Hivi Wasafi FM hamna program manager?

Hii redio ndo kwanza sijui ina mwaka mmoja?

Kwa hiyo bado Wanaendelea kuisuka!

Wapeni muda...

Ikibidi kama unajiona Uko presenter mzuri Basi omba nafasi ukaongezee ujuzi....

Siyo kuwasema tuu....
 
Hakuna kitu kinanikera Wasafi kama kumsifia Diamond kupita kiasi na kumuhusisha na kila kitu! Sio vibaya kumsifia mmiliki ila maana hata ITV walikuwa wanafanya hivyo kwa Mengi na Clouds walikuwa wanafanya hivyo kwa Ruge ila isiwe too much, hii ya Wasafi imezidi sana!

Msanii ataenda interview ila utaona watangazaji watajitahidi kumuweka Diamond hata eneo asilostahili,

"....aaah ni takribani wiki mbili zimepita tokea Diamond Platnumz atoe ngoma yake ya iliyotrend na kuweka rekodi tofauti tofauti kwa mfano hadi Jana video yake YouTube ilikuwa na views milioni tatu, huku ikiwa namba moja kwenye mtandao wa boomplay, leo na wewe umetoa wimbo wako, je itakuwa ndio desturi yako kutoa wimbo kila diamond anapotoa?"
 
Ile siku wanazindua masafa ya kahama alikuwepo pm wao daah ile speech yake ilinishangaza sana eti anajisifu kabisa kwenye media yeye ni bingwa wa fitina....hahahaha

Usikivu na ubora wa Wasafi FM Kahama hauna ubora kabisa kama unasikiliza medium wave
 
we unataka atangaze mtu mmoja hao wengine watakula wapi???
 
unitajie redio nyingine inayofanya hivyo, kwanini wabongo hatupendi vitu tofauti

ukitaka elimu nenda redio one TBC huko lazima tujipe space jamani
 
Yaani vipindi watangazaji wanapiga kelele, hamna hata mpangilio. Halafu hakuna ubunifu kabisa. Yaani mtangazaji anakuja studio hajui hata ataongelea nn. Unakuta mtangazaji anasubiri upigwe wimbo wa Diamond halafu mada inaanza hapohapo ili mradi tu
Viongozi wa Wasafi media, kwa kweli watangazaji wenu ni wapuuzi mno...hamna mtangazaji hata mmoja wa maana wote ni majina tu ila kazi hawajuwi hata kidogo. Mna kajamaa hapo kalikuwa EFM Radio kipindi cha michezo, yaani mbwembwe tu na kubana pua. Kaondoka EFM na kile kipindi ndiyo kiko juu zaidi shinda ya yeye alipokuwa pale, hii inaonyesha kuwa jamaa alikuwa hajuwi kazi yake, ni jina tu.
 
Yaani vipindi watangazaji wanapiga kelele, hamna hata mpangilio. Halafu hakuna ubunifu kabisa. Yaani mtangazaji anakuja studio hajui hata ataongelea nn. Unakuta mtangazaji anasubiri upigwe wimbo wa Diamond halafu mada inaanza hapohapo ili mradi tu
Kuna siku nilijiuliza mpk nikashirikisha wenzangu,nikasema wanashindwa hata kumuajiri mtangazaji wa zamani mfano Betty Mkwasa akawabrash,hawaoni azam au radio one walitegemea watangazaji wa zamani na radio au tv zikaendelea vzr
 
Utaskia tu wanasema.
"Babako" bango ni kubwaa",tukae humoo" lock Nene" .

Kwa kweli huwa sijui wanaongea nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…