Hivi wanyama walimfanya nini Mungu?

Hivi wanyama walimfanya nini Mungu?

Mkuu; Ni nani alikwambia kwamba wanateseka? Hilo ni kwa mujibu wa mtizamo wako au.. . Wenzako hatulioni hilo. Kama ni kweli unaona wanyama wanateseka tupatie kwanza namba yako (ref.No. ) katika Chama cha Kuzuia Ukatili kwa Wanyama halafu ndo tuendelee na mjadala.
Kwahyo wakifa wanafurahia?
Wanapokosa chakula na maji na kufa kwa njaa hawateseki?
Mkuu mbona kama unajizima data
 
Kwa taarifa yako, hakuna viumbe wana raha hii dunia kama wanyama.

Kwanza they live their lives to the fullest bila stress.

Pili responsibility kubwa waliyonayo ni kutafuta chakula na kulea watoto ama familia kama wanayo, majukumu ya baba na mama yako very clear.

Tatu wanyama wengi wana life span fupi ambayo inawafanya wasiteseke sana hapa duniani.

Mwisho, usitake kumpangia Mungu namna ya kuuendesha ulimwengu wake, hivyo vitu vyote unavyoviona alitupa sisi wanadamu tuvitumie tupendavyo. Hivyo acha kujitesa na mawazo mfu.
 
Adi uandike hivyo we binadamu una raha gani!? Navyoelewa mimi kila kiumbe chenye pumzi duniani kinapitia kwenye changamoto zake.
 
Kama hujaweza kutoa ref.No. katika chama nilichotaja ina maana wewe sio mkereketwa wa madhila na ukatili yanayowapata wanyama kutokana na harakati zetu sisi wanadamu za kutaka kujiletea maendeleo. i.e. Huna ushirika/umoja na wale wanaowatetea. Kufa ni kitu cha lazima(hakuna kiumbe kilicho hai ambacho hakitaonja Umauti). Ni nani anayesababisha wanyama wakose chakula na maji na hatimaye kufa kwa njaa? Sisi binadamu tunahusika sana -Ndio tulaumiwe na sio Mungu. Ipo kanuni ya survival of the fittest. Kama kiumbe ni kidhaifu, U-Asili( Nature) hukiondoa(kifo)kwa kuwa kinashindwa mpambano.
 
Lakn mm nahc.,....anyway ngoja niache nsije nkaandika tope mkanishangaaa.
 
Kama hujaweza kutoa ref.No. katika chama nilichotaja ina maana wewe sio mkereketwa wa madhila na ukatili yanayowapata wanyama kutokana na harakati zetu sisi wanadamu za kutaka kujiletea maendeleo. i.e. Huna ushirika/umoja na wale wanaowatetea. Kufa ni kitu cha lazima(hakuna kiumbe kilicho hai ambacho hakitaonja Umauti). Ni nani anayesababisha wanyama wakose chakula na maji na hatimaye kufa kwa njaa? Sisi binadamu tunahusika sana -Ndio tulaumiwe na sio Mungu. Ipo kanuni ya survival of the fittest. Kama kiumbe ni kidhaifu, U-Asili( Nature) hukiondoa(kifo)kwa kuwa kinashindwa mpambano.

Mambo ya survival of the fittest, Natural selection na evolution yanamtoa Mungu kwenye equation.

According to Dini, Mungu ndio alituumba Manyanyaso yote na shida zikaanza baada ya kula tunda.

Mungu angeweza isiwepo njaa wala ugonjwa wala kifo.
Lakini kwanini aliwawekea hayo mateso Wanyama?
 
Adi uandike hivyo we binadamu una raha gani!? Navyoelewa mimi kila kiumbe chenye pumzi duniani kinapitia kwenye changamoto zake.
Kwanini hizo changamoto ziwepo? Ni furaha ya Mungu kuona Viumbe alioumba wanateseka?
 
Chui asipokula atakufa, Kazi ya chui ni kuwapunguza swala wabalance ecology
 
Kwa taarifa yako, hakuna viumbe wana raha hii dunia kama wanyama.

Kwanza they live their lives to the fullest bila stress.

Pili responsibility kubwa waliyonayo ni kutafuta chakula na kulea watoto ama familia kama wanayo, majukumu ya baba na mama yako very clear.

Tatu wanyama wengi wana life span fupi ambayo inawafanya wasiteseke sana hapa duniani.

Mwisho, usitake kumpangia Mungu namna ya kuuendesha ulimwengu wake, hivyo vitu vyote unavyoviona alitupa sisi wanadamu tuvitumie tupendavyo. Hivyo acha kujitesa na mawazo mfu.
Wewe mkuu unaishi maisha yako kwa machale mda wote ukiangalia kulia na kushoto kama hakuna simba anayekuvizia??

Wewe ukisikia kiu unaenda tu bombani...Wenzako wanavuka mbuga hadi mbuga wakisaka maji.

Kwanini wanayama wafe?? Walimkosea nini Mungu mpaka wapate adhabu hiyo?
 
Chui asipokula atakufa, Kazi ya chui ni kuwapunguza swala wabalance ecology
Ahaa...kwahyo ilishindikana Chui na Swala wasile vitu tofauti mkuu? ili kuepusha mateso Wanayopata kuwindana?

Hiyo ecology haina njia nyingine ya kuibalance mpaka wauane?
Si Mungu angeweza tu kuweka limit katika kuzaana kwao automatically
 
Ilipangwa hivyo hivyo ni viumbe vya kuliwa
 
Mnyama, ndege, nk hawana hukumu wala hawana nafsi wao biashara yao uisha baada ya kufa
 
Tatizo lako wewe unafikiri sana.punguza kufikiri vitu visivyo na maana
 
Back
Top Bottom