Hivi Wanaume wenzangu wa Dar mbona mnapenda kujazana KFC

Hivi Wanaume wenzangu wa Dar mbona mnapenda kujazana KFC

Fikra za kimaskini zikizidi sana hutengeneza chuki na husda kwa wengine.

Mtoa mada anza na kubadilisha fikra negatives na zakimaskini basi kilakitu utaenjoye na kufanikiwa.
 
Aha.
Sitaki kurudi pale japo mimi ni member wao na nina loyality reward yao. Ila waliniuzi chicken wing yangu wakiitia sweet onion sauce. Nikashindwa kuila vizuri. Aaaastaki kurudi labda wewe nikupeleke masai kinondoni vip

Sijawahi kufika hapo.... Nakusikiaga tu.,
 
Kiwango kinachohitajika kwenye mwili hakipimwi kwa kilogram za chakula unachomeza, ukifanya hivyo utalitanua tumbo na kuwa na kitambi fulani kinachofurahisha kama wale wachekeshaji wa kiume wanaozunguka mitaa ya Dar es salaam wakiwa wamevaa nguo za kike. Mwili unahitaji kiasi kidogo tu cha virutubisho muhimu kwenye vyakula tunavyokula ambavyo ukivipima kwenye mzani utakuta vina soma kwenye miligramu au mikrogramu ...mfano wa vidonge upewavyo hospitalini.

Chips ulizozitaja ukila gramu 300 tu ambayo haijafika hata nusu kilo utakuwa umeingiza mwilini kalori 1614 ambazo zinamtosha kabisa mwanaume wa shoka kufanya kazi za wagumu. Pamoja na chips kwenye sahani huwa kuna aidha nyama, samaki, mayai au mboga mboga ambavyo,.. huongezea kalori kiasi cha kufikia kalori 3000. Hiki ni kiwango kikubwa sana kitakachokufanya kuwa na ziada ya nishati mwilini inayoakisiwa na minyama nyama iliyonona na kitambi.

Uzi huu umekuja katika muda muafaka, maana tangu juzi watu wanakula bila kusaza na bado hatujagusa bia n.k.. Mwaka haujaisha bado,..Tujitahidi kula vyakula vilivyo kwenye mlingano na kwa kiasi. Heri ya mwaka mpya.
 
Wako pale kutafta mademu au wamepeleka madem zao,..mim ni m1 wao..

Hua sishib,vinaishia kwenye meno..tukitoka pale tunaenda kwenye kitimoto,..sasa cha ajab.mwenzangu kala pale kfc na kitimoto nacho tunaenda sawa yani...

Ndo ujue madem wa kibongo ni walafi kinoma
 
Back
Top Bottom