Hivi Wapare makande mnayapendea nini?

Hivi Wapare makande mnayapendea nini?

Yaani ukioa mpare utalishwa makande hadi ukome, yaani imekuwa kama ndo chakula kikuu sijui ndo uvivu wa kupika?

Halafu mzigo unapikwa wa maana mtakula hata siku mbili, unampa hela za matumizi za kutosha lakini makande sasa ishakuwa tabu. Kuna nini kwenye makande.

Hapa naambiwa mme wangu unakula nini mchana huu, ugaliii au makande (hayo makande yalipikwa sijui jana mchana sijui juzi)

Makande nimeyajulia shule ya Boarding.

Kulikuwa na Makande ya aina Mbili ...... Kande kama kande yaani Mahindi+Maharage siku Nyingine Kande Nyama(Mahindi+Nyama).

Kwasasa Nyumbani tunapika mara moja moja kwa mwezi Kande original Plus tui la nazi kisha nakula na parachichi.
 
Itakuwa anapenda unavyojamba,ujue makabila mengine mume ukijamba mkeo anafurahi akijua mumewe umeshiba sana,hiyo inakuwa ndio kama shukrani yako kwake...

BTW makande matam jomonii ukila kwa hamu na ayapike mpishi haswa,utaenjoyy,[emoji39][emoji39]
Really[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]?!
 
Nazi, yaungwe na kitunguu then kando aniwekee nyanya chungu za kukaanga tu bila nyanya wala nini au dagaa wa kukaanga...... Huwa natamani siku hio nisiwe na kazi za usiku maana nalala usingizi mtamu balaa
Tatizo ni nini jamani hadi mna enjoy vitu vya ajabu?!
 
Mimi si mpare ila makande nayapenda, kande limetiwa nazi na sukari,hatari hatari.. Halafu kuna njugu mawe imeungiwa nazi kwa sukari, kisha kuna zile ndizi zilizoiva ziungwe kwa nazi,
Hivyo vitu bimkubwa akivipika tu lazima aniambie nikamtembelee kwake aisee

[emoji39][emoji39]
Now you are talking. Usisahau na ka hiliki kwa mbaali.
 
Yaani ukioa mpare utalishwa makande hadi ukome, yaani imekuwa kama ndo chakula kikuu sijui ndo uvivu wa kupika?

Halafu mzigo unapikwa wa maana mtakula hata siku mbili, unampa hela za matumizi za kutosha lakini makande sasa ishakuwa tabu. Kuna nini kwenye makande.

Hapa naambiwa mme wangu unakula nini mchana huu, ugaliii au makande (hayo makande yalipikwa sijui jana mchana sijui😁
 
Mimi hunichosha na hivi meno husumbua ndo staki kabisa naonaga hayana ladha na hunikumbusha shule bure
Mimi naweza kuwa kibogoyo zaidi yako,natafunia upande mmoja, lakini nikimuona bimkubwa kapika kande, siwezi kuwazia meno [emoji39], ama anipigie simu aniambie leo napika kande lazima 12 jioni niwe kwake... [emoji23]
 
Yaani ukioa mpare utalishwa makande hadi ukome, yaani imekuwa kama ndo chakula kikuu sijui ndo uvivu wa kupika?

Halafu mzigo unapikwa wa maana mtakula hata siku mbili, unampa hela za matumizi za kutosha lakini makande sasa ishakuwa tabu. Kuna nini kwenye makande.

Hapa naambiwa mme wangu unakula nini mchana huu, ugaliii au makande (hayo makande yalipikwa sijui jana mchana sijui juzi)
Hahaha bwasheee shuveeee.

Nitakupa Historia ya Mapande.

Kwetu kuna wasabato wengi. Siku ya Sabato inaanza ijumaa saa 12 na kuisha jumamosi jioni was 12 .

Ndani ya huo muda hawaruhusiwi kupika.
Kwa hio ijumaa wanapika Makande (mpureeeee)
kwenye chungu kikubwa ambayo yataitosha familia kwenye muda wote wa sabato.
 
Imekaa vzr
 
Back
Top Bottom