Hivi weupe ndio urembo au?

Hivi weupe ndio urembo au?

Siku hizi kuna hadi Herbal lightening cream,yaani wamejua serikali inapinga kwasababu ya madhara ya kiafya sasa wanakuwekea picha au hata kutumia papai na parachichi na ndani kuna hydroquinone inayokuchubua.
Tatizo letu ni kulazimisha vitu jamani,mwanaume kama anavutiwa na weupe muachie huyo mwanaume weupe waliozaliwa hivyo,gharama ya kujichubua na matokeo ya hizo kemikali hakuna mwanaume mwenye thamani hiyo. Si hawa wa sayari hii.Kesho hushindwi kumkuta na baamedi mweusi.
 
Nmeona umeweka profile ya MTU mweupe so inaonekana wee unapendelea vyeupe nahii inaonyesha naww nimweupeeee hahahhshshshshsh khantwe
Sijamweka kwa sababu ni mweupe. Huyo dada ni mwigizaji wa kikorea nampenda sana
 
Siku hizi kuna hadi Herbal lightening cream,yaani wamejua serikali inapinga kwasababu ya madhara ya kiafya sasa wanakuwekea picha au hata kutumia papai na parachichi na ndani kuna hydroquinone inayokuchubua.
Tatizo letu ni kulazimisha vitu jamani,mwanaume kama anavutiwa na weupe muachie huyo mwanaume weupe waliozaliwa hivyo,gharama ya kujichubua na matokeo ya hizo kemikali hakuna mwanaume mwenye thamani hiyo. Si hawa wa sayari hii.Kesho hushindwi kumkuta na baamedi mweusi.
Exactly lady
 
Shukrani naendelea kujifunza
sure mkuu! Watu weusi waliopo marekani wanajaribu kukumbuka walikotoka...majina kama Sasha ni watu weusi kwa kule, sasa dadaako huku achelewi kujiita Daisy....!
Wamarekani weusi wana tamasha la kukumbuka asili yao kwa jina linaitwa "Kwanza festival" Derived from Swahili word "Mti wa kwanza" wakimaanisha asili.
 
Kujichubua hata kwa watu wenye ngozi nyeupe hasa waAsia kupo sanaa...uzuri wanaona ni pale unapokua mweupe zaidi...
To me uzuri sio mchubuo kwa kweli..uzuri wa ngozi ni bringing the best out of the skin shade you have kwa ngozi kuwa na rangi moja,smooth,youthful na yenye afya...
 
Aibu mno!

Tena sasa hivi nadhani huo mtindo ndo umeshika kasi sana.

Zamani walau moja ya majina ya mtu lilikuwa lazima liwe lile la ukoo.

Lakini siku hizi sivyo kabisa.

Ukitaka kuliona hilo kwa wingi basi angalia matokeo ya mitihani ya wanafunzi wa shule za sekondari au angalia orodha ya wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu.

Yaani mtu unayasoma hayo majina hadi unaanza kuona aibu kabisa.
Majina tuitwe sisi aibu uone wewe
 
Ndiyo maana wachina, wazungu, waarab wanatucheka sana kwa kutuletea kemikali zilizo oza huku Afrika. Pia inashangaza unaweza ona mwanamke jeusiiii limevaa wigi ya kijani, nyekundu, njano, sielewi wanaona uzuri gani. Yaani baada ya kuonekana mzuri anakuwa anatisha kuwa a zombie.

Waarabu na mhindi wenyewe wanajichubua tu. Tena mwarabu ukimwambia u look like white anafurahi sana.
 
Waafrika tujue kuwa vyovyote tufanyavyo kutaka kuwa kama wazungu mfano urembo, majina na utamaduni, kamwe hatuwez kuwa wazungu milele na milele. unajichubuaje wakati ngoz nyeusi haizeeki haraka. Ndo maana wanasema Blacks dont crack. mcheki Usher, will smith, etc Lakini tujue kadri tunavoelimika na kujua historia yetu ndo tutarud tulipotoka. tuboreshe tulivyonavyo.
 
Ndiyo, kwenye jamii nyingi, hususan za watu weusi [walio na asili ya Afrika] rangi nyeupe ya ngozi huhusishwa na urembo.

Naamini ni ukweli ambao watu wengi hatuupendi, lakini ndo hivyo tena. Ukweli mara nyingi huwa ni mchungu na tulio wengi huwa tunajitahidi kuukataa waziwazi.

Hapo juu umezungumzia watu kujichubua ili kujibadili rangi ya ngozi na wawe weupe zaidi. Vipi kuhusu nywele bandia zilizonyooka? Ina maana nywele asilia za kipilipili ni mbaya, siyo?

Na vipi kuhusu majina ya kigeni siku hizi?

Unakuta mtu anaitwa Anthony Francis wakati baba ni Mgogo na mama ni Mnyiramba!

Au Maxwell John wakati baba ni Mmakonde na mama ni Mzaramo!

Hiyo mifano inanileta kwenye hoja ya kuhusisha Uafrika na uduni na Uzungu na ubora.

Hata watu wenye tabia za kishenzi huwa tunawaita 'waswahili'. Halafu tabia flani flani zinazoonekana au kudhaniwa kuwa ni za kistaarabu ndo zinaonekana ni za 'kizungu'.

Ni ndivyo tulivyo tu.
Well said mkuu
 
Sijawahi kusikia sababu yoyote ile iliyo na mashiko.

Nyingi ambazo huwa nazisikia huwa hazina mashiko kabisa.

Naweza kusema nyingi ya hizo sababu zinatokana na ujinga [ignorance] tu.
Mkuu naona ili swalaa linakukeraa sanaaa...by da way unaongea fact
 
Back
Top Bottom