Hivi wanawake mnawatenda nini waume zenu, mbona makasiriko yamezidi sana huku vijiweni?

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Nilipita somewhere kwenye kijiwe cha kahawa mida ya jioni, nikakutana na waume za watu wanalaani vikali wake na ndoa zao, kiufupi wanajazana sumu. Nilijikuta mdomo wazi baada ya jibaba limoja kumkandia mkewe mpaka kufika hatua ya kububujikwa machozi, alibebelea kijifuko chenye kitoweo ndani yake, kauli yake ya mwisho alisema, "Hata hawa broila, nawapelekea tu viumbe wa Mungu wakale, maake sidhani kama wale ni viumbe wangu"

Jamaa mmoja akaanzisha kikolomboizo akisema kuwa hakuna mke wa mtu asiyeliwa nje ya ndoa, tena huenda wanakula majirani kabisaa, yaani unatoka tu, na jirani linaingiza mushedede chumbani kwako. Dah! Nilijikuta naanza kutafuna samaki wa 5000 niliyemnunua, nikawagawia kidogo kidogo, nikaamua kuingia tu bar. Pale nyumbani kuna kijana nimewahi kushuhudia akitaniana na mke wangu, huenda vichwa vyetu vinapita reli moja, kinachonisikitisha zaidi, huenda chake ni mwendokasi

Ila wanawake mnasemwa sana huku vijiweni. Ukikutana na mwanaume anazungumza mwenyewe, chunguza! Kuna mdomo wa mwanamke pembeni
 
Unasahau kwamba malaya wote walikua bikra mwanzoni. Kuna jamaa alikua analalamika hapa juzi kupigwa tukio na alioa bikra.
 
Pale nyumbani kuna kijana nimewahi kushuhudia akitaniana na mke wangu, huenda vichwa vyetu vinapita reli moja, kinachonisikitisha zaidi, huenda chake ni mwendokasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…