Hivi wanawake wanatamani tamani kama wanaume?

Nitakupambania upunguziwe hata TOZO na kodi kandamizi kwako mkuu... Congole kwako!
 
Ahha ha ha ha haadu. Kweli wewe ni ke?
 
Umeongea point moja hatari sana. Yaan inabidi hii comment ifunguliwe uzi na uwe sticky hapo juu.

Pia umenikumbusha kuhusu kesi ya marehemu Kobe Bryant aliwahi kufunguliwa kesi na mdada fln hv, huyo mdada alimtuhumu Kobe kulazimisha kulala nae so akadai fidia. Cha kushangaza hio siku mahakamani alikuwepo na mke wa Kobe, Vanessa Bryant. Sasa kilichotokea jamaa alikubali kweli alilala na huyo dem lkn hapohapo mahakaman akamwambia Vanessa(mke wake) kwamba Moyoni mwake yeye ndo mwanamke wa pekee. The rest is history lkn inasemekana couple ya Kobe na Vanessa ni kati ya couple bora na walitengeneza familia bora sana.
 
Kwa kifupi, mwanamke aliyeanza mahusiano kabla ya ndoa hafai kuwa mke wa ndoa, labda kama wewe ndiye uliyemlala tangu mwanzo. Mwanamke hakuumbiwa kupenda bali KUTII, mwanamume ndiye mwenye uwezo wa kupenda.

Huwa ikisemwa hoja hii watu wanakuja juu tu bila kuelewa, lakini ukweli ni kuwa kuna tofauti ndogo sana kati ya kahaba na mwanamke aliyekutana na wanaume mbalimbali nje ya ndoa. Wote ni makahaba ila mmoja amebadili mbinu na jina kwa kuita boyfriends. Sasa ukioa mtu wa aina hii jiandae kwa rough ride kwenye ndoa yako
 
Men love women by who they are.
Women love men by WHAT they are.

Ndio maana humu jukwaani kuna mathread meeengi wavulana wakihamasishana watafute pesa ili wawapate hata wake za watu. You see? Wanawake wanatamani, lakini sio sex, bali kuwa tofauti na wengine, kila mwanamke anatamani awe juu kuliko wote. Ndio maana watalala hata na masudi sura mbaya mradi tu ana uwezo wa kuwajengea status kwenye jamii.

Ukiwa huna pesa ama status kwenye jamii utatumia nguvu kubwa sana kudate na vibinti vinavyojiona high value, lakini ukiwa juu tu, basi huhitaji kuvifukuzia wanawake kwani wao ndio watakuwa wakipigana vikumbo kukutaka japo kufanya nao ngono tu.
 
Kisha ndipo uelewe, kuna wanawake huingia kwenye ndoa sio kwa malengo ya kindoa, bali hutafuta kujijengea status katika jamii. Kundi hili ndilo kubwa zaidi kwa sasa na ndio maana ndoa zimepoteza maana na talaka tiririka zimekuwa nyingi mno
 
Dah, mkuu umechambua vizuri sana na bila shaka wakuu wengine wamekuelewa vema sana. Binafsi nimeshuhudia hili ulilolisema na ndivyo lilivyo kwa asilimia 100 na nimelishuhudia kwa jirani yangu huku mtaani kwetu, yaani mwanaume ni mpole, anajali majukumu yake kwa familia kwa kiwango kikubwa sana(kuna watoto wawili ndani ya ndoa). Cha ajabu ni kwamba mwanamke anatoka hata ikiwa ni saa nne usiku kwenda kwa mchepuko, tena anaaga kabisa kwa mumuewe, eti oooh kuna mtu naenda naye out nikirudi utanifungulia mlango.

Mume kaona isiwe shida, kwa kua wapo na watoto akawa anamvumilia na hiyo michezo yake na kujiweka zaidi jirani na watoto. Yaani asubuhi kabla ya kwenda kazini anawaamsha watoto na kuwaandaa tayari kwa kwenda shule, na jioni anawahi kurudi nyumbani kuwaandalia chakula watoto wakati mkewe yuko kwenye mizunguko yake na michepuko yake.

Kwa kuona bado hapati uhuru vizuri, akaanza kuomba talaka kwa mumewe, eti anasema anataka talaka maana anaona mumewe kipato chake ni kidogo hawezi kumuhudumia anavyotaka yeye. Mume kajizuia kumpa talaka lakini akashindwa, akalazimika tu kuita ndugu zake na ndugu wa mke na kumpa talaka naye kuondoka kwenda kuishi mahali pengine.

Kwa kweli hawa wenzetu ni changamoto sana aisee!....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…