Hivi watanzania wanaohangaikiwa na CHADEMA ni hawa hawa au kuna wengine siwafahamu

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Nauliza tu kwa nia njema.
Hivi hawa Watanzania ambao kila siku tunaambiwa wanahangaikiwa sana mambo ya CHADEMA ni hawa hawa ninaowaona mitaani au kuna kundi jingine ambalo mimi sijawahi kuliona?

Maana mimi naona hawa hawa

wanaokesha kwa Mwamposa
wanaofungua Instagram kila dakika kuangalia Zuchu kajifungua lini, Diamond ka-post nini, mwijaku kasemaje,dotto magari kasema nini.
Ndio wanaotafuta connection ya x wakisikia imevuja
Ndio wanaokwenda Jangwani kuchimba dawa
Ndio wanaosubiri tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva kwa hamu
Ndio wanaonunua tiketi za Color Festival
Ndio wanaojitokeza kwa maelfu kwenye Dodoma Marathon.
Ndio wanaokesha matamasha mengine ya muziki kama vigodoro mitaani

Kwa sababu ukiangalia maisha ya kila siku, watu wengi wanaonekana wako bize na biashara zao, kazi zao, familia zao, mpira, burudani, social media, harusi, kitchen party, graduation, marathon, concert, memes, gossip na mambo mengine ya maisha.

Siasa zipo, zina nafasi yake, lakini wakati mwingine tunaonekana tunakosea kudhani kwamba kila Mtanzania anaamka asubuhi akiwaza chama fulani. Ukweli ni kwamba wengi wanaamka wakiwaza kodi ya nyumba, ada ya mtoto, biashara ya leo, mteja wa kwanza au mechi ya jioni.

Kwa hiyo kabla hatujasema Watanzania wote wanataka tume huru ya uchaguzi, watanzania wanataka samia asishinde kwa asilimia 90 ashinde kwa asilimia 70 ndo anastahili,watanzania wanataka wahuni kwenye maandamano wavamie sheli wachome mwendokasi wavamie maduka ya watu na waachwe , labda tujiulize kwanza... hao Watanzania tunaowazungumzia ni hawa hawa tunaokutana nao kila siku, au kuna Tanzania nyingine ambayo sisi wengine hatuijui?
 
nauliza tu kwa nia njema.

Kwa kuwa umevimbiwa ndiyo maana huoni kinachoendelea
 
Hata hizo biashara na matamasha unayoyasifia yanahitaji katiba bora. Unadhani Color Festival, Dodoma Marathon, au matamasha ya Bongo Fleva yanaweza kuwepo kama nchi haina amani na utulivu wa kisiasa unaotokana na mifumo thabiti?

CHADEMA na wanaharakati wengine wanapambana sasa hivi ili kuweka misingi salama, siasa ndio inayo-shape hiyo daily hustle yako.
 
Ungehoji huo ufisadi mkubwa wa CCM
unaousikia wa mabilioni ndio nchi hiyo hiyo watoto wanakaa chini kwenye vumbi na madirisha hakuna?
 
Back
Top Bottom