni

Nauliza hivi wale wanaofanya kinyume cha haya yaliyopo hapo juu mnayawezaje?
Na ni marufuku kula chakula mwenyewe yaaaani akila tu na mm nasusa mzigo wiki hata 2
 
Kwa wanawake wa dunia ya leo sijui kama watakuweza..!
 
Mnaoolewa na wafalme mna kazi sana aiseee mnakuwa watumwa hiyo ya kupiga goti [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Huwezi kupangiana zamu na mme ya kupika au usafi akijisikia kukusaidia akussaidie
Mkeo atapata tabu sana
Unajua mume ni mfalme ktk ndoa so anastahili kupewa heshima zote za kifalme,ndo mana ktk dini yetu ya kiislamu mtume alisema "lau kwamba angeambiwa na mwenyez Mungu awaamrishe kiumbe kimsujudie kiumbe mwenzake basi angearisha mke msujudie mumewe.

Sitaki kutoka nje ya mada napenda kukuunga mkono hoja ya mtoa mada,
 
Mleta mada ulichoandika hapa ni 'vakues' zako na matarajio ya mwandani wako iwapo ukijaaliwa kumpata, nami nakuombea umpate. Katika maisha yetu ya kila siku wanaume na wanawake pamoja na mambo mengine tunajengwa na tunaishi kwa kuendeshwa na 'values' na matarajio yetu binafsi. 'Values's maana yake ni misingi ya maadili tunayoona kwamba ni muhimu sana kwetu sisi binafsi, hii inatokana na malezi yetu, imani, makabila, makuzi elimu na vingi vinavyotuzunguka, kwa lugha rahisi ni kwamba kila mmoja wetu ana vitu anavyoona kwamba kwake yeye vitu hivyo vya msingi (Values) ni muhimu na hakuna mjadala. Vinatofautiana hapa na pale lakini kila mtu anavyo - vitu hivyo tunaviona ni muhimu sana (kwetu) na tunatamani kila mwenzetu mwingine awe/afanye au afuate misingi hiyo (Vaules) kama tunavyotaka sisi. tunasahau kwamba sio kila unachokiona wewe ni muhimu na mwingine atakiona muhimu.

Mnapoingia kwenye mahusiano au ndoa ni muhimu kutafuta mtu ambaye mtakuwa mna values zinazofanana ili msipishane sana. Umewahi kusikia mtu akisema kwamba ' I like him/her because we share the same values' , maana yake ni kwamba mnaendana kwenye misingi muhimu ya kimaadili - na katika hali kama hii hakuna atakayemshangaa mwingine. Pia umewahi kuona unajaribu 'kumbadilisha mtu' awe unavyotaka wewe lakini lakini unashindwa? Ni kwasababu vaules zako na zake ni tofauti na values huwa hazibadilishiki hata ufanyeje. Umewahi kuona watu wamekutana kwa muda mfupi tu lakini wanaelewana sana - wame click kabisa, kumbe values zao zinaendana kabisa!

Mfano kuna watu wanaume/wanawake wanaamini katika kutoa mimba lakini wengine hawaamini kabisa - hata amebakwa atakuambia lazima azae hawezi kutoa mimba - hii matokeo ya misingi ya kimaadili/imani aliyolelewa nayo.

Mfano kuna wanaume wanaamini kwamba mwanamke anapaswa akae nyumbani apike/aangalie nyumba na kulea watoto lakini wengine wanaona fahari mwaname wake kufanya kazi/shughuli ya kipato - yote haya ni matokeo ya malezi/imani nk (values)
Mifano ni mingi

Umeshawahi kuona watu/wapenzi wanapendana kweli kweli lakini kila mara aidha wanaachana tena kwa hasira, na muda tu wanarudiana na hawaishi kugombana tena na tena, ukichunguza utakuta kwamba kuna mapenzi lakini kati yao lakini pia kuna tatizo la misingi ya kimaadili iliyotokana na malezi au makuzi (Values),

Mleta mada kuna baadhi ya watu watakushangaa kwabasababu wako kinyume na 'values' zako lakini wengine ambao wanaona sawa utakuta values zao zinaendana nawe.

Kila la heri.
 
Umesahau ile unaongea mwnamke anakupita pita hataki kukusikiliza

Na mkigombana umekaa zako kmya yeye anaendelea kufoka kama koka

Kama unaskiaga kuua bila kukusudia anifanyie huu wehu
 
Uzungu unawala wanaume wa ki africa sasa.ndio maana wanawake wamekuwa wanawapanda kichwani wanaume.
Mke wangu atamiliki jiko na kaz zote kuhusu usalama na usafi wa nyumba.Mm niulizwe mahitaji yote ya familia ila sio swaga za kizungu
 
Unadhani hayo hatuyafanyi baba tunayafanya kiroho safi lakini tu ndo na wewe unihudumie vizuri km malkia na unikaze nitosheke vinginevyo ntakufanyia kinyume ya hayo yote na ungenyooka fala wewe
 
Halafu na yote hayo unakuta huna pesa, wewe ni wale wanaume wa 50/50 kila kitu uchangie na mkeo. Ufalme huo hakikisha hapo ndani hadi sindano unanunua wewe.
 
Hapa unaongea tu Mkuu
Yani huyu hajawah kuta watu hasa wanawake wakichukia na mara nyingi hapa had mwanaume anapigwa hilo kofi sababu huwaga ni usaliti mi huwa hasira zinapanda sana naonaga angalau nikimtwisha kofi napata nafuu
 
Mie najua katika ndoa kikubwa maelewano tu na kila anayekifanya ndoani ambacho mwenzie anaona hawezi basi ndio maelewano hayo.

Japokuwa namba 1, 2 na namba 06 uko sahihi. Ila hiyo namba nne haikwepeki hasa utakapofanya kitu chenye kuudhi na muhusika akashindwa kukustahi aiseee kibao kitakuhusu kisha kuombana radhi baadae.
Et nin?
 
Umeongea point tupu ila hawa mabinti waliozaliwa baada ya kuingia multpartism wanaona unawabana
 
daaaahh" wewe utakuwa ni mjamaa tu " sio bure"...
 
Mimi siku akinitukana au kunifokea nitamcharaza na faru atajuta kuishi na mimi.
 
Back
Top Bottom