Hivi wanawake wenzangu wa JF mmeshaandika kuhusu Tanzania tuitakayo kwenye Stories of Change?

Habari Wanawake wote wa JF, Salaam ziwafikie mliko Wanaume pia hakika mnastahili pongezi kwa kuwa waibua mijadala na watoa maoni yanasaidia katika ujenzi wa Taifa letu kwa ujumla.

Leo naongoe na wanawake, jeshi kubwa, nina swali kwenu je, mmeshaanza kuandika, mmeshiriki shindano na kupost mawazo, maoni, ubunifu kuhusu Tanzania yetu? Kama bado, mnasubiri nini? Kama ndio pokea tano kwani utakuwa umechangia katika kuifanya Tanzania ijayo iwe njema kama ambavyo wengi tunaiota.

Shindano la Stories of change limekuwepo na sasa ni awamu ya Nne, binafsi nimekuwa nikifatilia pale wanapowatangaza washindi na kugundua ushiriki wa wanawake umekuwa hafifu kwani wakitangazwa wanaonekana kushinda wanaume kwa idadi kubwa, Wanawake tunafeli wapi? Kwanini hatuingii kutoa mawazo yetu na ninakubali wanawake tuna mawazo mazuri yanayohitajika kwa Taifa hili.

Ufuatiliaji wangu ulianza tangu shindano la kwanza ambapo nilifurahi kwani mshindi wa kwanza wa shindano hili alikuwa Mwanamke, na walikuwepo zaidi ya mmoja>>> Soma hapa
Wanawake wawagaragaza wanaume Stories Of Change Uzi huu niliuandika mara tu baada ya kuwaona washindi wa shindano la kwanza kabisa.

Niliendelea kufatilia shindano la Pili, tatu na sasa la nne, ndio maana nimejitokeza kuwahamasisha na kuwakumbusha kuwa tunahitajika kuandika kwa ajili ya Taifa na vizazi vijavyo kwani mawazo yetu yatalifaa taifa la leo na kesho na kwa maandishi tutaishi milele mbali na zawadi zitolewazo.

Haya wanawake tujitokeze kuandika kwa wingi kwenye Stories of Change kwani shindano hili ni letu sisi wanafamilia ya JF
 
Mshindi wa kwanza kabisa wa story of change alikuwa Mwanamke @Abbriana
 
Nikishinda nitachagua watu watatu wa kwenda nao dubai 😎
Una hela ya ziada ama wategemea hiyo zawadi tu
 
Mtumeeee.....mie ni huu mdomo tu, ila ukinipa niandike chochote, nakuwa bubu.
Yaani we acha tu.
Hizo vitu zina wenyewe mwaya🤭🤭🤭
Jirikodi basi halafu uandike uliyokuwa unayasema🤣🤣🤣
 
Mtumeeee.....mie ni huu mdomo tu, ila ukinipa niandike chochote, nakuwa bubu.
Yaani we acha tu.
Hizo vitu zina wenyewe mwaya🤭🤭🤭
Unarekodi kwenye sauti, halafu unahamishia kwenye maneno.... simple kabisaaa
 
Mimi wananiboa wanaokuja inbox kuomba kura. Mwaga andiko lako mtu likimgusa atakupa kura.
 
Back
Top Bottom