Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 25,725
- 78,589
Nmeona umeweka profile ya MTU mweupe so inaonekana wee unapendelea vyeupe nahii inaonyesha naww nimweupeeee hahahhshshshshsh khantweHee kivipi tena mi ndo najijua bwana
Haaaaaaahhh aya buana ,, lkn Mimi nipo pale pale ,, wewe nimweupeeeeeeeSijamweka kwa sababu ni mweupe. Huyo dada ni mwigizaji wa kikorea nampenda sana
Exactly ladySiku hizi kuna hadi Herbal lightening cream,yaani wamejua serikali inapinga kwasababu ya madhara ya kiafya sasa wanakuwekea picha au hata kutumia papai na parachichi na ndani kuna hydroquinone inayokuchubua.
Tatizo letu ni kulazimisha vitu jamani,mwanaume kama anavutiwa na weupe muachie huyo mwanaume weupe waliozaliwa hivyo,gharama ya kujichubua na matokeo ya hizo kemikali hakuna mwanaume mwenye thamani hiyo. Si hawa wa sayari hii.Kesho hushindwi kumkuta na baamedi mweusi.
Ndio Mimi mtu mzm ila ubongo ndo wakitoto !! Wewe nimweupeeeeeNaona umeamua kucheza. Nlijua najibizana na mtu mzima mwenzangu
Heeeee kidding bana ,,usije ukanimezaNdio Mimi mtu mzm ila ubongo ndo wakitoto !! Wewe nimweupeeeee
sure mkuu! Watu weusi waliopo marekani wanajaribu kukumbuka walikotoka...majina kama Sasha ni watu weusi kwa kule, sasa dadaako huku achelewi kujiita Daisy....!Shukrani naendelea kujifunza
Majina tuitwe sisi aibu uone weweAibu mno!
Tena sasa hivi nadhani huo mtindo ndo umeshika kasi sana.
Zamani walau moja ya majina ya mtu lilikuwa lazima liwe lile la ukoo.
Lakini siku hizi sivyo kabisa.
Ukitaka kuliona hilo kwa wingi basi angalia matokeo ya mitihani ya wanafunzi wa shule za sekondari au angalia orodha ya wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu.
Yaani mtu unayasoma hayo majina hadi unaanza kuona aibu kabisa.
Ndiyo maana wachina, wazungu, waarab wanatucheka sana kwa kutuletea kemikali zilizo oza huku Afrika. Pia inashangaza unaweza ona mwanamke jeusiiii limevaa wigi ya kijani, nyekundu, njano, sielewi wanaona uzuri gani. Yaani baada ya kuonekana mzuri anakuwa anatisha kuwa a zombie.
Well said mkuuNdiyo, kwenye jamii nyingi, hususan za watu weusi [walio na asili ya Afrika] rangi nyeupe ya ngozi huhusishwa na urembo.
Naamini ni ukweli ambao watu wengi hatuupendi, lakini ndo hivyo tena. Ukweli mara nyingi huwa ni mchungu na tulio wengi huwa tunajitahidi kuukataa waziwazi.
Hapo juu umezungumzia watu kujichubua ili kujibadili rangi ya ngozi na wawe weupe zaidi. Vipi kuhusu nywele bandia zilizonyooka? Ina maana nywele asilia za kipilipili ni mbaya, siyo?
Na vipi kuhusu majina ya kigeni siku hizi?
Unakuta mtu anaitwa Anthony Francis wakati baba ni Mgogo na mama ni Mnyiramba!
Au Maxwell John wakati baba ni Mmakonde na mama ni Mzaramo!
Hiyo mifano inanileta kwenye hoja ya kuhusisha Uafrika na uduni na Uzungu na ubora.
Hata watu wenye tabia za kishenzi huwa tunawaita 'waswahili'. Halafu tabia flani flani zinazoonekana au kudhaniwa kuwa ni za kistaarabu ndo zinaonekana ni za 'kizungu'.
Ni ndivyo tulivyo tu.
Mkuu naona ili swalaa linakukeraa sanaaa...by da way unaongea factSijawahi kusikia sababu yoyote ile iliyo na mashiko.
Nyingi ambazo huwa nazisikia huwa hazina mashiko kabisa.
Naweza kusema nyingi ya hizo sababu zinatokana na ujinga [ignorance] tu.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]Wengine hawataki kufahamika makabila yao [emoji23] [emoji23] [emoji23] mfano ukiona Sanga unajua tu ni nani