Hivi Wapare makande mnayapendea nini?

Hivi Wapare makande mnayapendea nini?

Yaani ukioa mpare utalishwa makande hadi ukome, yaani imekuwa kama ndo chakula kikuu sijui ndo uvivu wa kupika?

Halafu mzigo unapikwa wa maana mtakula hata siku mbili, unampa hela za matumizi za kutosha lakini makande sasa ishakuwa tabu. Kuna nini kwenye makande.

Hapa naambiwa mme wangu unakula nini mchana huu, ugaliii au makande (hayo makande yalipikwa sijui jana mchana sijui juzi)
ahahaaa tehena petha avae twatonga na bajeti
 
Mimi si mpare ila makande nayapenda, kande limetiwa nazi na sukari,hatari hatari.. Halafu kuna njugu mawe imeungiwa nazi kwa sukari, kisha kuna zile ndizi zilizoiva ziungwe kwa nazi,
Hivyo vitu bimkubwa akivipika tu lazima aniambie nikamtembelee kwake aisee

[emoji39][emoji39]
 
Simple mathematics

Upareni zao kuu linalokubali kushinda mazao yote ni mahindi na maharage

Then what do you expect next?

Wale wali maana mpunga unalimwa sana kwao?
makande au mphure au pure ndio chakula cha asili cha wapare. hiyo ndio sababu ya kwanza kukipenda sana chakula hicho. lakini pia wapare wanaoishi maeneo ya tambarare ya south pare wanalima sana mpunga, hivyo chakula kingine wanachokula ni wali.

ukiacha mphure na wali kwa upande wa wanga, wapare wanapendelea protini za samaki, kondoo, na mbuzi. kuna aina ya mbuzi hapa tanzania wataalamu wanawaita " pare white " wanapatikana katika jamii za wafugaji upareni.
 
Back
Top Bottom