Hivi wauza magari wa JF wanaishi dunia gani?

Hivi wauza magari wa JF wanaishi dunia gani?

Madalali huwa wanapiga bei yoyote hata mara nyingine mara mbili ya bei bila kujua kanuni za angalau 5%, 7% na ikienda sana 10%
Wauza magari wengi hapa JF sio madalali na nadhani hawajui bei halisi za nagari ya mkononi
Wanauza kwa bei ambayo hata dalali akikuletea gari Kama hiyo hiyo yenye vigezo vinavyofaanana kabisa hawezi kukuuzi hiyo bei.. Wanauza juu mno
 
Mwenye website ndiyo itakuwa kazi yake kuhakiki. Tuseme unauza kiwanja, unawasiliana naye. Yeye anakuja mpaka ''site'' na anajihakikishia kuwa documents zote unazo ndiyo anaweka tangazo lako. Hata aki-charge fee kubwa lakini mnunuaji awe na uhakika kuwa anakwenda kununua mali ya uhakika na siyo kutoka kwa matapeli. NB: mwenye website anatakiwa awe na connection kubwa ya watu kufuatilia na kuhakiki kila sehemu eg Ardhi etc..
NB: mwenye website anatakiwa awe na connection kubwa ya watu kufuatilia na kuhakiki kila sehemu eg Ardhi etc
 
Niwekee bei elekezi mkuu yanaweza kuzungumzika
Ukiwa ready kwa gari unayohitaji unanijulisha ukinipa Specs nafatilia nakupa bei ukiweza unalipia gari baada ya kuiona imefika Tunduma hapo nanunua kwa pesa yangu nakuletea ila nafanya hivi kwa magari yalio sokoni ili gari ikifika zikiwa hadith za Mwalimu nyingi nabadilishana na hela hapo nageuza zangu..
 
... Shida sana, yaani kila mnada unaoingia unapokelewa na 'TUGBOATS' na ushuru wake hupandisha bei ya bidhaa mara kumi! ... Madalali wanaua biashara BONGO!
 
Tajiri auze gari lake milioni 10, msururu wa madalali zaidi ya watano kila mmoja kaweka cha juu million 2! Mwisho mununuzi anapambaniwa kwa milioni 25😂😂😂😂 gari linadoda 😂😂😂
Hahaha Madalali ni watu wenye tamaa sijawahi kuona, mtu Hana hela na wala maali si yake lakini anataka kufaidika kwanza yeye
 
Ukiingia kwenye jukwaa la JF Garage katika JamiiForums, utadhani wauza magari wa kule wanaishi kwenye ulimwengu wa njozi au uchumi wa nchi ya kufikirika.

Malalamiko kuhusu bei zisizo na uhalisia za magari ya JamiiForums (JF) ni ya muda mrefu, na wateja wengi wanahisi wauzaji hao wanakadiria bei kwa kuangalia "hadhi" ya jukwaa badala ya thamani halisi ya soko na hali ya gari lenyewe..!
Wanazani Critical thinker hadi mifukoni!!.
 
Yaani Niache kumchukua fundi wangu mzuri Kisha tukalenge magari pale magomeni mapipa badala yake nianze kuhangaika na wauzaju wa humu wenye mibei ya ajabu ajabu nimerogwa au !?
Oya mzee wangu hivi tunaweza lenga starlet au vits kwa hela ya honda click?
 
Wanatamaa za fisi, weka angalau cha juu laki mbili tatu ili biashara itembee chapu, sasa mtu anaweka cha juu milioni kadhaaa mwishoe biashara inabuma!!
Aisee wale jamaa ni nyoko, bidhaa ya Milioni 10 wao wanatembea na 15M, kwa kuwa wao ndio hukutana na wateja wewe unakuwa hujui kwanini hupati wateja na wanachoongea hukijui
 
Kwa wanaohitaji gari zozote za kuagiza na chasis za yard msisite kunicheki wakuu kikubwa tu ujue kuwa hakuna huduma ya bure ila kuna hali ya unafuu na ubinadamu.

Pia nawakaribisha wenye mizigo ya kuexport na kuimport kupitia Dar port to Burundi, congo, zambia, malawi, uganda, Rwanda na kwingineko.
 
Back
Top Bottom