Hivi wauza mafuta / (petrol, dizeli) ni akina nani nchi hii?

Hivi wauza mafuta / (petrol, dizeli) ni akina nani nchi hii?

CWR2016

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
2,773
Reaction score
6,349
Wana JF,
Wananchi..

Hili ni swali...
Hebu tusaidiane hapa kujua kiunaga ubaga, hawa wauza mafuta Tanzania ni akina nani..

Yani wale wa jumla, na wa rejareja (hizi petrol stations)

Nalenga hasa kupata wenye hisa/ au wamiliki, na marafiki zao...

Naomba tusaidiane tujue kwa sababu, si kosa kujua hela zetu zinaelekea wapi...

Halafu na hawa EWURA, haya mafuta yanayouzwa kwanzia kesho, tarehe 04 May 2022, si yaliagizwa miezi mitatu iliyopita. Hata vita ya Ukreini haijaanza. Sasa Hilo soko la dunia limeathiri vipi?

Hebu
Tuyataje haya ma "sheli" na wamiliki, au marafiki wa wamiliki. Huko ndiko hela zetu zinakopelekwa....tutake tusitake!
 
Mpira ulianza kupigwa mwingi hapa😆

20220503_213855.jpg
 
Nimeshtuka sana bei hizi!! Kuna nini kinaendelea ndugu zangu??
 
Kuna Mwanamke alidiriki kusema, Et tumeshushwa kutoka uchumi wa Kati nakurudi nyuma Si Kwa mapenzi ya mtu Bali mapenzi ya Mungu

Nilichekaaaa, nikajua huyu mtu MNAFIKI
sana, Mungu gan huyo anataka watu waendelee kua Masikini.

Baadae nikagundua, kasema vile, ili ionekane Si Kwa JUHUDI za Magufuli ndo kilifanya Taifa liingie uchumi wa Kati, Bali Mungu , kwa Lugha nyingine, Magufuli kwake hakufanya kazi !!

Hizi ni laana , laana wanazopitia Hawa watu,ndo zinafanya walipe Vijana njaaa Mitandaoni Kumchafua Hayati Magufuli ,asiyechafukika.
 
Hawa GSM nao ni waagizaji na wasambazaji wakubwa , wajanja Wajanja ,,,,,, Timu msoga.

Tayari hapo tumeshapigwa
 
Stock ya miezi mitatu imerudishwa kwanza soko la dunia then ikarudishwa tena duh hii nchi ngumu sana
Vijana wa mama tozo wanaosimamia wizara hiyo walijigamba kwamba Wana mafuta ya kutosha mpaka miez mitatu Sasa saivi mwezi Moja tu yameshapanda bei
 
Baadhi yetu tulipoona baada ya JPM kufariki Ewura, Nemc, Ardhi na Halmashauri zilitoa vibali visivyo maelezo vya ujenzi wa petrol filling stations nyingi yaani baada ya mita hata 300 unakuta vituo hata sita tulifahamu kwamba hii ni moja ya sekta ambayo wale wafanyabiashara wahuni na wajanja wanatega kuja kurudisha pesa zao walizodai zilibanwa enzi za JPM.

Hivi hili la soko ya dunia mbona Zambia na malawi haliwasumbui sana kwa kiwango kilubwa kama sisi. Maguta yamefika 3160 kuanzia kesho na yataendelea kupanda. Tuliaminishwa waziri January kaenda kwenye source ya mafuta ili kuweka mambo sawa tuweze kununua toka kwenye source huko Middle east lakini hakuna uwiano sawa na habari zilizoelezwa baada ya ziara ya waziri uarabuni.

Lazima tukubali kuna shida mahali haswa kwa waziri wetu wa fedha,nishati na ngazi zingine kututoa hapa kwenye recession. Hali itazidi kuwa ngumu haswa tukizingatia hakuna ongezeko la mishahara. Kenya Uhuru amebailout sector nzima ya mafuta haswa waagizaji wa mafuta na juzi amepiga mkwara kampuni ya mafuta ikiwemo Total kwa kuuzia mafuta nchizetu za jirani ili hali maguta hayo serikali ya kenya imeyalipia nusu gharama ili bei zisipande na kuumiza wakenya. Ameongeza mishahara 12%. Hapa kwetu ni uongouongo unaendelea kwa propaganda za bodi ya mishahara ikae ipige hesabu mara jambo letu lipo tuwe wakweli tuu. Msisahau Uhuru ana Economics and political science degree from Amherst College New York swala la akili kubwa linaingia hapa.
 
mmoja anaitwa Lake Oil , mwingine anaitwa Oilcom , wako wengine majina yao nimeyasahau .
Huyu Lake Oil ndio yule wa blue 🔵 blue, masheli makubwa makubwa, na mengi..

Wanahisa ni akina nani, na marafiki tuwajue. Ndio wanaokula hizi mpya za EWURA..
 
Kuna Mwanamke alidiriki kusema, Et tumeshushwa kutoka uchumi wa Kati nakurudi nyuma Si Kwa mapenzi ya mtu Bali mapenzi ya Mungu

Nilichekaaaa, nikajua huyu mtu MNAFIKI
sana, Mungu gan huyo anataka watu waendelee kua Masikini.

Baadae nikagundua, kasema vile, ili ionekane Si Kwa JUHUDI za Magufuli ndo kilifanya Taifa liingie uchumi wa Kati, Bali Mungu , kwa Lugha nyingine, Magufuli kwake hakufanya kazi !!

Hizi ni laana , laana wanazopitia Hawa watu,ndo zinafanya walipe Vijana njaaa Mitandaoni Kumchafua Hayati Magufuli ,asiyechafukika.
Naomba kukupa taarifa nenda u "gugu" in Amos Makalla's voice. Au ingia website ya World bank, Tz haijashushwa rank ya kiuchumi.
Kuna kitu kundi la Mama wanakiandaa, na wanakijua wao wenyewe na kina Madelu Mwigulu ..
 
Ni sawa na kumwambia ahamie Zambia, hii ni kauli ya kijinga sana umeitoa..
Hapana,maana ya ndani ya kauli yangu ni atuwekee Bei ya mafuta duniani,gharama za miundo mbinu ya kuuza mafuta,yaani ikiwemo na mishahara ya wafanyakazi
 
Kuna Mwanamke alidiriki kusema, Et tumeshushwa kutoka uchumi wa Kati nakurudi nyuma Si Kwa mapenzi ya mtu Bali mapenzi ya Mungu

Nilichekaaaa, nikajua huyu mtu MNAFIKI
sana, Mungu gan huyo anataka watu waendelee kua Masikini.

Baadae nikagundua, kasema vile, ili ionekane Si Kwa JUHUDI za Magufuli ndo kilifanya Taifa liingie uchumi wa Kati, Bali Mungu , kwa Lugha nyingine, Magufuli kwake hakufanya kazi !!

Hizi ni laana , laana wanazopitia Hawa watu,ndo zinafanya walipe Vijana njaaa Mitandaoni Kumchafua Hayati Magufuli ,asiyechafukika.
Kila mtu ana uchafu wake...hakujatawaliwa na malaika nchi hii...mazuri na mabaya yapo.
 
Nchi hii Ina watu wapumbavu, mtu hajui mafuta yanatoka nje ya nchi
 
Masikini hulalamika kuwa matajiri ndio hawafanyia maisha magumu wasijue ni jinsi wanavyoishi maisha yao wenyewe
 
Hatimaye mafuta yamepanda bei, kabla ya "pekeji" ya mishahara.
 
Back
Top Bottom