Hivi watu Wanaonunua hizi sarafu za zamani huwa wanaenda kuzifanyia nini?

Hua zina kazi katika kupandisha bahati ya uchumi , wengine huzitemgeneza na kuweka dukani, wengine hutengeneza kwa kutembea nazo, wengine hutengeneza kuogea zina kazi kubwa, sababu inaaminika peda ya zamani zilishikwa na watu wengi wa zamani waliokua na bahati tofauti hivyo sababu hao watu asilimia kubwa wamekufa hivyo nyota zao unaweza kuzitumia kwenye peda hizo za zamani
 
Na wanaonunuwa noti chakavu mtaani wanazipeleka wapi?
 
Mmh!! Teh tehee teehee nimecheka sana,ili kupata nyota ya wahenga,watu bhana,wanaimani za ovyo,utakuta hata msomi,anaamini hivyo!!!!🤣🤣
 
Itakuwa mambo ya ushirikina au kuuza kwenye makumbusho za historia
 
Na wanaonunuwa noti chakavu mtaani wanazipeleka wapi?
Benki...wananunua kwa nusu bei ya fedha halisi..noti ya 10000 anakupa 5000, noti ya 5000 anakupa 2500,noti ya 2000 anakupa 1000, noti ya buku unapata 500.

Akifika benki anapewa noti kamili. 10000 iliyochakaa inachukuliwa na anapewa 10000 mpya.

faida Nusu kwa nusu
 
Uwa ni mtandao wa matapeli. Wanaandaa mazingira ya kuzitafuta na kuwalipa vizuri wenye nazo. Baadae sarafu uonekana kutafutwa sana na malipo kuwa makubwa zaidi. Utafutwaji wa sarafu unapofikia kwenye peak mtandao huo huo utatoa sarafu hizo kwa kuwauzia kwa bei kubwa sana warugaruga wanaoamini zina soko mahali na wakitegemea kuvuna faida kubwa sana. Warugaruga wakishazinunua kwa bei kubwa sana na kuwatafuta wanunuzi uambulia patupu maana matapeli wanakuwa wameshafunga biashara.
 
Duh
 
Nafikiri ni biashara ya kubadilisha fedha za zamani na mpya kule BOT
 
Kuna wengine wameibuka wananunua utumbo wa simu ila nyumba yake hawachukui. Wanapita mitaani wakisaka simu mbovu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…