Hivi watu wanaosubiri kutekelezwa kwa hukumu ya kifo, siku au dakika za mwisho huwa wanakuwa katika hali gani?

Hukumu mbaya kuliko zote ni ile ya electric chair bora hizo nyingine, by the way hilo swali tuwaulize pia na wale wagonjwa wa cancer stage ya mwisho, nao wanakuwa wanajua kabisa kwamba baada ya muda fulani they will be no more
Kuna story moja ya dogo anaitwa George Stinney, ni black American alihukumiwa kufa kwa hiyo electric chair, alikuwa na miaka 14 tu. Daah ni story ya kusikitisha sana na kuna movie pia on the same story
 
Inakuwa kawaida tu, kama ulivyo wewe.

Nani asiyengojea kufa?

Panga mipango yako kama haufi na fanya ibada na unyeyekevu kwa Muumba wako kama unakufa sasa hivi.
 
Ni shida kubwa kiutu. Kwa aliyehukumiwa na kwa ndugu zake. Ndio maana kuna kampeni kubwa ya kuondoa adhabu ya kifo. Nchi nyingi tu tayari hazina adhabu hiyo kabisa.
 
Kuna story moja ya dogo anaitwa George Stinney, ni black American alihukumiwa kufa kwa hiyo electric chair, alikuwa na miaka 14 tu. Daah ni story ya kusikitisha sana na kuna movie pia on the same story
Na,la kusikitisha zaidi alikuwa kasingiziwa kutokana na rangi yake ya mwili na asili yake.
 
Hukumu ya kifo haitolewi ili kukuridhisha mfungwa inatolewa kukuadhibu kwanzia wewe famia yako hadi jamii lengo ni kujenga hofu kwa jamii ili wasifanye makosa fulani yenye hukumu hiyo
Mbona kila siku tu watu wanauwa kama vile hii adhabu haipo?Kuna mazingira mtu anau halafu baadae ndio anakuja kujuta mfano kumfumania mke wake au mume wake.
 
Ni shida kubwa kiutu. Kwa aliyehukumiwa na kwa ndugu zake. Ndio maana kuna kampeni kubwa ya kuondoa adhabu ya kifo. Nchi nyingi tu tayari hazina adhabu hiyo kabisa.
Adhabu ya kifo iendelee kuwepo. Kuna watu adhabu hii wanaistahiki kabisa. Wewe unamtazama anayehukumiwa (kwa kustahiki) na familia yake? Kwanini tusiwafikirie victims wake na familia zao?
 
Mbona kila siku tu watu wanauwa kama vile hii adhabu haipo?Kuna mazingira mtu anau halafu baadae ndio anakuja kujuta mfano kumfumania mke wake au mume wake.
Kwa Tz hukumu ipo ila adhabu haitekelezwi Rais huwa hasaini hukumu ya kunyonga maana ili itekelezwe inabidi yeye aweke saini yake
 
Mi nafikiri hakuna binadamu aliyewahi kukizoea kifo. Hata uwe hodari na imani vipi ukiwa na mwili lazima tu kuna point utakiogopa kifo.
 
Kwa nchi kama USA ambayo inatekeleza hukumu hiyo, siku ya mwisho mfungwa anaagiza last meal chakula anachopenda , anatenganishwa na wenzake, na muda mfupi kabla ya kutekelezwa kwa hukumu anaoga fresh lakini pia hukumu huwa inatekelezwa usiku
Niliona clip moja jamaa alikuwa anakula msosi wake wa mwisho akisubiri hukumu ya kunyongwa. Mikono yake ilikuwa inatetemeka balaa huku akila, expresion ya uso wake ukiiona itakutia huzuni sana.
 
Kama uliishi maisha Yako kwa kutendea wengine ubaya ubaya kama dhulma, utapeli,wizi,kudanga wanaume wa watu,kuua,masengenyo,magomvi,umbea umbea,unafiki,na matendo yanayofanana na hayo unakua na hofu kubwa na majuto makubwa sana ktk stage ya mwisho..but

Kama maisha Yako yalikua mazuri I mean umewatendea wengine mazuri unakua kawaida ktk hatua za mwisho Tena unaona mbona wanachelewa kuninyonga hawa nikapumzike!!!
 
Kuna uzi huku uliwahi tolewa umo nadhani bado wa mzee ambaye kazi yake ilikua kunyonga katika magereza ya dodoma yule mzee aliezea kila kitu mule
 
Hukumu mbaya kuliko zote ni ile ya electric chair bora hizo nyingine, by the way hilo s8lwali tuwaulize pia na wale wagonjwa wa cancer stage ya mwisho, nao wanakuwa wanajua kabisa kwamba baada ya muda fulani they will be no more
America depending on state kuna options kadhaa, electric chair, lethal injection, bullet by firing squad etc, to be honest sijaona hata moja yenye unafuu, zote zinatisha!!
Mbaya ni zile ambazo zinafeli wahusika wanachelewa kufa ndani ya muda ulipangwa, hutokea haswa kqenye lethal injection kama combination ya dawa haijafanya kaz inavyotakikana!
 
Hahaha
Nilitamani maisha yangekuwa rahisi hivyo!!!
Bro kuna watu wapo jela na wanahukumiwa adhabu nzito nzito, na hawakuwahi kufanya ubaya wowote.
Just be in the wrong place at a wrong time, unajipata na mirder case, ilhali humjui hata aliyeuwawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…