Hivi Wasafi FM hamna program manager?

Hivi Wasafi FM hamna program manager?

Kinachonishangaza wao ikipigwa nyimbo ya mondi ikiisha ni kuanza kusifu na kuabudu tu na mapambio juu kumuhusu mondi......
Weledi ni kitu muhimu sana kwenye izi kazi....
Anaemuelewa dida anijuze anamuelewaje mie nimeshindwa kabisa kumuelewa naona ni mpiga makelele tu.....

Wasukuma wanasema PUT YOUR MOUTH WERE .............

malizia
 
Tuchape kazi maendeleo hayana chama.. unamsema baba levo
 
Hakuna aliekataa basi unaiga hata kwa marehemu ruge kuibua vipaji vya watangazaji kuliko kujaza watu wa ovyo....
Wewe unawaona watu wa hovyo lakini mtaani kwa wateja hao ndio favorite.

Diamond ana msemo wake '' wape watu kitu wanachotaka".
 
Yes ni habari ya mjini, but inatokana na wanaosikiliza wanataka nn hasa. Wapo watu wanakaa pembeni ya radio ili mradi tu anaisikiliza. But in reality, kwa msikilizaji makini wa radio angependa sana kusikiliza content na pia kumsikiliza mtangazaji anayejua anachokiongea.

Though, hatutaki Wasafi itangaze kama Rtd, lakini tungetamani kuona mtiririko mzuri wa maongezi baina ya wafanyakazi, mada nzuri (japo hizo hizo za kijingajinga lakini zipangike basi), pia watangazaji waachie zamu ya kuongea na kuacha kubishana studio as if wanatangaza vituo tofauti.

Lakini kingine muhimu kupunguza kumsifia sana Diamond. Mimi sidhani kama hicho kituo kilianzishwa kama sehemu ya propaganda ya Diamond, ila kilianzishwa kwa ajili ya wasikilizaji. Then yanatoka wapi mambo ya kumfagilia tu Diamond mwanzo mwisho, kama siyo ushamba flani uliochanganyika na upimbi na ulimbukeni.
Wasafi wanafanya biashara awawezi kupeleka vipindi hewani kufurahisha watu kama wewe wakaacha kundi kubwa ambalo ndio wateja wao royal.

Hivyo vipindi unavyoona havieleweki kuna watu ndio ugonjwa wao wanavipenda ile mbaya.

Hao watangazaji unaoona wa hovyo wanapendwa kuliko watangazaji unaowaona wewe wa maana.

Kikubwa ni pesa kama kitu kinapendwa na kinaleta pesa basi hicho ndio chenyewe.
 
Mi sinaga muda wa kusikiliza radio aisee, yaani ratiba zangu ziko tofauti sana. TV yenyewe naangalia weekend alfajiri tu au football games jioni. Kitu ninachoshukuru ni hii teknolojia ya simu za mkononi, la sivyo sijui ningekwendaje na wakati.
 
Back
Top Bottom