Biblia inasema usimnyime Mtoto fimbo/bakora
Waswahili nao wanasema Samaki Mkunje angali Mbichi.
Suala la malezi ya watoto limekuwa changamoto kwa Wazazi wengi hasa baada ya kuanza kuwasomesha hizi shule za kwenda na Mabasi ya Njano
Lakini pia Wazazi wengi kukosa muda wa kukaa na watoto wao kwa kisingizio cha ubusy wa kazi na utafutaji, ukija kutahamaki unakuta Mwanao ni nunda kuanzia shuleni hadi nyumbani kwako.
Kwakuwa hukumjengea mazingira ya kumuadhibu anapofanya makosa, inakulazimu umpeleke kituo cha Polisi kwaajili ya kuadhibiwa.
Binafsi Watoto wangu wanapofanya makosa, nimekuwa nikiwaadhibu barabara huku nawaeleza makosa yao ili siku nyingine wasirudie kuyafanya.
Changamoto iliyopo ni kwa Mama zao kutowaadhibu hadi Baba ninaporudi, utasikia subiria Baba yako arudi akuchape. Imagine nimepata safari ya kikazi ya Wiki 1 huku nyumbani mtoto aadhibiwi eti hadi nirudi.
====================
Miaka ya zamani wakati nakua ilikuwa ukifanya kosa hata Mzee wa Jirani anakuadhibu akigundua umefanya kosa na Mzazi wangu/wako atapewa taarifa juu ya kosa ulilofanya.
Tupunguze kuwalea watoto Kimayai mayai