Hivi wazazi wanaolipaga polisi wawapigie watoto wao huwa wana lengo lipi?

Hivi wazazi wanaolipaga polisi wawapigie watoto wao huwa wana lengo lipi?

R-K-O

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2023
Posts
482
Reaction score
2,178
Nyumba unakuta ina baba lakini cha ajabu wanamlipa polisi eti aende kutoa hukumu

Nachojua suala la kutoa displini huwa linafaa zaidi mzazi ndio ashughulikie tena iwe kwa lengo la kumfunda mtoto na si kumuumiza.

kwa maana hii ni kwamba ukimkodi mtu akuchapie mtoto wako, impact huwa ni ndogo.

Hawa wazazi huwa wana lengo lipi ?
 
Au kumpeleka kwa mwalimu akamuadhibu kwa kosa lililo ndani ya mamlaka ya mzazi mwenyewe hivi tunakwama wapi?
 
Nifikiri ni mfo wa ukisasa sana lakini ni mbaya sana Haifai kwa utamaduni wa kwetu.

Yapasa mtoto awe treared na mama/ baba
 
Biblia inasema usimnyime Mtoto fimbo/bakora

Waswahili nao wanasema Samaki Mkunje angali Mbichi.

Suala la malezi ya watoto limekuwa changamoto kwa Wazazi wengi hasa baada ya kuanza kuwasomesha hizi shule za kwenda na Mabasi ya Njano

Lakini pia Wazazi wengi kukosa muda wa kukaa na watoto wao kwa kisingizio cha ubusy wa kazi na utafutaji, ukija kutahamaki unakuta Mwanao ni nunda kuanzia shuleni hadi nyumbani kwako.

Kwakuwa hukumjengea mazingira ya kumuadhibu anapofanya makosa, inakulazimu umpeleke kituo cha Polisi kwaajili ya kuadhibiwa.

Binafsi Watoto wangu wanapofanya makosa, nimekuwa nikiwaadhibu barabara huku nawaeleza makosa yao ili siku nyingine wasirudie kuyafanya.

Changamoto iliyopo ni kwa Mama zao kutowaadhibu hadi Baba ninaporudi, utasikia subiria Baba yako arudi akuchape. Imagine nimepata safari ya kikazi ya Wiki 1 huku nyumbani mtoto aadhibiwi eti hadi nirudi.

====================
Miaka ya zamani wakati nakua ilikuwa ukifanya kosa hata Mzee wa Jirani anakuadhibu akigundua umefanya kosa na Mzazi wangu/wako atapewa taarifa juu ya kosa ulilofanya.


Tupunguze kuwalea watoto Kimayai mayai
 
Hao tunawaita wazazi mcharuko, wengine hulaza watoto selo kwa matarajio wakitoka hawatawasumbua. Ni upumbavu tu wa kunyanyasa watoto
 
Nyumba unakuta ina baba lakini cha ajabu wanamlipa polisi eti aende kutoa hukumu

Nachojua suala la kutoa displini huwa linafaa zaidi mzazi ndio ashughulikie tena iwe kwa lengo la kumfunda mtoto na si kumuumiza.

kwa maana hii ni kwamba ukimkodi mtu akuchapie mtoto wako, impact huwa ni ndogo.

Hawa wazazi huwa wana lengo lipi ?
Watu hudhani kuzaa ni suala la akili,kuzaa ni maimbile tu hata mgonjwa akili ana uwezo huo
 
Back
Top Bottom