Hivi wauzaji wanaoongea na simu wakati mteja unasubiri huduma ndo wamiliki wa biashara au nao ni waajiriwa?

Hivi wauzaji wanaoongea na simu wakati mteja unasubiri huduma ndo wamiliki wa biashara au nao ni waajiriwa?

Kumbe na wewe umeliona hili?
Leo asubuhi nimepita kwenye duka moja nikamkuta jamaa mmoja teenager hivi, nikawa namuuliza bidhaa fulani kama ipo jamaa akawa yupo bize kuongea na mtu wa nje kuhusu mpira, nikamuuliza mpaka mara tatu hata hanijali yupo bize " Nawaambia simba hamfiki popote labda arudi yesu"
Nikaona niondoke zangu labda pale sio dukani ni kijiwe cha kuzungumza mpira.
Kiukweli nimegundua hivi vitu huenda fan, talent au acquired knowledge.
###Mteja ni mfalme!
Hakuna Cha ufalme shida yako ndo imekupeleka pale. Hata hivo maamuzi ulo chukua ni sahihi kabisa. Hupaswi kulalamika wakati ulikua na option ya kwenda kupata huduma kwingine.
 
Hakuna Cha ufalme shida yako ndo imekupeleka pale. Hata hivo maamuzi ulo chukua ni sahihi kabisa. Hupaswi kulalamika wakati ulikua na option ya kwenda kupata huduma kwingine.
mimi kwangu mteja sio mfalme.

siwez kuacha kuongea na simu kisa mteja anahitaji huduma.kwani akieleza nini anataka kweny huduma yangu siwez kumuelewa?

tatizo lililopo ni ni ujinga tu wa watu baadhi kushindwa kuelewa nini maana ya busara.
 
Hakuna Cha ufalme shida yako ndo imekupeleka pale. Hata hivo maamuzi ulo chukua ni sahihi kabisa. Hupaswi kulalamika wakati ulikua na option ya kwenda kupata huduma kwingine.
Nataka nikufundishe kitu, hapa naona hujaongea kwa kufikilia ila UMEROPOKA.( samahani kwa maneno makali but you deserve it!.
Msemo/Kauli ya mteja ni mfalme hutumiwa na wafanyabiashara wakimaanisha kuwa mteja ndio mtu ambae anaifanya biashara yako ikupe faida hivyo kumfanya aridhike na huduma yako au bidhaa is something you can't escape if you’re serious with your business.
Sasa kanunua mzigo kaweka dukani auze apate faida alafu mteja anamtreat in a way that sounds like "Kama unataka nunua kama hutaki nenda sehemu nyingine " ukitreat wateja kumi hivyo wote wakawa wanakukwepa means umepoteza mauzo ambayo ungeyapata kwa kuwa treat like kings which doesn't cost you anything.
It's simple to please people just make them feel important, kwisha.
 
Sometimes wateja wana visirani vyao tu, ukiwa kama mtoa huduma huwezi kua perfect na kuhudumia kwa usawa wateja wote.
Wateja wengine mizinguo tu.
Hapana it comes with training, train yourself as companies train their customer care.
Piga simu Yas, Airtel, vodacom, tanesco, au Taasisi yoyote waambie upuuzi wowote au visilani vyako uone kama watakujibu vibaya!

Huu ni upuuzi hakuna ex excuses huu ni upuuzi
 
mimi kwangu mteja sio mfalme.

siwez kuacha kuongea na simu kisa mteja anahitaji huduma.kwani akieleza nini anataka kweny huduma yangu siwez kumuelewa?

tatizo lililopo ni ni ujinga tu wa watu baadhi kushindwa kuelewa nini maana ya busara.
Wewe umeona hiyo ni busara, nimekuja unaongea na simu kata, hudumia mteja!
Heshimu kazi yako, heshimu wateja.
 
Kumbe na wewe umeliona hili?
Leo asubuhi nimepita kwenye duka moja nikamkuta jamaa mmoja teenager hivi, nikawa namuuliza bidhaa fulani kama ipo jamaa akawa yupo bize kuongea na mtu wa nje kuhusu mpira, nikamuuliza mpaka mara tatu hata hanijali yupo bize " Nawaambia simba hamfiki popote labda arudi yesu"
Nikaona niondoke zangu labda pale sio dukani ni kijiwe cha kuzungumza mpira.
Kiukweli nimegundua hivi vitu huenda fan, talent au acquired knowledge.
###Mteja ni mfalme!
Watu hawajielewi aisee.....

Yaani mpaka unabaki mdomo wazi....

Yale machanjo ya corona huenda yamewafanya watu kuwa misukule .... huwa nastaajabu sana.
 
Kuna wateja wanaweka order zao kwa kutumia simu alafu unataka akatiwe usikilizwe wewe na umemkuta…
 
Zero customer care!, kuna kila haja ya kufundisha watu customer care wiki mbili zilizopita nilienda kwenye mgahawa nikakuta wahudumu wanalumbana mbele ya wateja huku nao wakiwa wamekaanao!!, nilifikiri ile situation nikaona kabisa hapa ni zero!.
nilitaka nimuambie yule mkubwa lkn nikaona nisije kushushuliwa maana unaweza sikia "hebu nawewe kula uende zako mengine hayakuhusu!"🤣
Si unajua tena wabongo tena wadada!.

but customer care ni muhimu kwenye biashara yoyote na muda mwengine inaweza kukupelekea pakubwa bila wewe kujua!, japo mwengine anaweza kudharau!. all in all bosses kuweni na mtindo wakutoa maarifa kwa mnaowaachia biashara zenu nawewe ulieachiwa ama kuajiliwa ni muhimu kuwa kind kwa unaowahudumia.
Point ya msingi
 
Wakati mwingine nyie mnao jifanya mpogo sahihi ni wajinga, vitu vingine unahitaji busara ya kawaida Sana ya Nini ku complect mambo kiasi hiko.?

Huyo unae mtuhumu ana ndugu ana ana marafiki na ana hisia. Pengine unakuta unae mtuhumu kapigiwa na shangazi, dada, mama, kaka na hata rafiki pengine kapigiwa smu mda ambao alikua free, inakua ningumu mtu kumkatia simu ghafla lazima umtegee Kisha um- please sio ghafla kiasi hicho kaka.

Unapo kua na angalau na punje ya busara na hekima jaribu kuangalia hisia za mwenzako sio kila kitu kulalamika tu kama Janamke.

Mfano leo kuna mzee mmoja namfahamu hanaga mishe yeye nikama mji wake mke wake ndo mtafutaji, yeye kawa wale wazee wa mitaani (balozi) sasa Leo saa 3 asubuhi nikamkuta mtaani mie nilikua kwenye harakat zangu bahati mbaya nikawa nimemskia anasema. "Huyu wa saluni hajafungua mpaka saiv ana hela Sana, watu wengine biashara hawazijui wanadhani biashara nizao kumbe niza wananchi bila sisi biashara hazipo".

Nikasema hili lizee kazi kulalamika lenyewe biashara yake iko wapi.? Au hajui Kama kina dharula, yule mzee na wewe mtoa post ni wale wale.
Hizi zote ni excuses.
Na nimegundua elimu yako ni ndogo sana!
 
Hapana it comes with training, train yourself as companies train their customer care.
Piga simu Yas, Airtel, vodacom, tanesco, au Taasisi yoyote waambie upuuzi wowote au visilani vyako uone kama watakujibu vibaya!

Huu ni upuuzi hakuna ex excuses huu ni upuuzi
Yaani uje kipuuzi halafu utegemee nikupe sijui customer care ya Yas sijui voda huko??
Mkuu labda kama hujawahi kufanya biashara na kashkash za wateja huzijui.
Wengine ni majaribu tu, hata hao wa mitandao ni vile hawawaoni hao customers ila kingekua kinawaka, na mbona hata wao wakiona hueleweki wanakata simu.

Ukiwaendekeza wanakupanda kichwani na kukutangazia mbovu kwa wengine, mpe makavu kesho harudii.
Kaja dukani kwako kwakua nae ana shida na mnasaidiana.
Na yeye mteja afate taratibu ulizojiwekea dukani kwako, sio kwakujifanya yeye ni mfalme basi atake umtreat vile anataka yeye hata kama ni nje ya utaratibu wako.
 
Back
Top Bottom